Subscribe:

Sample text

Sample Text

Wednesday, 4 October 2017

TANZANIA KUKUMBWA NA TETEMEKO LA KIROHO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

Tanzania ambayo kihistoria imekuwa na sifa ya kuwa nchi ya amani, hata kuwa kimbilio la wakimbizi, sasa amani iko katika tetemeko la kutisha nchini Tanzania.
NANI WA KULAUMIWA?
Hili ni tetemeko ambalo liko katika ulimwengu wa roho. Tendo lolote la kulichukulia tetemeko hili kimwilimwili, tendo hilo litakuwa ni tendo la kumwabudu Yule mwovu aliye Baba wa Uovu (Kol.2:18). Na ni hatari kubwa.
Maelezo Na.3 ya Yn.8:12 ya Bibilia Takatifu toleo la Iringa hufafanua usemi wa Kristo Neno la Mungu kwamba Yeye amekuja kuwa Nuru ya Ulimwengu, na kwamba yeye amfuataye hatkwenda gizani kamwe, bali atakuwa na Nuru ya Uzima.
Maelezo Na.3 yanasomeka kama ifuatavyo: “Nuru na giza ni kielelezo cha falme mbili zinazohitilafiana na kupigana, yaani Ufalme wa Mema utawaliwao na Kristo, na Ufalme wa uovu unaomilikiwa na shetani. Kila ufalme unajaribu kuushinda mwingine. Watu wanagawanyika baina ya wana wa Nuru na wana wa giza kadiri waishivyo, kwa mvuto wa Nuru Kristo au kwa mvuto wa giza shetani. Wana hao wote watambulikana katika vitendo vyao”.
Kuhusu hao wawili wanaopambana, Biblia yenyewe hutuambia “Basi nasema, Nendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho na Roho kushindana na mwili kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka (Gal.5:16-17)”.
Gal.5:19-21 hutuorodheshea matendo ya mwili ambayo ni uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, UADUI, UGOMVI, Wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na kwamba wayatendao mambo ya jinsi hii hawataurithi ufalme wa Mungu.
Kinyume chake, Gal.5:22-23 hutuorodheshea tunda la Roho ambalo ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole kiasi.
NAFASI YA MAOMBI NA MAOMBEZI
Wewe na mimi tunakabiliwa na hawa wawili wapiganao ambao wanatugombania. Huyu hutaka tuwe maskani au Hekalu lake, na huyu hutaka tuwe kiti chake: 1Yoh.3:8a hutuambia kwamba atendaye dhambi (atendaye yale yaliyo orodheshwa katika Gal.15:19-21) ni wa Ibilisi.
Na anayemilikiwa na Ibililisi hukaliwa na Ibilisi kuwa kiti chake. Katika hali hiyo, mhanga hupofushwa; na moyo wake hufanywa kuwa mgumu kuiona na kufahamu iliyo kweli asije akamwongokea Mungu Kweli akamponya Yn.12:40; 2Kor.4:3-4).
Ndiyo maana Yn.8:47 hutuambia kwamba asiye wa Mungu Kweli hayasikii maneno ya Mangu kweli. Na kwa sababu ya kumilikiwa huko na Yule mwovu, Mungu Kweli hamsikii mhanga au mmilikiwa wa Yule mwovu (Yn.9:31). Kwa sababu hiyo, kulikurupukia swala la maombi na maombezi, ni kupoteza wakati na nyenzo katika ujumla wake. Watu wataomba na kuombea; lakini wataishia kuwa wambea.
MAPASWA YALIYOKO MBELE YETU
Kukubali kukusanywa kundi moja na Jemedari mmoja tu (Yn.10:16; 11:52). Vinginevyo, tunaambiwa katika YBS.34:23-24. “Iwapo mtu mmoja anajenga, mwenzake akabomoa, je! Faida yao ni nini ila kazi bure tu? Iwapo mtu mmoja anaomba, na mwingine analaani; Je! Bwana ataisikia sauti ya yupi?” Hivyo, katika vita hivi dhidi ya Ibilisi tunapaswa kuwa wamoja sawasawa na Neno la Mungu Efe.4:3-6.
Ili kuufikia Umoja huo tunapaswa kunyweshwa (1Kor.12:13) na kuvalishwa (Gal.3:27) utimilifu wote wa Mungu katika Kristo Neno la Mungu Kol.2:10; Efe.3:19). Ili hili lipate kutimilika, tunapaswa kulenenda kwa jinsi ya Kristo tukiwa tumeachana kabisa na kila kilicho cha kibinadamu, wala mafundisho ya awali ya ulimwengu (Kol.2:8-10). Kwenda kwa jinsi ya Kristo ndiko kule kwenda kwa imani 100% (Gal.5:4-5). Kwenda kwa jinsi ya Kristo ndiko kule kuenenda kwa Roho (Gal.5:16) sawasawa na mapenzi ya Mungu ambaye hutafuta watu wamwabudu katika Roho na kweli (Yn.4:23-24; 1Yoh.5:14-15).
KWA ANGUKO LA ADAMU NA EVA, WATU WOTE NI WA IBILISI (1Yoh.3:8a)
Kutokana na ukweli wa mambo ulivyo, watu wote wamekuwa wa Ibilisi kwa dhambi ya Adamu na Eva. Lakini kwa upande wa mpiganaji wa upande wa pili ni kwamba kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa (Ebr.10:14). Na utakaso umetimilika kwa kutolewa Mwili (Nafsi) wa Kristo Neno la Mungu mara moja tu (Ebr.10:10); ambamo ndani yake mna maji safi na hai yaliyomo katika Damu ya Yesu, Roho Mtakatifu (Yn.7:37-39) aliyemo katika Neno la Mungu (Ebr.10:19-22; Yn.17:17, 19; Efe.5:25-27).
Utakaso ni kule kuondolewa kwa ule mlima farakanishi ambao Yule mwovu ameupandikiza ndani yetu kuharibu mahusiano na mawasiliano na Mungu Kweli. Mlima huo unapoondolewa, ndipo Mungu huwa ndani ya nafsi ya mtu na nafsi ya mtu ndani ya Umoja wa Nafsi Tatu za Mungu Kweli. Hapo mtu huwa Umoja na Mungu. Mungu huwa ndiye Mtendaji Mkuu ndani ya nafsi ya mtu. Hapo ndipo nafsi ya mtu katika kuwa umoja na Nafsi Tatu za Mungu huwa mshindi na zaidi ya mshindi dhidi ya Ibilisi (Rum.8:37).
SIRI YA UMOJA UNAOTAKIWA, IMO KATIKA KUPOKEA HIYO ZAWADI YA UTAKASO
ambao hufuatiwa na kukamilishwa katika Umungu. Isisahaulike wala kupuuzwa kwamba pale Msalabani Kristo Neno la Mungu alionja mauti kwa ajili ya kila mtu; bila kujali dini, jinsia, umri, cheo, wala chochote kile kiwacho. Ni kwa ajili yako hapo kama ulivyo, na mimi hapa kama nilivyo.
Tumeona hapo juu kwamba Kristo Neno la Mungu alionja mauti kwa ajili ya kila mtu. Kristo Neno la Mungu alikufa kutuokoa kutoka utumwa wa dhambi ili atuweke huru kweli kweli (Mt.1:21; Yn.8:36) maana atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi (Yn.8:34).
Wasomi wa Bibilia tunaona kwamba kila akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila atendaye dhambi hakumwona wala hakumtambua (1Yoh.3:6). Na katika Kol.2:23 tunaambiwa kwamba ibada mnazojitungia wenyewe ambazo hazifai kitu kuzizuia tamaa za mwili zile zilizo- orodheshwa katika Gal.5:19-21.
