Miongoni mwa maswala nyeti ambayo Papa Yohani Paulo II aliagiza
yajifunzwe kwa upya ni swala la Mama yetu Bikira Maria (The Call for
Christian Unity (Kifungu cha 79).
Katika uhalisia wa mambo ni
kwamba ubinadamu unakabiliwa na tatizo la utumwa wa dhambi unaotokana na
dhambi ambayo imepelekea ulimwengu huu kuwa chini ya miliki ya Yule
mwovu.
MPANGO WA UKOMBOZI
Mshahara wa dhambi ni mauti (Rumi
6:23). Watu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu
(Rumi 3:23). Hivyo, kiuhalisia watu wote wamekufa, ni maiti.
Ili
kurejesha uzima, ilibidi Yeye mwenyewe arudi ndani ya mtu wake
aliyejifarakanisha kwa kumwamini Yule mwovu. Na haiwezekani arudi ndani
ya mtu wake hali dhambi ingalimo ndani yake.
Katika hali yake ya
umauti, na kutokana na hali ya dhambi kuwa ukuta au kiambaza kati yake
Mungu na mtu wake, mtu hawezi kufanya lolote lile kujikwamua kutoka
utumwa wa dhambi.
Ndipo Yeye mwenyewe akamua kushiriki ubinadamu,
ili Yeye mwenyewe katika hali ya kibinadamu amharibu shetani
(Ebr.2:11-17), kuifuta na kuiondoa dhambi isiwepo tena; na hivyo kufuta
enzi na mamlaka ya shetani (Kol.2:13-15).
Kukamilisha kusudio
hili la kushiriki hali ya kibinadamu, akamteua Bikira Maria, ambaye
amekubali na kubarikiwa kwa utakaso na kuingiwa na Roho Mtakatifu. Na
kadiri ya 1Yoh.4:13, kwa huko kushirikishwa Roho Mtakatifu, Bikira Maria
akawa ndani ya Mungu na Mungu ndani ya Bikira Maria, akawa umoja na
Mungu katika Utatu wake Mtakatifu, tayari kutimiza kazi ya ukombozi kama
ilivyokusudiwa.
Hivyo katika kutimiza kazi ya ukombozi Bikira Maria hayuko nje ya Mungu katika Utatu wake Mtakatifu.
BIKIRA MARIA MAMA MZAZI WA WAZALIWA MARA YA PILI
Bikira Maria ni Mama wa Yesu ambaye ni Neno la Mungu aliyefanyika Mwili (Yn.1:14).Tumboni mwa Bikira Maria.
Wale ambao kiuhalisia wanaambiwa “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili kwa
mbegu isiyoharibika, kwa Neno la Mungu lenye uzima lidumulo hata milele
(1Pet.1:23); hao ndio wale wanaosemekana katika Ebr.2:11, “Maana Yeye
atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja; kwa ajili hii
Yesu haoni haya kuwaita ndugu zake.
Atakasaye ni Neno
aliyefanyika Mwili. Wanaotakaswa ni hao waliozaliwa mara ya pili kwa
Neno la Mungu lidumulo hata milele. Wote wamezaliwa na Neno la Mungu.
Neno la Mungu ndiyo mbegu ya kiume iliyowazaa. Ni ndugu, ni makaka
“Brothers)” siyo “Half-Brothers”).
Maadamu sisi nasi tumezaliwa
kwa Neno la Mungu, Yesu Neno la Mungu aliyefanyika Mwili tumboni mwa
Bikira Maria, sisi tuliyezaliwa kwa Neno la Mungu nasi tulikuwa naye
tumboni mwa Bikira Maria. Alipomzaa Yesu katuzaa pamoja na Yesu.
Hivyo, kiuhalisia, Bikira Maria ni Mama yetu mzazi wala si mama wa Kambo.
