Subscribe:

Sample text

Sample Text

Tuesday, 24 December 2019

AONDOA LA KWANZA ,ILI KUSUDI ALISIMISHE LA PILI(EBR.10;9

Kristo Neno la Kweli amekuja kuliondoa agano la Kwanza ambalo kwalo pepo watawala (2Thes 2;3-4) waliwatumikisha watu (Gal.4:3) kwa njia ile iliyosemekana katika (2Thes2:9--10) ili watu waukatae ukweli wasije wakaokoka (Yn.12:40) Ndiyo Maana tunaambiwa katika Kol. 2:18   "Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu ya wokovu mkaendelea kung'ang'ania na pepo watawala " legion " au Mungu .kamwe tusipotewe na ule ukweli kwamba kwa njia ile iliyosemekana katika 2Thes.2:3--4 Pepo watawala waliwatumikisha watu kwa njia ya torati au sheria ya Musa kujitengenezea kuwa miungu ya kuabudiwa kupingana na makusudi na taratibu za yeye aliye baba wa wote .
Kristo Neno la Kweli akaliteka jina Yoshua (Yesu).ambalo liliendeleza utawala wa torati ya Musa kuukomesha utawala wa torati ya Musa Rum.10:4.

Hii ni hekima ya Muumba ambayo wenye kuitawala dunia hii (hao pepo )hawaijui hata moja .Maana kama wangaliijua ,wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu (1Kor.2:8).kwa sababu ya kutojua Siri hii ,Jina Yesu (Yoshua )likawa mwisho wa Jina Yesu (Yoshua )pale msalabani kwa utukufu wa Kristo Neno la Kweli(Kol.2:13--15)Na torati ikafikia mwisho wake.
Kwa tendo hilo, Kristo Neno la Kweli ,akawa amehitimisha Imani mpya (Ebr,12:2)Na kwamba Mtu akiwa katika huyu Kristo amekuwa kiumbe kipya : Ya kale yamepita tazama ! Yamekuwa mapya (2kor.5:17).
Tunapohimizwa kwenda kwa Roho katika Gal.5:16, ni pamoja na kutomwangalia Yesu wa kimwili (2kor.4:18).Yesu wa kimwili ,Yesu wa Torati.ni kivuli tu Cha Kristo Neno la Kweli adumuye milele .Kazi y kivuli au nakala iliishia pale msalabani ambapo torati imefutwa na kuondolewa Isiwepo tena (Kol 2:13--15)
Ndiyo maana tunaambiwa ule ukweli wa Gal.5:4,. "Mmetengwa na Kristo ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria ambayo ni torati ya Musa.
Mbarikiwe san

0 comments:

Post a Comment