MWIVI HAJI ILA AIBE ,. ACHINJE NA. KUHARIBU(YN.10:10a)
Katika 2Thes.2:3--4. Paulo Mtume hutueleza habari za yule Mtu was kuasi.Mwana wa uharibifu ;. Yule mpingamizi.ajiinuaye nafsi yake juu ya Kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa : hata yeye mwenyewe kuketi hekalu la Mungu :akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
Hivyo ndivyo pepo watawala walivyowatumikisha watu kwa njia ya torati ya Musawajitengeneze kuwa miungu ya dunia kuabudiwa na watu badala na kinyume Cha Mwumba mwenyewe.kwa sababu wamejitengeneza hivyo .hawa miungu ni sanamu za kiroho .Na ndivyo hawa tuliotakiwa katika 1Yoh.5;21 kwamba tujilinde nafsi zetu na hao sanamu.Na ndiyo kahaba na wazinzi waliosemekana katika 1Kor.6;15---20. Ufu.14;4,. 8. Na Ufu.18;3.
KRISTO NENO LA KWELI AMEKUJA ILI TUWE. NA UZIMA ,KISHA TUWE NAO TELE(YN 10;10b)
1Yon.5;6. Hutuambia kwamba KRISTO NENO la. Kweli amekuja katika Maji na katika Damu.Amekuja katika Maji ili kututakasa na kutusafisha ili atunyweshe Tena maji yake ya kutububujikia uzima wa milele.(Yn4;10. 14;7;37--39 Maana Ndani yake Kristo. Ndimo ulimo uzima (Yn 1;4;. 6;63). Amekuja katika damu ili kuwa dhabihu ya Ukombozi .kutupatanisha na Baba. (Mt.26;28. Ebr .2;17; Kol. 1;14; 1Yoh 2;1--2)
Kristo. amekuja kututoa katika hali ya kuwa wana. Wa giza la Mungu wa Dunia .na kutuingiza Tena katika hali ya kuwa wana wa Nuru(Yn.8;12;. 12;36. 46) yake yeye mwenyewe.
UTAKATIFU UKO KATIKA KRISTO NENO LA KWELI TU.
Mambo ya Kristo neno la Kweli hakuna ayafahamuye ila Roho wake yeye mwenyewe tu.1Kor.2;11)
Sisi hatukuipokea roho ya Mungu wa dunia.bali Roho atokaye kwa Muumba .aliye Kweli.Tena twayanena tuliyokirimiwa na Mwumba wetu si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu .ambayo chanzo chake. Ni. Pepo.Tawala (Kol. 2;8)Bali yanayofundishwa na Roho wa Kristo.tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya Rohoni (2pet.1;20-21).1kor.2;3
Sasa ni budi tuzingatie tuambiwayo. Na mwenye utakatifu wake .soma Yn.15;3
17;17,Efe 5;25--27.
Aidha tuzingatie lile sharti la kuwa mwanafunzi wa Kristo ;nalo ni kukaa katika Neno lake litakasalo (Yn8;31--32,. 36.)na kuachwa huru kutoka utumwa wa dhambi na umilikiwaji na Mungu wa dunia hii (1Yoh.3;8;5;19).Kinyume chake ni kuwa mwanafunzi wa Mungu wa dunia na kuwa mmilikiwa wake .Huyu mwivi na kahaba kwa majina religioni na Mungu.
Ili kuokoa nafsi zetu na kizazi chetu tunapaswa kubadilika mara moja kwa kukaa katika Neno la Bwana wetu (Yn 8;31--32;. 15;7)bila Ajizi yoyote .Hapa ndipo penye usalama wetu wa uhakika na salama
Mbarikiwe sana.



0 comments:
Post a Comment