Tanzania ambayo kihistoria imekuwa na sifa ya kuwa nchi ya amani,
hata kuwa kimbilio la wakimbizi, sasa amani iko katika tetemeko la
kutisha nchini Tanzania.
NANI WA KULAUMIWA?
Hili ni tetemeko
ambalo liko katika ulimwengu wa roho. Tendo lolote la kulichukulia
tetemeko hili kimwilimwili, tendo hilo litakuwa ni tendo la kumwabudu
Yule mwovu aliye Baba wa Uovu (Kol.2:18). Na ni hatari kubwa.
Maelezo Na.3 ya Yn.8:12 ya Bibilia Takatifu toleo la Iringa hufafanua
usemi wa Kristo Neno la Mungu kwamba Yeye amekuja kuwa Nuru ya
Ulimwengu, na kwamba yeye amfuataye hatkwenda gizani kamwe, bali atakuwa
na Nuru ya Uzima.
Maelezo Na.3 yanasomeka kama ifuatavyo: “Nuru
na giza ni kielelezo cha falme mbili zinazohitilafiana na kupigana,
yaani Ufalme wa Mema utawaliwao na Kristo, na Ufalme wa uovu
unaomilikiwa na shetani. Kila ufalme unajaribu kuushinda mwingine.
Watu wanagawanyika baina ya wana wa Nuru na wana wa giza kadiri
waishivyo, kwa mvuto wa Nuru Kristo au kwa mvuto wa giza shetani. Wana
hao wote watambulikana katika vitendo vyao”.
Kuhusu hao wawili
wanaopambana, Biblia yenyewe hutuambia “Basi nasema, Nendeni kwa Roho,
wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani
ukishindana na Roho na Roho kushindana na mwili kwa maana hizi
zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka (Gal.5:16-17)”.
Gal.5:19-21 hutuorodheshea matendo ya mwili ambayo ni uasherati, uchafu,
ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, UADUI, UGOMVI, Wivu, hasira, fitina,
faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na kwamba wayatendao mambo ya
jinsi hii hawataurithi ufalme wa Mungu.
Kinyume chake,
Gal.5:22-23 hutuorodheshea tunda la Roho ambalo ni upendo, furaha,
amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole kiasi.
NAFASI YA MAOMBI NA MAOMBEZI
Wewe na mimi tunakabiliwa na hawa wawili wapiganao ambao
wanatugombania. Huyu hutaka tuwe maskani au Hekalu lake, na huyu hutaka
tuwe kiti chake: 1Yoh.3:8a hutuambia kwamba atendaye dhambi (atendaye
yale yaliyo orodheshwa katika Gal.15:19-21) ni wa Ibilisi.
Na
anayemilikiwa na Ibililisi hukaliwa na Ibilisi kuwa kiti chake. Katika
hali hiyo, mhanga hupofushwa; na moyo wake hufanywa kuwa mgumu kuiona na
kufahamu iliyo kweli asije akamwongokea Mungu Kweli akamponya Yn.12:40;
2Kor.4:3-4).
Ndiyo maana Yn.8:47 hutuambia kwamba asiye wa Mungu
Kweli hayasikii maneno ya Mangu kweli. Na kwa sababu ya kumilikiwa
huko na Yule mwovu, Mungu Kweli hamsikii mhanga au mmilikiwa wa Yule
mwovu (Yn.9:31). Kwa sababu hiyo, kulikurupukia swala la maombi na
maombezi, ni kupoteza wakati na nyenzo katika ujumla wake. Watu
wataomba na kuombea; lakini wataishia kuwa wambea.
MAPASWA YALIYOKO MBELE YETU
Kukubali kukusanywa kundi moja na Jemedari mmoja tu (Yn.10:16; 11:52).
Vinginevyo, tunaambiwa katika YBS.34:23-24. “Iwapo mtu mmoja anajenga,
mwenzake akabomoa, je! Faida yao ni nini ila kazi bure tu? Iwapo mtu
mmoja anaomba, na mwingine analaani; Je! Bwana ataisikia sauti ya
yupi?” Hivyo, katika vita hivi dhidi ya Ibilisi tunapaswa kuwa wamoja
sawasawa na Neno la Mungu Efe.4:3-6.
