Subscribe:

Sample text

Sample Text

Friday, 21 June 2019

UBATILI WA KUTUKUZA JINA “YESU”





Katika
1Kor.8:5-6, Paulo Mtume anatueleza swala la kuwepo miungu mingi na mabwana
wengi, kinyume cha ukweli kwamba kwetu sisi yupo Mungu mmoja na Bwana mmoja.

Katika
2Kor.11:4 Mtume Paulo anawashangaa wao ambao wanawapokea wao ambao wanahubiri
mayesu wengine.

Biblia
inatueleza habari za Mungu wa dunia hii (2Kor.4:3-4). Biblia inatueleza pia
habari za yule mwasi ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama cha
kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu akijionesha nafsi
yake kana kwamba yeye ndiye Mungu (2Thes.2:4).

Kwamba
kuna akina Yesu wengine kunapelekea kuwapo akina Yesu wa aina mbili: kuna akina
Yesu ambao walilipata jina hilo kwa mujibu wa kawaida za kwanza za dunia
(Gal.4:3) ambazo huelezeka kwamba ni pepo watawala wa ulimwengu walioitumia
torati ya Musa kupanga na kuamuru kila jambo katika maisha ya kila siku(Gol.4:3).

Kwa
upande mwingine, kuna Kristo Neno la Mungu aliyelipewa Jina hilo Yesu la
kibinadamu kwa taratibu ambazo chanzo chake ni hao pepo watawala wa ulimwengu
ili kukomesha hizo taratibu au sheria hizo zilizoanzishwa na pepo watawala wa
ulimwengu (Gal.4:4; Gal.5:4-5; Ebr.10:9-18).

Sasa
Jina hilo ambalo chanzo chake ni pepo watawala wa ulimwengu kamwe haliwezi
kutamalaki milele. Jina hilo ambalo chanzo chake ni pepo watawala wa ulimwengu
haliwezi kulipindua Jina NENO LA MUNGU (Ufu.19:13), Jina ambalo ni la milele
yote (Yn.1:1-5; 1Yoh.1:1-3;) ambalo ni Neno aliyefanyika Mwili (Yn.1:14).
Mungu
Kweli aliyewatumia manabii kuonesha kughadhibishwa kwake na taratibu za kidini
(Zab.50; Isa.1;66;  Yer.7; 18:12-17;44;
Amo.5:21-27), Mungu aliyebatilisha sheria na taratibu za pepo tawala wa ulimwengu,
kisha yeye huyo huyo akubaliane milele hicho kilichotokana na taratibu au
sheria hizo batili. HAIWEZEKANI. Munguhajikani mwenyewe (2Tim.2:13).

Jina
“Yesu” limeisha pamoja na sheria zilizotumika kumpatia Jina hilo. Mkombozi na
mwokozi anaendelea kutukuzwa kwa Jina lake la milele “NENO LA MUNGU”.

Jina
“Yesu” limebatilishwa pamoja na sheria za mapepo. (Rum.10:4; Gal.5:4-5). Ndiyo
maana tunamsifu na kumtukuza “Kristo NENO LA MUNGU” sasa na milele bila aibu
yoyote, tukisema, “Atukuzwe Kristo Neno la Mungu” sasa hata milele. Amina

LUKA
ROKI CHAMAYOMBE
0714118428

KUKULIA UKWELI WA MUNGU: KUKULIA UKWELI WA MUNGU: NI LIPI KANISA LA KRISTO ...





JE,
MBINGUNI YA MUNGU PEKEE WA KWELI IKO WAPI?
Tumehakikishwa
kwamba Mungu pekee wa kweli ni Umoja wa Nafsi Tatu: (1) Kweli (Yn.3:33; 8:26;
1Yoh.1:1-3), (2) Neno (Yn.1:1-5; 1Yoh.1:1-3) na (3) uzima au Roho (Yn.6:63).

1Yoh.5:8
hututhibitishia kwamba Nafsi Tatu hawa hukaa mbinguni katika hali ya umoja
usiogawanyika.






Kwa
mantiki hii tuna kila haki ya kuamini kwamba (1) Nafsi Kweli hukaa katika Nafsi
Neno na Nafsi Uzima au Roho; (2) Nafsi Roho au Uzima hukaa katika Nafsi Kweli,
na Nafsi Neno; na (3) Nafsi Neno naye hukaa katika Nafsi Kweli na Nafsi Uzima
au Roho.


Kifupi
ni kwamba kila Nafsi miongoni mwao hukaa katika kila Nafsi miongoni mwao.


Hivyo,
wanaoshuhudia mbinguni iliyo maskani au kao la Nafsi hao watatu ni Umoja wa hao
Nafsi Tatu miongoni mwao. Umoja wa Nafsi Tatu ndio mbinguni halisi anakokaa
Mungu Umoja wa Nafsi Tatu: Kweli, Neno na Uzima (1Yoh.5:8).

Hivyo
Nyumba ya Mungu tunayoikuta Ebr.10:21, Efe.2:19, Hekalu na Maskani tunayokuta
katika Efe.2:21 na 22 na Patakatifu tupatapo katika Ebr.10:19 si chochote kile
bali Umoja wa Nafsi Tatu za Mungu pekee wa Kweli na ndiyo mbinguni wanakokaa
Nafsi Tatu za Mungu pekee wa kweli.


Tamani
kuingia mbinguni leo kwa njia ya Kristo Neno la Mungu aliye katika Utatu
Mtakatifu, na aliyetuombea kwamba pale alipo na sisi tuwepo (Yn.17:24). Yeye
ndiye aliye Njia, Kweli na Uzima (Yn.14:6) na ndiye Mwombezi wetu (Yn.17; Rum 8:34;
Ebr. 7:25; 1Yoh.2:1). Hakuna Mwombezi wa uhakika na aliyelipa fidia ya
kukubalika kwa Baba ila Yeye tu.

Hatuna
cha kufanya ila kumshukuru Mungu kwa wema, huruma, ukarimu, uwezo na upendo
wake bila mipaka yoyote katika yote. (Efe.3:20).
LUKA
ROKI CHAMAYOMBE
0714118428

KUKULIA UKWELI WA MUNGU: NI LIPI KANISA LA KRISTO NENO LA MUNGU

KUKULIA UKWELI WA MUNGU: NI LIPI KANISA LA KRISTO NENO LA MUNGU: Itakumbukwa kwamba ile mada yetu tuliyoipa jina "KANISA LA KRISTO NENO LA MUNGU" ilitufikisha tu kwenye sifa 4 za Kanisa; Kwamba K...