JE, MBINGUNI YA MUNGU PEKEE WA KWELI IKO WAPI? Tumehakikishwa kwamba Mungu pekee wa kweli ni Umoja wa Nafsi Tatu: (1) Kweli (Yn.3:33; 8:26; 1Yoh.1:1-3), (2) Neno (Yn.1:1-5; 1Yoh.1:1-3) na (3) uzima au Roho (Yn.6:63).
1Yoh.5:8 hututhibitishia kwamba Nafsi Tatu hawa hukaa mbinguni katika hali ya umoja usiogawanyika.
Kwa mantiki hii tuna kila haki ya kuamini kwamba (1) Nafsi Kweli hukaa katika Nafsi Neno na Nafsi Uzima au Roho; (2) Nafsi Roho au Uzima hukaa katika Nafsi Kweli, na Nafsi Neno; na (3) Nafsi Neno naye hukaa katika Nafsi Kweli na Nafsi Uzima au Roho.
Kifupi ni kwamba kila Nafsi miongoni mwao hukaa katika kila Nafsi miongoni mwao.
Hivyo, wanaoshuhudia mbinguni iliyo maskani au kao la Nafsi hao watatu ni Umoja wa hao Nafsi Tatu miongoni mwao. Umoja wa Nafsi Tatu ndio mbinguni halisi anakokaa Mungu Umoja wa Nafsi Tatu: Kweli, Neno na Uzima (1Yoh.5:8).
Hivyo Nyumba ya Mungu tunayoikuta Ebr.10:21, Efe.2:19, Hekalu na Maskani tunayokuta katika Efe.2:21 na 22 na Patakatifu tupatapo katika Ebr.10:19 si chochote kile bali Umoja wa Nafsi Tatu za Mungu pekee wa Kweli na ndiyo mbinguni wanakokaa Nafsi Tatu za Mungu pekee wa kweli.
Tamani kuingia mbinguni leo kwa njia ya Kristo Neno la Mungu aliye katika Utatu Mtakatifu, na aliyetuombea kwamba pale alipo na sisi tuwepo (Yn.17:24). Yeye ndiye aliye Njia, Kweli na Uzima (Yn.14:6) na ndiye Mwombezi wetu (Yn.17; Rum 8:34; Ebr. 7:25; 1Yoh.2:1). Hakuna Mwombezi wa uhakika na aliyelipa fidia ya kukubalika kwa Baba ila Yeye tu.
Hatuna cha kufanya ila kumshukuru Mungu kwa wema, huruma, ukarimu, uwezo na upendo wake bila mipaka yoyote katika yote. (Efe.3:20). LUKA ROKI CHAMAYOMBE 0714118428 www.chamayombe.blogspot.com
1 comments:
JE, MBINGUNI YA MUNGU PEKEE WA KWELI IKO WAPI?
Tumehakikishwa kwamba Mungu pekee wa kweli ni Umoja wa Nafsi Tatu: (1) Kweli (Yn.3:33; 8:26; 1Yoh.1:1-3), (2) Neno (Yn.1:1-5; 1Yoh.1:1-3) na (3) uzima au Roho (Yn.6:63).
1Yoh.5:8 hututhibitishia kwamba Nafsi Tatu hawa hukaa mbinguni katika hali ya umoja usiogawanyika.
Kwa mantiki hii tuna kila haki ya kuamini kwamba (1) Nafsi Kweli hukaa katika Nafsi Neno na Nafsi Uzima au Roho; (2) Nafsi Roho au Uzima hukaa katika Nafsi Kweli, na Nafsi Neno; na (3) Nafsi Neno naye hukaa katika Nafsi Kweli na Nafsi Uzima au Roho.
Kifupi ni kwamba kila Nafsi miongoni mwao hukaa katika kila Nafsi miongoni mwao.
Hivyo, wanaoshuhudia mbinguni iliyo maskani au kao la Nafsi hao watatu ni Umoja wa hao Nafsi Tatu miongoni mwao. Umoja wa Nafsi Tatu ndio mbinguni halisi anakokaa Mungu Umoja wa Nafsi Tatu: Kweli, Neno na Uzima (1Yoh.5:8).
Hivyo Nyumba ya Mungu tunayoikuta Ebr.10:21, Efe.2:19, Hekalu na Maskani tunayokuta katika Efe.2:21 na 22 na Patakatifu tupatapo katika Ebr.10:19 si chochote kile bali Umoja wa Nafsi Tatu za Mungu pekee wa Kweli na ndiyo mbinguni wanakokaa Nafsi Tatu za Mungu pekee wa kweli.
Tamani kuingia mbinguni leo kwa njia ya Kristo Neno la Mungu aliye katika Utatu Mtakatifu, na aliyetuombea kwamba pale alipo na sisi tuwepo (Yn.17:24). Yeye ndiye aliye Njia, Kweli na Uzima (Yn.14:6) na ndiye Mwombezi wetu (Yn.17; Rum 8:34; Ebr. 7:25; 1Yoh.2:1). Hakuna Mwombezi wa uhakika na aliyelipa fidia ya kukubalika kwa Baba ila Yeye tu.
Hatuna cha kufanya ila kumshukuru Mungu kwa wema, huruma, ukarimu, uwezo na upendo wake bila mipaka yoyote katika yote. (Efe.3:20).
LUKA ROKI CHAMAYOMBE
0714118428
www.chamayombe.blogspot.com
Post a Comment