Ili kuufikia Umoja huo
tunapaswa kunyweshwa (1Kor.12:13) na kuvalishwa (Gal.3:27) utimilifu
wote wa Mungu katika Kristo Neno la Mungu Kol.2:10; Efe.3:19). Ili hili
lipate kutimilika, tunapaswa kulenenda kwa jinsi ya Kristo tukiwa
tumeachana kabisa na kila kilicho cha kibinadamu, wala mafundisho ya
awali ya ulimwengu (Kol.2:8-10). Kwenda kwa jinsi ya Kristo ndiko kule
kwenda kwa imani 100% (Gal.5:4-5). Kwenda kwa jinsi ya Kristo ndiko
kule kuenenda kwa Roho (Gal.5:16) sawasawa na mapenzi ya Mungu ambaye
hutafuta watu wamwabudu katika Roho na kweli (Yn.4:23-24;
1Yoh.5:14-15).
KWA ANGUKO LA ADAMU NA EVA, WATU WOTE NI WA IBILISI (1Yoh.3:8a)
Kutokana na ukweli wa mambo ulivyo, watu wote wamekuwa wa Ibilisi kwa
dhambi ya Adamu na Eva. Lakini kwa upande wa mpiganaji wa upande wa
pili ni kwamba kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao
wanaotakaswa (Ebr.10:14). Na utakaso umetimilika kwa kutolewa Mwili
(Nafsi) wa Kristo Neno la Mungu mara moja tu (Ebr.10:10); ambamo ndani
yake mna maji safi na hai yaliyomo katika Damu ya Yesu, Roho Mtakatifu
(Yn.7:37-39) aliyemo katika Neno la Mungu (Ebr.10:19-22; Yn.17:17, 19;
Efe.5:25-27).
Utakaso ni kule kuondolewa kwa ule mlima
farakanishi ambao Yule mwovu ameupandikiza ndani yetu kuharibu mahusiano
na mawasiliano na Mungu Kweli. Mlima huo unapoondolewa, ndipo Mungu
huwa ndani ya nafsi ya mtu na nafsi ya mtu ndani ya Umoja wa Nafsi Tatu
za Mungu Kweli. Hapo mtu huwa Umoja na Mungu. Mungu huwa ndiye
Mtendaji Mkuu ndani ya nafsi ya mtu. Hapo ndipo nafsi ya mtu katika
kuwa umoja na Nafsi Tatu za Mungu huwa mshindi na zaidi ya mshindi dhidi
ya Ibilisi (Rum.8:37).
SIRI YA UMOJA UNAOTAKIWA, IMO KATIKA KUPOKEA HIYO ZAWADI YA UTAKASO
ambao hufuatiwa na kukamilishwa katika Umungu. Isisahaulike wala
kupuuzwa kwamba pale Msalabani Kristo Neno la Mungu alionja mauti kwa
ajili ya kila mtu; bila kujali dini, jinsia, umri, cheo, wala chochote
kile kiwacho. Ni kwa ajili yako hapo kama ulivyo, na mimi hapa kama
nilivyo.
Tumeona hapo juu kwamba Kristo Neno la Mungu alionja
mauti kwa ajili ya kila mtu. Kristo Neno la Mungu alikufa kutuokoa
kutoka utumwa wa dhambi ili atuweke huru kweli kweli (Mt.1:21; Yn.8:36)
maana atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi (Yn.8:34).
Wasomi wa
Bibilia tunaona kwamba kila akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila
atendaye dhambi hakumwona wala hakumtambua (1Yoh.3:6). Na katika
Kol.2:23 tunaambiwa kwamba ibada mnazojitungia wenyewe ambazo hazifai
kitu kuzizuia tamaa za mwili zile zilizo- orodheshwa katika Gal.5:19-21.
