Subscribe:

Sample text

Sample Text

Monday, 8 March 2021

A hali tunazingatia ukweli.

A.Hali tunazingatia ukweli wa Yn.8:31-32 ambao ni sharti la kuwa mwanafunzi wa kristo kwelikweli, safari yetu ya kufuatilia roho hizi ianze 1Yoh.4:6. Aya hii inatuonesha jinsi kweli anavyochukua nafasi ya mungu akiwa mmiliki wa roho ambaye anasigana na roho ya upotevu ambayo katika 1kor.2:12 imeoneshwa kuwa roho ya dunia. Kwa kadiri ya Yn.8:23 na Yn.8:44 roho ya dunia ni ibilisi aliye mwuaji tangu mwanzo wala hakusimama katika kweli,asemapo uongo anasema yaliyo yake mwenyewe,maana yeye ni mwongo na baba wa uongo. Kwa sifa yake hii, huyu roho ya dunia ndiye ambaye katika 2kor.4:3-4 anaitwa mungu wa dunia au katika Yn.12:31;14:30 na 16:11 anaitwa mkuu wa ulimwengu huu. Hapa ndipo inapolala Siri ya ukweli wa post hii, kwamba kuamini uwapo wa shetani, ibilisi, majini na uchawi ni ishara ya kuwa waangalifu kwa uwepo wa adui ambaye angalikwamisha baraka zetu. Paulo mtume anatuambia Wana juhudi kwa mambo ya mungu lakini si katika maarifa.