"UT UNUM SINT"
BARAGUMU LA KIKOROKORONI.
Kwa kadiri ya Eze.3:16--21 "UT UNUM SINT" Ile barua ya kichungaji iliyoandikwa na papa Yohana paulo 11 mwaka 1995.ni baragumu la kikoro koroni au kiulinzi.kuitangazia dunia kwamba iko kwenye njia potevu.
Katika kifungu cha kwanza (1) Barua hiyo tunakuta habari za Mpinga kristo asemaye ."Mtu si chochote .bali ni kitu cha kiudongo tu ambaye anapaswa aishi kana kwamba hakuna Baba wa wote aliye juu ya yote.atendaye kazi katika yote na ndani ya yote.(Efe.4:6)
Dhidi ya mtazamo huo wa kimpinga kristo uliopelekesha dunia upotevuni.kifungu cha 15 huwataka waamini kuwa waaminifu kwa Injili.kuwa na fikra mpya na mtazamo mpya wa mambo.kinyume kabisa na fikra na mtazamo wa mambo ambao umeipeleka dunia upotevuni.
Kifungu cha 18 chaeleza ubatili wa umoja wowote ule au makubaliano yoyote yale yaliyofikiwa kwa gharama ya ukweli.Hii ni sababu makubaliano kama hayo hupingana na Baba wa wote aliye "Kweli"(Yn8:26 . 3:33) asiye na uongo wowote ule ndani yake(1Yoh.2:21.
Katika ujumla wake.kifungu cha 18 ni rejea mada DIGNITATIS HUMANAE ya VATIKANI 11 ya 1965.mada ambayo ilisisitiza kwamba hadhi au uthamani wa Utu .Uko katika kutafuta"Kweli" na kuambatana nayo.
Kifungu cha 32 chaelekeza kwamba katika safari ya kutafuta kweli .wadau husika wawe wanashirikishana "Kweli" wanayoifikia .kwa njia ya mafundisho.mawasiliano au kwa njia ya mazungumzo.
Katika jambo hili.Baba na Mwokozi wetu ashukuriwe na kutukuzwa sana kwa kuwezesha njia za mitandao .kama vile Whatsapp ,Facebook,Instagram n.k. yeye aliye Baba wa wote.aliye juu ya yote .atendaye kazi katika yote na ndani ya yote .awahifadhi na kuwabariki kwa Baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa Roho ndani yake kristo Neno la Kweli wahudumu wa vyombo hivyo (efe1:3)
Kifungu cha 36 chasema kwamba wadau husika wanapaswa kuing'ang'ania Imani walio fikishiwa na roho wa kweli ,bala mapunguzo yoyote .wala makubaliano ya kiwepesiwepesi .Vifungu 77--78 Vinagisia tamanio la kufikia kanisa lililo moja .takatifu .katoliki na la Kimitume.
Kifungu cha 80 chagusia swala la Upakwa mafuta uliyo kwa wote bila ubaguzi wa aina yoyote ile.
Korokoroni au Mlinzi amekwisha kutimiza jukumu lake mbele za Bosi wake aliyemtuma .hadaiwi chochote .
Je? Wewe na mimi tunalichukuliaje jambo hili la kuwa waaminifu kwa Injili ,kuwa na fikra mpya , kuwa na mtazamo mpya,kuitafuta kweli na kuing'ang'ania kwa sifa na utukufu wa Baba yetu atupendaye upeo kwa upendo wa milele ? Tunamrudishia nini ?
Je ? Ni busara kuendelea kumng'ang'ania aliyetupeleka upotevuni kwa hasara yetu ya milele ?
Mimi mwenzio nimemkataa sasa na hata milele .Hata maiti yangu nimekwisha kutangaza Jumuiani mbele ya Paroko ."SITAKI IFANYIKE IBADA YA KIDINI YOYOTE ILE"
LUKA ROKI CHAMAYOMBE
0714118428
Www.chamayombe.blogspot.com



0 comments:
Post a Comment