Sasa sisi tunataka tuwe na ujasiri mmoja wa kumkaribia Mungu wetu kuhusu hili janga analotuletea Ibilisi. Tusipoteze ukweli kwamba Kristo Neno la Mungu Kaonja mauti kwa ajili ya kila mmoja wetu. Lengo la kufanya hivyo ni kututoa kwenye utumwa wa dhambi tuweze kuhusiana na kuwasiliana na Mungu katika Umoja wake wa Nafsi Tatu (Yn.17:21-23; 1Yoh.4:13).
Kwa kusimama katika aya hizi Kol.2:23 na Gal.5:19-21) kiukweli, bila uongo wala unafiki wowote mbele za Mungu Roho (Yn.4:24) katika Umoja wa Nafsi Tatu. “Kweli, na Neno, na Roho Mtakatifu, zipime ibada zinazoendeshwa kwenye dini au dhehebu lako lolote lile, je zinafaa chochote kuzizuia tamaa za mwili zilizoorodheshwa katika Gal.5:19-21? Kama jibu la kweli ni ndiyo mbele za Mungu Kweli basi ni vema na vizuri sana! Jibu likiwa hapana; basi ujue kwamba uko hatarini; kwani imekuwa kwamba uko mbali na Mungu.
Lakini hiyo isikutishe. Iko faraja kutoka kwa Mungu. Kwamba bado una uhai huu wa mwili wa nyama hata sasa ni kwa sababu Mungu kweli hapendi wewe upotee, bali kwamba umwongokee Yeye uwe mzima (2Pet.3:9). Na siku na wakati uliokubalika wewe kupata msaada wa Roho Mtakatifu, ni sasa.
Hivyo, nakuomba wewe rafiki yangu mpendwa wa Kristo Neno la Mungu, uliye mpenzi wa kujiunga katika jeshi la Kristo Neno la Mungu kuuangamiza ufalme wa Ibilisi kwako, kwa Tanzania na dunia katika ujumla wake, na kuomba kwanza ya yote kupokea zawadi au neema ya ondoleo la dhambi au utakaso kwa njia ya imani ya 100% (Mk.11:23) kwamba umeoshwa kwa maji safi na hai yaliyomo katika Damu ya Kristo Neno la Mungu, Roho Mtakatifu aliyemo katika Neno la Mungu ambaye ndiye Mwombezi wetu mbele za MUngu kweli.
Jambo hilo lifuatiwe na Ukweli kwamba Mungu kweli amesema, kwa Utakazo huo sasa amekushirikisha utimilifu wote wa Umungu wake. Kama Yeye alivyo ndivyo ulivyo na wewe duniani hapa (1Yoh.4:17); na kwamba dhambi zako na uasi wako uliopita hataukumbuka tena hata milele (Rum.3:25; Ebr.10:17).
Katika hali hiyo ya amani na Mungu kweli, sasa kwa nafsi yako mshukuru Mungu kwa ajili yako, kwa ajili ya Taifa letu Tanzania na kwa dunia katika ujumla wake.
UBARIKIWE SANA!!!
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0787 765 759
0714 118 428
0753 298 707
Chamayombe37@gmail.com

2 comments:

Unknown said...

Baba umebarikiwa sana, endelea kutupa NENO.

said...

Ex wangu alinisababishia maumivu mengi na nimevunjika moyo na kuharibiwa tangu wakati huo. Nimewasiliana na wachawi wengi na wananinyang'anya pesa bila matokeo yoyote. Nilituma barua pepe nyingi sana nikitafuta uchawi wa kweli hadi nikaelekezwa na mwanamke wa miaka 45 ambaye Dk DAWN aliwahi kusaidia hapo awali, bila kujua niliwasiliana na Dk DAWN ingawa sikuamini, lakini baada ya kufanya kile alichoelezea, nilifuata maagizo yangu. ex alirudi kwangu akiniambia nimsamehe na nikamsamehe na leo nina furaha na ndoa yangu. Unaweza kuwasiliana na Dk DAWN kupitia barua pepe kwa ( dawnacuna314@gmail.com ) au kupitia WhatsApp kwa (+2349046229159) na jaribio litakushawishi.

Post a Comment