Kati ya vipengere hivi viwili, “Karismatiki”na “Katoliki”, kipengere
“Katoliki” kimekwisha kushughulikiwa katika mada iliyoitwa “KANISA LA
KRISTO NENO LA MUNGU”. Hivyo, hapa tutajikita katika kujifunza
kipengere “KARISMATIKI”.
Katika mada iliyohusu IMANI tumepitia
fundisho la Mitume wa Kristo Neno la Mungu kuhusu ukombozi, upatanisho,
ondoleo la dhambi au utakaso kwa njia ya IMANI katika Damu ya Kristo
Yesu.
Lakini utakaso si jambo linaloishia hewani. Utakaso ni
kuondoa kizingiti au kifarakanishi. Kifarakanishi kinaondolewa ili
iweje?
Ebr.10:14 hutuambia, “Lakini kwa toleo moja amewakamilisha
hata milele hao wanaotakaswa, Kumbe matokeo ya kutakaswa ni
kukamilishwa. Na aliye kamili ni Mungu. Hivyo , kukamilishwa
kunahusika na mtu kushirikishwa Umungu wa pekee wa kweli.
Kunafanyikaje? 1Kor.12:13 hutuambia, “Kwa maana katika Roho mmoja sisi
sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu wayahudi au kwamba tu
Wagiriki; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru, nasi sote tulinyweshwa
Roho mmoja”. Kumbe kubatizwa kwa roho ni kunyweshwa roho mtakatifu.
Nikushirikishwa Mungu wa pekee wa kweli.
Na kwa Ubatizo huo wa
kunyweshwa Roho Mtakatifu, wote watakuwa wamemvaa Kristo Yesu kuwa
watoto wa Mungu wa pekee wa kweli (Gal.3:27, 26). Kwa ubatizo huo wa
kunyweshwa Roho Mtakatifu, wahusika huwa ndani ya Mungu, na Mungu ndani
ya nafsi husika. Nafsi husika huwa warithi wa Mungu warithio pamoja na
Kristo Neno la Mungu (Rum.8:17). Watu au nafsi husika zitakuwa
zimetimilika katika utimilifu wote wa Mungu (Efe.3:19; Kol.2:9-10).
Kama vile mtoto wa simba alivyo simba, vivyo hivyo, mtoto wa Mungu ni
Mungu (1Yoh.4:17).
KUTIMILIKA KWA SHARTI LA KUUONA NA KUUINGIA UFALME WA MUNGU
Kwa ubatizo huo wa kunyweshwa na kuvalishwa Umungu alilolitoa Bwana
wetu Kristo Neno la Mungu kwamba mtu asipozaliwa mara ya pili hatauona
Ufalme wa Mungu, litakuwa limetimilika (Yn.3:3; 1Pet. 1:23).
MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO (Yn.3:5)
Mtu asipozaliwa kwa maji yapi? Katika mazungumzo kati ya Kristo Yesu
na Yule mwanamke Msamaria pale kisimani, Kristo Neno la Mungu alimwambia
Yule mwanamke, “Kama ungalijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye
nipe maji ninywe, wewe ungalimwomba Yeye Naye angalikupa maji yaliyo
hai. Yeye anywae maji haya ataona kiu tena. Bali yeye anywaye maji
nitakayompa mimi ataona kiu hata milele. Bali maji hayo yatakuwa ndani
yake chemchemi ya maji yakimbubujikia uzima wa milele” (Yn.4:10, 14).
Na katika Yn.7:37-39 Bwana Yesu Neno la Mungu anatualika, “Mtu akiona
kiu na aje kwangu anywe. Aniaminiye Mimi kama vile Maandiko
yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na Neno hilo
alilisema kuhusu Roho ambaye wale waaminio watampokea baadaye; kwa maana
Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa”.
Hivyo
maji yanayohusika na ubatizo aliouleta Kristo Neno la Mungu si maji ya
kumwagiwa wala kuzamishwa; bali ni maji ya kunyweshwa yakae ndani ya mtu
kumbubujikia uzima wa milele, uzima ule ule wa Mungu wa pekee wa kweli.
La kukazia hapa ni kwamba Mkarismatiki kweli kweli ni Yule
aliyenyweshwa Roho Mtakatifu. Na kwa tendo hilo mtu huyo yuko ndani ya
Kristo Neno la Mungu na Kristo Neno la Mungu yumo ndani ya mtu
ahusikaye. Hivyo mtu huwa Roho moja na Kristo Neno la Mungu. Na kwa
jinsi hiyo mtu huwa mshiriki wa utimilifu wote wa Mungu. Na hapo aweza
kufanya yote aliyofanya Kristo Neno la Mungu; (Yn.14:12) maana Mtendaji
ni Roho Yule Yule atendaye ndani ya Kristo aliye ndani ya huyo mtu
ahusikaye. Maana atendaye si huyo mtu ahusikaye, bali ni Roho Mtakatifu
ambaye yuko ndani ya Kristo aliye ndani ya mtu husika. Na hivyo,
kumsifu huyo mtu ni dhambi ya kumwibia Mungu Utukufu wake.
Kamusi
ya Kiingereza inatuelezea msukumo wa Kikarismatiki (Charismatic
Movement) kwamba ni msukumo wa kimsingi katika Makanisa ya Kikristo
ambao hukazia karama au vipawa ambavyo husadikiwa kwamba vinatolewa na
Roho Mtakatifu.
Mtazamo huu wa kukazia karama au vipawa
hauzingatii ukweli kwamba Yule asi huwa anajiinua juu ya kila kiitwacho
Mungu au cha kuabudiwa; huyu ambaye haachi kuingia katika hekalu la
Mungu akijionesha nafsi yake kama kwamba yeye ndiye Mungu
(2Thes.2:3-4).
Kuhusu ukweli huu, Bwana aliye Kristo Neno la Mungu
anatuonya, “Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au
yuko kule msisadiki; kwa maana watajitokeza makristo wa uongo, na
manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu wapate kuwadanganya,
ikiwezekana, hata hao wateule. Bali ninyi jihadharini; nimekwisha
kuwaonya yote mbele” (Mk.13:21-23).
Katika hili mafundisho ya Mitume yanazidi kuweka wazi; hao waliambiwa Roho Mtakatifu atawaongoza awatie katika kweli yote:
1. “Kuja kwa Yule mwasi ni kazi ya shetani, atumiaye uwezo wote, ishara
na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao
wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli wapate kuokolewa
(2Thes.2:9-10).
2. Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto
kushuka kutoka mbinguni juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha
wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya
huyo mnyama (Ufu.13:13-14).
3. “Hizo ndizo roho za mashetani zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote (Ufu.16:14).
Kuhusu swala hili la ishara na ajabu, Kristo, Neno la Mungu alituonya
mbele (Mk.13:23). Je, wakarismatiki tunaonyeka kiasi gani katika hili.
Ikiwa watu, baada ya kupokea utakaso kwa njia ya imani katika Damu ya
Yesu, hunyweshwa Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu huwa mkazi ndani ya watu
kuwabubujikia uzima, (Yn.4:14). Huyo roho ambaye huwa anaitwa “Shuka
roho, shuka na moto wako!! N.k. ni roho gani huyo kama siyo Yule
aliyeshangawa na Paulo Mtume katika 2Kor.11:4? Je, huko si kumtumikia
shetani badala ya Kristo Neno la Mungu?
Tukubali, tusikubali,
ukweli unabaki kwamba Karismatiki Katoliki ni tunda la Vatikani II; na
Mababa waliofuata waliipokea Karismatiki Katoliki kuwa ni Baraka kwa
Kanisa.
Kutokana na ukweli huu, Karismatiki Katoliki inapaswa
kuwa ni chombo cha utekelezaji wa fundisho la Vatikani II kama
tunavyofikishiwa na Mababa Mtakatifu.
Mababa wanatutaka tuwe
waaminifu kwa Injili; tuiongokee Injili kwa kina, kuwa na fikira mpya,
kuwa na mtazamo mpya wa mambo, kuiheshimu kweli kuliko chochote kila;
na, katika mchakato wa kutafuta kweli, namna zetu za kuelezea imani zetu
kamwe zisiwe kizingiti.
Ili kuwa waaminifu kwa Injili au
kuongokea Injili kwa kina kunadai utekelezaji wa sharti la kuwa
mwanafunzi wa Yesu kweli kweli, nalo ni kukaa katika Neno lake
(Yn.8:31-32).