BIKIRA MARIA WA MLIMA KARMERI NA BIKIRA MARIA WA FATIMA
Je, Bikira Maria anayehusika na matumizi ya Skapulari iliyoandikwa,
“Whoever dies wearing this Scapular will never suffer eternal hell” na
Bikira Maria wa Fatima aliyetuhimiza kusali rosari, ni Bikira Maria wa
kweli?
Tumeagizwa kuzipima roho, maana kuna Roho wa kweli na roho
ya upotevu (1Yoh.4:1, 6). Bikira Maria wa kweli kamzaa Yesu wa
kuwaokoa watu wake kutoka utumwa wa dhambi (Mt.1:21). Sasa Bikira Maria
anayehimiza taratibu ambazo hazisaidii kitu kuokoa watu kutoka utumwa
wa dhambi, huyo anaweza kuwa Bikira Maria wa kweli? Je, huyo atakuwa
nje ya Yule mwasi ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho mungu au
cha kuabudiwa? Yule ambaye huketi hata katika hekalu la Mungu,
akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu? (2thes.2:4)
Kwenye Mabanda ya Huduma ya Kufunguliwa, wanapelekwa watu wenye mapepo
ambao wamevaa rosari na Skapulari. Kama vitu hivi vina nguvu ya Mungu
pekee wa kweli, mapepo yanaishije na watu waliovaa vitu hivi? Na kama
yanaweza kuishi nao wanovaa vitu hivi, yatashindwaje kuwasindikiza
kuzimu mwishoni mwa maisha yao hapa duniani?
Ikiwa ibada
wanazoenenda nazo (kuungama, kuhudhuria Misa, kukomunika, kutoa zaka na
sadaka) hazifai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili (Kol.2:23;
Gal.5:19-21), yaani, hazifai kitu kulikabili tatizo la utumwa wa dhambi.
Ibada hizo anapofanyiwa akiisha kufa zitapata wapi nguvu ya kuweza
kutatua tatizo la dhambi?
Hivi, ibada hizi haziishii kuwa mchezo
wa kuigiza tu? Nakubaliana na agizo la Papa Yohani Paulo II kwamba tuwe
waaminifu kwa Injili tuwe na fikira mpya, mtazamo mpya wa mambo na
wongofu wa kina.
Kwa usalama wetu tuzingatie agizo hili ambalo
linatokana na Mtaguso wa Vatikani II. Mungu anataka watu wote waokolewe
na kupata kujua iliyo kweli (1Tim 2:4). Maana watu wake wanapotea kwa
kuwa hawajui Maandiko wala uwezo wa Mungu (Mt.22:29). Na njia ya kujua
kweli ni kukaa katika Neno lake; ndipo tutakapo kuwa wanafunzi wake Yesu
kiukweli, na kujua kweli itakayotuweka huru (Yn.8:31-32).
Ibada hizo kwa Bikira Mria ni ibada zilizo laaniwa kwa sababu
• Ziki nje kabisa ya injili iliyohubiriwa na mitume wa Kristo Neno la MUNGU.
• Zinawapambanisha Kristo Neno la Mungu mbaye, kwa kadiri ya mapango wa
MUNGU, ndiye Mwombezi( Rum.8:26-27,34; ebr.2:17; 7:25; 1Yoh.2:1-2).
• Kadiri ya 1Yoh.4:13, Bikira Maria ni mshiriki wa umoja wa nafsi tatu
za MUNGU. Hivyo ,fikra za kumchomoa Bikira Maria awe nje ya utatu
mtakatifu wa Mungu ni fikra farakanishi amabazo ni za yule mwovu.
Hatupaswi kuafikiana naye.
Ni ujumbe kutoka kwa nduguyo katika
Neno la Mungu, la Mungu aliyefanyika Mwili kututoa kwenye utumwa wa
dhambi. Tumshukuru kwa Roho Mtakatifu.
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0714 118 428
0787 765 759
0753 298 707
Email: chamayombe37@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



0 comments:
Post a Comment