Subscribe:

Sample text

Sample Text

Sunday, 2 September 2018

NI LIPI KANISA LA KRISTO NENO LA MUNGU

Itakumbukwa kwamba ile mada yetu tuliyoipa jina "KANISA LA KRISTO NENO LA MUNGU" ilitufikisha tu kwenye sifa 4 za Kanisa; Kwamba Kanisa hilo ni Moja, Takatifu Katoliki na la Kimitume.  Lakini kuna haja ya kulijua Kanisa lenyewe lenye sifa hizo ni lipi.
Kamusi ya Biblia hutufahamisha kwamba neno "Kanisa" chimbuko lake ni neno la Kigiriki "Ekklesia" lenye maana "Mkutano" au kusanyiko au unganiko.
Ile mada yetu "MJUE MUNGU PEKEE WA KWELI" imetufikisha kwenye ukweli kwamba Mungu pekee wa kweli ni Roho aliye katika Umoja wa Nafsi Tatu; Kweli, Neno na Uzima au Roho Mtakatifu.
Umoja huu wa Nafsi Tatu huashiria "MKUTANO" au "UUNGANIKAJI" wa wale "NAFSI TATU" kuwa UMOJA usiogawanyika.  Kwamba, hawa Nafsi Tatu wamekutanika, wamekusanyika na kuunganika kuwa Umoja usiogawanyika.  Hawa watatu ni Mkutano, Unganiko, Jumuiko, au Jumuiya, Ekklesia, ni "KANISA".
Hivyo, "Kanisa", kama Jumuiko, au Mkutano (Ekklesia) wa Nafsi Tatu si kitu cha kuchukuliwa kiwepesiwepesi tu.  Kanisa au Mkutano au Unganiko hilo la Nafsi Tatu ni Mungu Kweli mwenyewe katika Umoja wa Nafsi zake Tatu.  Kweli, Neno, na Uzima au Roho wa Kweli.  Mungu pekee wa kweli, Roho aliye katika Umoja wa Nafsi zake tatu, ndiye Kanisa mwenye zile sifa 4, kwamba ni Moja, Takatifu, Katoliki na la Kimitume.

SIFA YA NNE NI YA "KIMITUME"
Sifa ya nne ya Kanisa la Kristo Neno la Mungu ni kwamba Mitume walitekeleza Utume wao kikusanyiko au kijumuiya, kama tunavyoona katika Nyaraka zao kwa Makusanyiko au Jumuiya za Mungu Kweli zilivyokuwa pale na pale.  Mitume walikuwa vyombo vya Mungu kueneza Jumuiko au Mwili wa Mungu pekee wa kweli aliye Jumuiko au Mkutano, yaani, Kanisa la Nafsi Tatu za Mungu Kweli.
Kwa msaada na utendaji wa Roho wa kweli waliyeahidiwa kwamba atawaongoza awatie kwenye Kweli yote (Yn. 16: 12-13), na ambaye walimnyweshwa kiukweli na kiuhalisia baada ya kutukuzwa kwake Kristo. (Yn. 20:21-22; 4:10, 14; 7:37-39).  Mitume walilieneza Neno la Mungu litakasalo na kuwakamilisha watu wa Mungu kwenye Mikutaniko (Makanisa) yao pale na pale.  Neno lililo Kweli ya Mungu ndilo lililotawala katika Makanisa.  Zingatia maangalisho na mafundisho ya hapa na pale.

KUHUSU IBADA ZA KIDINI, MITUME WAMETUAMBIA NINI?
Katika Kol. 2:23 wanatuonya dhidi ya Ibada za kujitungia wenyewe ambazo hazifai kitu kaw kuzizuia tamaa za mwili zilizosembekana katika Gal. 5: 19-21 na penginepo pengi tu.  Katika (Ebra. 10:11) tunaambiwa kuhusu Ibada wanazozitoa kila mara makuhani ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.  ZIngatia maonyo yao katika Rumi 10:4; Gal. 4:8-10; 5:4-5; 5:16-17; Kol. 2:8-10; 2:16-23.  Katika ufu. 14:4 na 8 tunasisitiziwa ukweli wa unajisi au uzinifu ambao watu wanaufanya na ibilisi dhidi ya Mungu kweli kwa njia ya ibada za Kidini.  Rejea na ile mada yetu "Mungu wa pekee wa kweli haendani na Ibada za Kidini."

WADU WA KANISA LA KRISTO NENO LA MUNGU, WOTE NI WAPAKWA MAFUITA
Wadau wa Kanisa la Kristo Neno la Mungu wote, bila ubaguzi wowote ule, ni wapakwa mafuta sawasawa na (1Yoh. 2:20, 27)/ Wala mafuta hayo si ya mitishamba bali Roho wa kweli aliye Mwalimu (Yn. 14:26), Kiongozi (Yn. 16:13), wenye kufunulia yote katika Kristo Neno la Mungu (1 Kor. 2: 10-14). Roho huyo hupatikana kwa ubatizo katika Roho (Yn. 1:33; 1Kor. 12: 13). Bila Roho huyo wa Kweli hakuna awezaye kuwa mdau wa Kanisa la Kristo Neno la Mungu (Efe. 2:18-22) (Rum. 8:9), maana hakuna ayafahamuye mambo ya Mungu, ila Roho atokaye kwa Mungu.  Ndiyo maana Roho wa Kweli ni wa lazima katika kufahamu tuliyokirimiwa na Mungu (1 Kor. 2:11-12).

HITIMISHO
Tumalize kwa sisitizo kwamba Kanisa si chochote kile bali Mungu pekee wa Kweli mwenyewe katika Utatu wake Mtakatifu.  yeye ndiye kutaniko (Kanisa) la Nafsi Tatu na hata kuwa Mwili mmoja.  Na ni mapenzi yake ya milele yote kwamba uumbaji wake woke uungwe katika Yeye aliye Kanisa au Mwili mmoja, ijapokuwa yuko katika Nafsi Tatu.
Nikuhimize wewe mpenzi au mpenzi mtarajiwa wa Mungu Kweli kung'ang'ana katika Kanisa au Mwili huu wa Mungu Kweli, iwapo umekwisha kuungwa nao.  Na kama bado, basi sasa ni wakati wa kuachana kabisa na ibada ambazo ni uzinzi na ibilisi dhidi ya Mungu Kweli.  Ibada hizo ambazo zinaelekezwa kwa viumbe badala ya Mungu Kweli mwenyewe ni chukizo ni unajisi, ni uzinizi dhidi ya Mungu pekee wa kweli amabaye ndiye Mume wetu halali (Isa. 54:5). Tena Jima lake ni Mungu mwenye wivi (Kut. 34:14).
Ubarikiwe kwa kuitubu na kuiacha kabisa dhambi hii, bila hoja au kisingizio chochote kile ambacho ni kwa hasara ya nafsi yako mwenyewe na nafsi za wezio unaohusiana nao kwa namna moja au nyingine.
Yote yakiwa si kwa sifa na utukufu wa yeyote ule; bali kwa sifa na utukufu wake huyu Mungu pekee wa kweli katika Umoja usiogawantika wa Nafsi zake Tatu, sasa na milele yote.

LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE

0787 - 765759
0714 - 118428
0753 - 298707

info.chamayombe@gmail.com
www.chamayombe.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment