Subscribe:

Sample text

Sample Text

Tuesday, 31 December 2019

KUMJUA YULE MWIVI (YN.10:10) NA MWOVU (1YOH.5:19)

Ile habari tuliyoitafakari katika mada yetu "MWIVI NA KRISTO NENO LA KWELI".  Imefufikisha kwenye ukweli unaosemekana katika 1Yoh 4:6. Kwamba wapo Roho wa Kweli na Roho wa Upotevu .
1Yoh 5:19 Hutuambia kwamba dunia hukaa katika yule Mwovu .Ukweli huu unasemekana kwa namna nyingine katika 2Kor.4:3--4 Kuhusu "Mungu wa dunia "anayepofusha fikra za watu isiwazukie Nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Muumba mbingu na dunia.
Tumekwisha kuona kwamba Neno "MUNGU"  limebuniwa na Mtu wa kuasi .Mwana wa uharibifu .Yule mpingamizi  ajiinuaye nafsi yake juu ya Kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa (2Thes.2:3--4)
Tumeona kwamba Muumba amejihakikishia kwamba Yeye ni Umoja usiogawanyika wa nafsi Tatu :Kweli ,Neno la Kweli na Uzima wa milele .
Huyu ni Baba wa wote,Wala hana  hoja ya kujiinua nafsi zake katika chochote kile Wala kuabudiwa .Manabii wametuhakikishia jinsi Muumba wetu anavyochukia kuabudiwa
Kutokana na ukweli kwamba katika maskani ya mbinguni "Mungu"hayumo ,na kutokana na Ukweli kwamba "Mungu " hutokana na Mtu wa kuasi haiwezekani Muumba wetu atam ulikane kwa Jina hilo mbali na vile alivyojishuhudia mwenyewe ,Mungu hana nafasi yoyote katika maskani ya Muumba wetu.Mbinguni .Na Muumba wetu hana chochote katika Mungu.Kutokana  na Kweli hizi ni dhahiri kwamba. Mungu ndiye MWIVI aliyesemekana katika. Yn.10:10
Huo ndiyo ukweli ,dunia inatawaliwa na Mwivi ,Ibilisi Yn8:44  Dunia Inamwabudu na kumwomba Ibilisi ili Ipate Nini kama siyo maangamizi tu?

Tuzinduke usingizini .Tupokee Ufufuko Kristo atuangaze (Efe.5:14)Tukae katika Neno lake tu Yn.8:31---32.Humo  ndimo ulimo Uzima na usalama wetu

0 comments:

Post a Comment