Subscribe:

Sample text

Sample Text

Wednesday, 4 October 2017

MAELEZO KUHUSU NURU NA GIZA


Maelezo yanayopatikana katika Bibilia Takatifu toleo la Iringa kuhusu aya Yn.8:12 yatuelezea kwamba Nuru na Giza ni kielelezo cha falme mbili zinazohitilafiana na kupigana; yaani ufalme wa mema unaotawaliwa na Kristo na Ufalme wa uovu unaomilikiwa na shetani.
Maelezo yanatueleza kwamba kila ufalme unajaribu kuushinda mwingine. Na kwamba watu wanagawanyika baina ya wana wa Nuru na wana wa giza kwa kadiri waishivyo. Kwa mvuto wa Nuru, Kristo au kwa mvuto wa giza shetani.
Maelezo yanahitimisha kwa kusema kwamba wana hao wote watambulikana katika vitendo vyao.
Kwa upande wa Mungu wa pekee wa kweli, Bibilia yenyewe hutuambia kwamba Mungu hutaka watu wote waokolewe na kupata kujua yaliyo kweli (1Tim.2:4).
Kwa upande wa shetani, 2Kor.4:3-4 hutueleza kwamba iwapo Injili yetu imesitirika, imestirika kwa hao wanaopotea ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini isiwazukie (wasiione) Nuru ya Injili ya Utukufu wake Kristo aliye Sura yake Mungu.
Na Yn.12:40 yatueleza “Amewapofusha macho na kuifanya mizito mioyo yao; wasije wakaona kwa macho yao, wakafahamu kwa mioyo yao, wakaongoka nikawaponya (kwa kuwaokoa).
Kumbe tuko katika mkabala wa vita vikali. Mungu wa pekee wa kweli anataka watu waijue kweli ili waokoke. Shetani yeye hataki watu waijue kweli wasije wakaokolewa na kuponywa.
Hebu, ndugu yangu, jipime mwenyewe mbele za Mungu wa pekee wa kweli ukiwa mwenye moyo wa kweli kwa utimilifu wa imani. Kama huna muda na Neno la Mungu, kama Neno la Mungu kwako ni jambo la ziada tu, au ikiwa kwako kutafuta kweli ya Mungu ni kupoteza wakati ambao umepewa na Mungu, basi tambua kwamba Yule mwovu yuko kazini kwa maangamizi yako ya milele yote.
Mbaya zaidi ni pale mtu, kwa kutumia cheo, huwa kizingiti kwa wengine kuitafuta kweli. Mtu kama huyo hujithibitisha kwamba ni mtumishi wa shetani. Kwake mtu huyo kile kiapo “Namkataa shetani, na mambo yake yote, na fahari zake zote”, ni kiapo cha uongo, unafiki na ubatili mtupu. Na ibada yenyewe huwa ni ibada ya kujisajiri kwenye ufalme na utumishi wa Shetani.
Hapo moja kwa moja zile laana zilizosemekana katika Yn.8:44 na 20:29 huwa halisi kwa mhusika. Mhusika huwa mmilikiwa wa shetani.
Hivyo mtu kuwa mtumwa wa dhambi, hasa dhambi ile kuu ya kutomwamini Mungu (Mk.11:22), dhambi ya kumfanya Mungu mwongo (1Yn.5:10) huwa ni kitu cha kawaida, si cha ajabu kwake.
Wakati uliokubalika wa kufuta usajili batili kwa shetani ndiyo sasa. Kufanya kosa siyo kosa. Kosa ni kuendelea na kosa.
Kuijua kweli ndicho Mungu anachokutaka (1Tim.2:4) na kukuagiza (Yn.8:31-32). Kamwe usimruhusu shetani aendelee kukukamata katika ujinga kwa maangamizi yako na ya wengine.
Ubarikiwe!!
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0714 118 428
0787 765 759
0753 298 707
chamayombe37@gmail.com

0 comments:

Post a Comment