Kujikita katika Uinjilishaji badala ya kujikita
katika kujua kweli huishia kujawa na wafanya mazingaumbwe (Conjurers)
badala ya wainjilishaji katika Karismatiki Katoliki ambao bila aibu
wanajiita, “Wakarismatiki kweli kweli na wakatoliki kweli kweli. Na kwa
sababu hiyo, hawatakuwa nje ya wale walioambiwa “Ninyi ni wa baba yenu
ibilisi; na tamaa za baba yenu ndizo mpe ndazo kuzitenda; maana yeye
alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli. Asemapo
uongo asema yaliyo yake mwenyewe; maana yeye ni mwongo na baba wa huo”
(Yn.8:44).
NENO LA MUNGU NI UZIMA
1. Kumeshuhudiwa watu
watatu kuondokewa na kansa ya ziwa walipojua na kuamini ukweli wa Neno
la Mungu kwamba mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu na kuyachukua magonjwa
yetu (Mt.8:17). Tangu tarehe 24/12/2005, mhusika mmoja wapo ni hai hadi
sasa. Hata wawili waliofuata miaka ya badaye, nao ni hai.
2.
Wawili kuondokewa na ukimwi wa shetani kwa kujua na kuamini
kushirikishwa kwao utimilifu wote wa Mungu (1Yn.4:13; Efe.3:19;
Kol.2:9-11). Badala ya ukimwi wa ibilisi wakapokea Ukimwi wa Yesu,
ukamilifu au utimilifu wa kinga mwilini. Wanadunda katika uzima wa
Yesu, Neno la Mungu hata sasa.
3. Kuna Mama aliyepokea
kutodhurika kwa mwanawe aliyekunywa sumu ya kutibia minyanya kwa hoja
kwamba Yesu Neno la Mungu amesema, “Hata mkinywa cha kufisha
hakitawadhuru” (Mk.16:17-18).
Yote kwa yote, kweli, ni dawa; tena
ni dawa ya uhakika; kwani kweli ni Mungu mwenyewe mwenye kuponya yote
(Hek.16:12). Tena Kristo Neno la Mungu, kasha tuombea kwa Baba,
“Uwatakase kwa ile Kweli; Neno lako ndiyo kweli. Nami najiweka wakfu
mwenyewe ili na hao watakaswe katika Kweli” (Yn.17:17, 19). Je,
inawezekana Baba kumkatalia Mwana ombi hili? Mungu hudumu wa kuaminiwa;
maana hawezi kujikana mwenyewe (2Tim.2:13). Ukiwa na moyo mgumu
kuupokea na kuuamini Ukweli huu ni kwa hasara yako.
Badala ya
kujikita kwenye makongamano yanayogharimu muda na mali nyingi; hebu sasa
Karismatiki iwe Chuo Kikuu cha Elimu ya mbinguni kwa kujikita katika
Neno la Mungu (Yn.8:31-32) ili kukidhi mapenzi ya Mungu anayetaka watu
wote waokolewe na kujua ile kweli (1Tim.2:4). Watu wa Mungu wanaangamia
kwa kukosa maarifa (Hos.4:6). Tena watu wa Mungu wanapotea kwa kutojua
Maandiko wala uwezo wa Mungu, (Mt.22:29). Karismatiki iwe chombo cha
kudhihirishia njia ya wokovu.
Mungu akubariki kwa Roho wake wa
Kweli wa kukuongoza akutie kwenye kweli yote (Yn.16:13) na kukuwezesha
kuukulia Umungu wa pekee wa Kweli hata kumfikia Yeye katika yote
(Efe.4.13-15). Yote yakiwa kwa sifa na utukufu wa Mungu wa pekee wa
Kweli, kwa usalama wako na wa dunia yote Mungu aliyoiumba kwa ajili
yake.
Kujigamba kwamba Umkarismatiki kweli kweli na Mkatoliki
kweli bila kunyweshwa na kuvalishwa utimilifu wote wa Mungu ni kuwa
mwongo na mtumishi wa Ibilisi; ni KUJILAANI.
Amini kwamba Mungu
wa pekee wa kweli, Baba wa Bwana wetu Kristo Neno la Mungu, na Baba
yetu, amekubariki kwa sababu ya kuikubali na kuipenda ile Kweli kwani
Kweli ni Yeye mwenyewe. Kuikubali na kuipenda Kweli ndipokumkubali na
kumpenda Mungu wa pekee, wa Kweli. Achana kabisa na uongo.
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0787 765 759
0714 118 428
0753 298 707
Chamayombe37@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



0 comments:
Post a Comment