Sasa sisi tunataka tuwe na ujasiri mmoja wa kumkaribia Mungu wetu
kuhusu hili janga analotuletea Ibilisi. Tusipoteze ukweli kwamba Kristo
Neno la Mungu Kaonja mauti kwa ajili ya kila mmoja wetu. Lengo la
kufanya hivyo ni kututoa kwenye utumwa wa dhambi tuweze kuhusiana na
kuwasiliana na Mungu katika Umoja wake wa Nafsi Tatu (Yn.17:21-23;
1Yoh.4:13).
Kwa kusimama katika aya hizi Kol.2:23 na Gal.5:19-21)
kiukweli, bila uongo wala unafiki wowote mbele za Mungu Roho (Yn.4:24)
katika Umoja wa Nafsi Tatu. “Kweli, na Neno, na Roho Mtakatifu, zipime
ibada zinazoendeshwa kwenye dini au dhehebu lako lolote lile, je zinafaa
chochote kuzizuia tamaa za mwili zilizoorodheshwa katika Gal.5:19-21?
Kama jibu la kweli ni ndiyo mbele za Mungu Kweli basi ni vema na vizuri
sana! Jibu likiwa hapana; basi ujue kwamba uko hatarini; kwani imekuwa
kwamba uko mbali na Mungu.
Lakini hiyo isikutishe. Iko faraja
kutoka kwa Mungu. Kwamba bado una uhai huu wa mwili wa nyama hata sasa
ni kwa sababu Mungu kweli hapendi wewe upotee, bali kwamba umwongokee
Yeye uwe mzima (2Pet.3:9). Na siku na wakati uliokubalika wewe kupata
msaada wa Roho Mtakatifu, ni sasa.
Hivyo, nakuomba wewe rafiki
yangu mpendwa wa Kristo Neno la Mungu, uliye mpenzi wa kujiunga katika
jeshi la Kristo Neno la Mungu kuuangamiza ufalme wa Ibilisi kwako, kwa
Tanzania na dunia katika ujumla wake, na kuomba kwanza ya yote kupokea
zawadi au neema ya ondoleo la dhambi au utakaso kwa njia ya imani ya
100% (Mk.11:23) kwamba umeoshwa kwa maji safi na hai yaliyomo katika
Damu ya Kristo Neno la Mungu, Roho Mtakatifu aliyemo katika Neno la
Mungu ambaye ndiye Mwombezi wetu mbele za MUngu kweli.
Jambo hilo
lifuatiwe na Ukweli kwamba Mungu kweli amesema, kwa Utakazo huo sasa
amekushirikisha utimilifu wote wa Umungu wake. Kama Yeye alivyo ndivyo
ulivyo na wewe duniani hapa (1Yoh.4:17); na kwamba dhambi zako na uasi
wako uliopita hataukumbuka tena hata milele (Rum.3:25; Ebr.10:17).
Katika hali hiyo ya amani na Mungu kweli, sasa kwa nafsi yako mshukuru
Mungu kwa ajili yako, kwa ajili ya Taifa letu Tanzania na kwa dunia
katika ujumla wake.
UBARIKIWE SANA!!!
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0787 765 759
0714 118 428
0753 298 707
Chamayombe37@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



2 comments:
Baba umebarikiwa sana, endelea kutupa NENO.
Ex wangu alinisababishia maumivu mengi na nimevunjika moyo na kuharibiwa tangu wakati huo. Nimewasiliana na wachawi wengi na wananinyang'anya pesa bila matokeo yoyote. Nilituma barua pepe nyingi sana nikitafuta uchawi wa kweli hadi nikaelekezwa na mwanamke wa miaka 45 ambaye Dk DAWN aliwahi kusaidia hapo awali, bila kujua niliwasiliana na Dk DAWN ingawa sikuamini, lakini baada ya kufanya kile alichoelezea, nilifuata maagizo yangu. ex alirudi kwangu akiniambia nimsamehe na nikamsamehe na leo nina furaha na ndoa yangu. Unaweza kuwasiliana na Dk DAWN kupitia barua pepe kwa ( dawnacuna314@gmail.com ) au kupitia WhatsApp kwa (+2349046229159) na jaribio litakushawishi.
Post a Comment