Blblia husimulia Vita vilivyopo kati ya Muumba na Mwizi wake .Hivyo ni kosa kubwa kuitazama na kuifikiria Biblia kihistoria ya kibinadamu.
Biblia inatueleza kwamba Muumba wa vyote amejishuhudia mbinguni kwamba ,Yeye ni "Umoja was nafsi Tatu"Baba ,Neno na Roho Mtakatifu".
Kwa kuwa tunatakiwa tupate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika ,tupate kujua kabisa Siri ya Kristo Neno la Kweli ambaye Ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika (kol. 2:2__3.
Efe. 4:13__15)tunapaswa kuwafahamu hawa watatu.
Baba si jina,balini sifa TU kwamba kazaa.Mwana kamfunua baba yake kwamba yeye aliyenipeleka ni Kweli
Shart Biblia itufafanulie. Zaidi habari ya "NeNO. Ufu,19:12__13,yatuambia kwamba ,,kabla ya kumjua. Baba ,jina lake ni "Neno la Mungu" Hivyo baada ya Mwana kamfunua Baba yake kuwa "Kweli". Jina lake Sasa ni NENO la KWELI"
Kuhusu Roho Mtakatifu,hata ile Roho ya upotevu naye anaweza kuniita "MTAKATIFU"kuondokana na utata huu Roho wa NENO l a Kweli Jina lake tunalipata Yn,6:63. Kwamba ni uzima wa milele"
Katika ukweli huu ,majina "Mungu "na Yesu " Hayapo mbinguni.kuhusu Jina "Mungu"katika 2kor.4:3__4 .tunaelezwa habari za "Mungu wa dunia hii"ambaye hupofusha fikra za watu isiwazukie Nuru ya Injili ya Kristo.
Katika 2Thes.2:3---4,Biblia inatueleza habari ya yule Mtu wa kuasi.Mwana wa uharibifu yule mpingamizi ajiinuaye nafsi yake juu ya Kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa.Yule mpingamizi kwa jinsi anavyopofusha fikra za watu wasizukiwe na utukufu wa Injili ya Kristo .Mungu huyu ni mpinga Kristo ,anayetaka watu waishi kana kwamba hakuna Mungu duniani na 1Kor,8:5. Hutuhakikishia kwamba wako miungu wengi .
Hawa ni pepo watawala wanaotawala dunia kwa njia ya Torati ya Musa ambayo imefutwa.
Kwa habari ya Yesu ,Rum.10:4 Hutuambia kwamba Kristo ni mwisho wa sheria.Ndiyo Maana Biblia 2kor.11:4. Inawashangaa watu wanao wavumilia watu wanaohubiri Yesu mwingine na Maroho mengine nje ya yule aliye uzima wa milele .Yesu wa torati ameishia Torati.Ndiyo Maana tunaelezwa swala la kutengwa na Kristo Neno la Kweli wale watakao kuhesabiwa haki kwa ile sheria ya Musa(Gal.5:4)
Kwa kadiri ya Gal. 5:16---24,Muumba wetu aliye Roho huenenda kwa Roho ,na Mungu wa dunia huenenda kwa mwili.Vita vimeshamiri kati ya Mungu wa dunia DHIDI ya Kweli.
ATUKUZWE MUUMBA NA MKOMBOZI WETU ,ALIYE UMOJA WA NAFSI TATU ,KWELI,NENO LA KWELI,NA UZIMA WA MILELE



1 comments:
Amen hakika ni kweli usemayo asante Kwa ujumbe mzuri
Post a Comment