Subscribe:

Sample text

Sample Text

Monday, 27 January 2020

KWA KUWA MBINGUNI MUNGU HAYUPO YUKO WAPI. SASA?

Hili ni swali nyeti linalotukabili kwa haki kabisa :kwamba baada ya Watatu  kushuhudia na kuthibitisha kwamba mbingu inakaliwa na Roho(Yn.4:24)Aliye Umoja wa Nafsi  Tatu : Kweli ,Neno la Kweli  na Uzima wa milele .Kwamba Neno "Mungu " halipo kabisa mbinguni.
Harakati tulizozichukua kumtafuta aitwae "Mungu"Zikatufikisha  kwa Mungu wa dunia hii aliye NDANI YA WASIOAMINI  isiwazukie Nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu(2kor,4:3--4)
Tukamkuta Tena "Mungu " katika 2Thes,2:3--4iliyotueleza habari za yule Mtu wa kuasi ,Mwana wa uharibifu .Yule mpingamizi ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa ,Hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu akijionesha  nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
1kor,8:5 Hutueleza kwamba wako wengi hawa .Na torati  ya Musa Vitabu 5 vya Kwanza vya Biblia hutueleza habari ya kuniinua kwake kwamba yeye ndiye Mungu na kudai watu washikamane naye((kumb,30:20)Haya yote yametufikisha kwenye ukweli wa Yn,8:44
Ambapo Kristo aliwaambia waisrael"Ninyi ni wa baba yenu Ibilisi Na tamaa za baba yenu -------nk
Kumbe ndiyo maana Mungu hayumo  kati ya walio shuhudiwa mbinguni (1Yoh,5:8)Takasika na barikiwa  sana kwa Kristo Neno la Kweli(Yn.17:17, 19.  Efe,5:26--27). 
Luka Chamayombe Mzumbe Morogoro

Thursday, 23 January 2020

MBWA JASIRI KUJIKOMBAKOMBA KWA CHATU.

Hali ya kibinadamu inayoendelea kimaisha inanikumbusha tukio lililompata aliyekuwa mbwa wangu ambaye  alikuwa  mkali hata aliwahi kumwua  nyani yeye peke yake.
Lakini siku moja nilishuhudia akimwendea chatu kwa kujikombakomba huku akiwa amefyata mkia kwa unyenyekevu,na kuishia kukamatwa na yule chatu.
Kristo Bwana wetu akatupatia sharti la kuwa wanafunzi wake ili kuijua ile Kweli ya kutuweka huru ,Nalo sharti Hilo ni kukaa katika Neno lake (Yn8:31--32)
Kwa harufu yake ya kiuchawi Mungu was dunia hii ,yule chatu wa kiroho ,amewaroga binadamu wasikubali kuipenda Kweli ili waokolewe (2Thes. 2:9--10 na 2Tim 4:3--4)Badala ya kutafuta Kweli katika Neno la Kweli kama Kristo Neno la Kweli alivyotueleza ,Ibilisi ,Yule Mungu wa dunia hii ,amewakamata watu kwamba yeye awe anawajulisha Mambo kwa njia ya maono(kol 2:18)
Ndivyo Mungu wa dunia hii ,katika uwingi wake uliosemekana katika 1Kol,8:5 na ambao Hutambiwa na wenye maono "wakisema  Mungu wangu ni mkubwa  (2Thes 2:3--4) Kwamba Kila mmoja ana Mungu (mzimu )wake. Kati ya wale miungu mingi na mabwana wengi kumpa maono.
Binadamu kama binadamu hawezi kuondokana na janga la pepo wanaotuzunguka ,lakini kwa yeye aliye Umoja wa nafsi Tatu ;Kweli,Neno la Kweli na Uzima wa milele,Yote yanawezekana ,tayari (Mk,10:27. Kol.2:2--3,.  8--10)
Kwa Kristo Neno la Kweli ,nashika bega la nafsi yako ,na kukutikisa na kukuamuru "Zinduka kutoka kwenye usingizi huo mzito wa hao Miungu ,Na Kristo Neno la Kweli aliyeutimilifu wote wa Kweli atakuangaza (Efe,5:14) kwa sifa na utukufu wa Muumba na Mkombozi aliye Umoja wa nafsi Tatu Kweli ,Neno la Kweli na Uzima wa milele,Sasa na milele,

