Hali ya kibinadamu inayoendelea kimaisha inanikumbusha tukio lililompata aliyekuwa mbwa wangu ambaye alikuwa mkali hata aliwahi kumwua nyani yeye peke yake.
Lakini siku moja nilishuhudia akimwendea chatu kwa kujikombakomba huku akiwa amefyata mkia kwa unyenyekevu,na kuishia kukamatwa na yule chatu.
Kristo Bwana wetu akatupatia sharti la kuwa wanafunzi wake ili kuijua ile Kweli ya kutuweka huru ,Nalo sharti Hilo ni kukaa katika Neno lake (Yn8:31--32)
Kwa harufu yake ya kiuchawi Mungu was dunia hii ,yule chatu wa kiroho ,amewaroga binadamu wasikubali kuipenda Kweli ili waokolewe (2Thes. 2:9--10 na 2Tim 4:3--4)Badala ya kutafuta Kweli katika Neno la Kweli kama Kristo Neno la Kweli alivyotueleza ,Ibilisi ,Yule Mungu wa dunia hii ,amewakamata watu kwamba yeye awe anawajulisha Mambo kwa njia ya maono(kol 2:18)
Ndivyo Mungu wa dunia hii ,katika uwingi wake uliosemekana katika 1Kol,8:5 na ambao Hutambiwa na wenye maono "wakisema Mungu wangu ni mkubwa (2Thes 2:3--4) Kwamba Kila mmoja ana Mungu (mzimu )wake. Kati ya wale miungu mingi na mabwana wengi kumpa maono.
Binadamu kama binadamu hawezi kuondokana na janga la pepo wanaotuzunguka ,lakini kwa yeye aliye Umoja wa nafsi Tatu ;Kweli,Neno la Kweli na Uzima wa milele,Yote yanawezekana ,tayari (Mk,10:27. Kol.2:2--3,. 8--10)
Kwa Kristo Neno la Kweli ,nashika bega la nafsi yako ,na kukutikisa na kukuamuru "Zinduka kutoka kwenye usingizi huo mzito wa hao Miungu ,Na Kristo Neno la Kweli aliyeutimilifu wote wa Kweli atakuangaza (Efe,5:14) kwa sifa na utukufu wa Muumba na Mkombozi aliye Umoja wa nafsi Tatu Kweli ,Neno la Kweli na Uzima wa milele,Sasa na milele,
Thursday, 23 January 2020
MBWA JASIRI KUJIKOMBAKOMBA KWA CHATU.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



0 comments:
Post a Comment