Sunday, 12 January 2020

BIBLIA SI YA HISTORIA

Blblia husimulia Vita vilivyopo kati ya Muumba  na Mwizi wake .Hivyo ni kosa kubwa kuitazama na kuifikiria Biblia kihistoria  ya kibinadamu.
Biblia inatueleza kwamba Muumba wa vyote amejishuhudia mbinguni kwamba ,Yeye ni "Umoja was nafsi Tatu"Baba ,Neno na Roho Mtakatifu".
Kwa kuwa tunatakiwa tupate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika ,tupate kujua kabisa Siri ya Kristo Neno la Kweli ambaye Ndani yake yeye hazina  zote za hekima na maarifa zimesitirika (kol. 2:2__3. 
Efe. 4:13__15)tunapaswa kuwafahamu hawa watatu.
Baba si jina,balini sifa TU kwamba kazaa.Mwana kamfunua baba yake kwamba yeye aliyenipeleka ni Kweli
Shart Biblia itufafanulie. Zaidi habari ya "NeNO.    Ufu,19:12__13,yatuambia kwamba ,,kabla ya kumjua.  Baba ,jina  lake ni "Neno la Mungu" Hivyo baada ya Mwana kamfunua Baba yake kuwa "Kweli". Jina lake Sasa ni NENO la KWELI"
Kuhusu Roho Mtakatifu,hata ile Roho ya upotevu naye anaweza kuniita "MTAKATIFU"kuondokana na utata huu Roho wa NENO l a Kweli Jina lake tunalipata Yn,6:63.  Kwamba ni uzima wa milele"
Katika ukweli huu ,majina "Mungu "na Yesu " Hayapo mbinguni.kuhusu Jina "Mungu"katika 2kor.4:3__4 .tunaelezwa habari za "Mungu wa dunia hii"ambaye hupofusha fikra za watu isiwazukie Nuru ya Injili ya Kristo.
Katika 2Thes.2:3---4,Biblia inatueleza habari ya yule Mtu wa kuasi.Mwana wa uharibifu yule mpingamizi ajiinuaye nafsi yake juu ya Kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa.Yule mpingamizi kwa jinsi anavyopofusha fikra za watu wasizukiwe na utukufu wa Injili ya Kristo .Mungu huyu ni mpinga Kristo ,anayetaka watu waishi kana kwamba hakuna Mungu duniani na 1Kor,8:5. Hutuhakikishia kwamba wako miungu wengi .
Hawa ni pepo watawala wanaotawala dunia kwa njia ya Torati ya Musa ambayo imefutwa.
Kwa habari ya Yesu ,Rum.10:4  Hutuambia kwamba Kristo ni mwisho wa sheria.Ndiyo Maana Biblia 2kor.11:4.  Inawashangaa watu wanao wavumilia watu wanaohubiri Yesu mwingine na Maroho mengine  nje ya yule aliye uzima wa milele .Yesu wa torati ameishia Torati.Ndiyo Maana tunaelezwa swala la kutengwa na Kristo Neno la Kweli wale watakao kuhesabiwa haki kwa ile sheria ya Musa(Gal.5:4)
Kwa kadiri ya Gal. 5:16---24,Muumba wetu aliye Roho huenenda kwa Roho ,na Mungu wa dunia huenenda kwa mwili.Vita vimeshamiri kati ya Mungu wa dunia    DHIDI ya Kweli.

ATUKUZWE MUUMBA NA MKOMBOZI  WETU ,ALIYE UMOJA WA NAFSI TATU ,KWELI,NENO LA KWELI,NA UZIMA WA MILELE

Wednesday, 1 January 2020

KATIKA KRISTO NENO LA KWELI,AMBAYE AMEKUJA KATIKA MAJI NA KATIKA. DAMU,

NAKUTAKIA WEWE ,FAMILIA,NA JAMII YAKO YOTE"HERI" BARAKA NA USHINDI WA KISHINDO  DHIDI YA IBILISI ,KWA ILE ZAWADI YA KUTAKASWA,KUKAMILISHWA KATIKA UTIMILIFU WAKE WOTE KRISTO NENO LA KWELI;ZAWADI AMBAYO YEYE MWENYEWE AMETUPATIA KWA WEMA NA UPENDO,.  TANGU 2020 NA MILELE
Endeleza ujumbe huu kwa wore kadiri iwezekanavyo