Subscribe:

Sample text

Sample Text

Tuesday, 31 December 2019

KUMJUA YULE MWIVI (YN.10:10) NA MWOVU (1YOH.5:19)

Ile habari tuliyoitafakari katika mada yetu "MWIVI NA KRISTO NENO LA KWELI".  Imefufikisha kwenye ukweli unaosemekana katika 1Yoh 4:6. Kwamba wapo Roho wa Kweli na Roho wa Upotevu .
1Yoh 5:19 Hutuambia kwamba dunia hukaa katika yule Mwovu .Ukweli huu unasemekana kwa namna nyingine katika 2Kor.4:3--4 Kuhusu "Mungu wa dunia "anayepofusha fikra za watu isiwazukie Nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Muumba mbingu na dunia.
Tumekwisha kuona kwamba Neno "MUNGU"  limebuniwa na Mtu wa kuasi .Mwana wa uharibifu .Yule mpingamizi  ajiinuaye nafsi yake juu ya Kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa (2Thes.2:3--4)
Tumeona kwamba Muumba amejihakikishia kwamba Yeye ni Umoja usiogawanyika wa nafsi Tatu :Kweli ,Neno la Kweli na Uzima wa milele .
Huyu ni Baba wa wote,Wala hana  hoja ya kujiinua nafsi zake katika chochote kile Wala kuabudiwa .Manabii wametuhakikishia jinsi Muumba wetu anavyochukia kuabudiwa
Kutokana na ukweli kwamba katika maskani ya mbinguni "Mungu"hayumo ,na kutokana na Ukweli kwamba "Mungu " hutokana na Mtu wa kuasi haiwezekani Muumba wetu atam ulikane kwa Jina hilo mbali na vile alivyojishuhudia mwenyewe ,Mungu hana nafasi yoyote katika maskani ya Muumba wetu.Mbinguni .Na Muumba wetu hana chochote katika Mungu.Kutokana  na Kweli hizi ni dhahiri kwamba. Mungu ndiye MWIVI aliyesemekana katika. Yn.10:10
Huo ndiyo ukweli ,dunia inatawaliwa na Mwivi ,Ibilisi Yn8:44  Dunia Inamwabudu na kumwomba Ibilisi ili Ipate Nini kama siyo maangamizi tu?

Tuzinduke usingizini .Tupokee Ufufuko Kristo atuangaze (Efe.5:14)Tukae katika Neno lake tu Yn.8:31---32.Humo  ndimo ulimo Uzima na usalama wetu

Sunday, 29 December 2019

MWIVI NA KRISTO NENO LA KWELI

MWIVI HAJI ILA AIBE,ACHINJE NA KUHARIBU(YN10:10a)
Katika 2Thes 2:3--4  Paulo Mtume hutueleza habari za yule Mtu wa kuasi,mwana wa uharibifu :yule mpingamizi ,ajiinuaye nafsi yake juu ya Kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa :hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu :akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
Hivyo ndivyo pepo watawala walivyowatumikisha watu kwa njia ya Torati ya Musa wajitengeneze kuwa miungu ya dunia kuabudiwa na watu badala  na kinyume Cha Mwumba mwenyewe.kwa sababu wamejitengeneza hivyo ,hawa miungu ni sanamu za kiroho .Na ndiyo hawa tuliotakiwa katika 1Yoh.5:21 kwamba tujilinde nafsi zetu na hao sanamu.Na ndiyo kahaba na wazinzi waliosemekana katika 1Kor.6:15--20  Ufu.14:4,.  8. Na Ufu.18:3

KRISTO NENO LA KWELI AMEKUJA ILI TUWE NA UZIMA ,KISHA TUWE NAO TELE.(YN.10:10b)
1Yon.5:6 Hutuambia kwamba Kristo Neno la Kweli amekuja katika Maji na katika Damu.Amekuja katika Maji ili kututakasa na kutusafisha ili atunyweshe Tena maji yake ya kutububujikia uzima wa milele (Yn.4:10,. 14:.  7;37--39).Maana Ndani yake Kristo ndimo ulimo uzima (Yn.1:4. 6;63).Na amekuja katika Damu ili kuwa dhabihu ya Ukombozi ,kutupatanisha na Baba (Mt. 26:28. Ebr.2;17;.  Kol. 1:14;.   1Yoh. 2:1--2)Hata akatangaza ukweli wake kwamba dhambi zetuna uasi  wetu haukumbuki Tena (Ebr.10:17)
Kristo amekuja kututoa katika hali ya kuwa wana wa giza la MUNGU wa dunia ,na kutuingiza  Tena katika hali ya kuwa wana wa Nuru (Yn  8:12;   12:36,.  46). Yake yeye mwenyewe.
UTAKATIFU UKO KATIKA KRISTO NENO LA KWELI TU.
Mambo ya Kristo Neno la Kweli hakuna ayafahamuye ila Roho wake yeye mwenyewe tu.(1Kor.2:11)
Sisi hatukuipokea roho ya Mungu wa dunia ,Bali  Roho atokaye kwa Muumba ,aliye Kweli .Tena Twayanena tuliyokirimiwa na Mwumba wetu si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu ,ambayo  chanzo chake ni pepo watawala (Kol.2:8),Bali yanayofundishwa kwa Roho wa Kristo ,Tukiyafasiri mambo ya Rohoni  kwa maneno ya Rohoni(2Pet.1:20--21). 1Kor.2:3
Sasa ni budi tuzingatie tuambiwayo na mwenye utakatifu wake ,soma Yn.15:3;. 17:17 ,19;. Efe 5:25---27.
Aidha tuzingatie lile sharti la kuwa mwanafunzi w Kristo;Nalo ni kukaa katika Neno lake litakasalo (Yn 8:31 --32,. 36)na kuachwa huru kutoka utumwa wa dhambi na umilikiwaji na Mungu wa dunia hii.(1Yoh.3:8;. 5:19).Kinyume chake Mtu huwa  Mwanafunzi wa Mungu wa dunia na kuwa mmilikiwa wake  huyu mwivi na kahaba kwa majina "religion " na "Mungu".
Ili kuokoa nafsi zetu na kizazi chetu tunapaswa kubadilika mara moja kwa kukaa katika Neno la Bwana wetu (Yn.8:31---32;.  15:7) bila Ajizi yoyote .Hapo ndipo penye usalama wetu wa uhakika na salama
Mbarikiwe sana.

Thursday, 26 December 2019

HATMA YA KUUKULIA UKWELI WA MUNGU NA KUMJUA MUNGU KWA NJIA YA UAMINIFU KWA INJILI.

Katika safari yetu hiyo tumekutana na ukweli usiopingika kwamba pepo wamejiita "Legioni "kutokana na wingi wao (Mk.5:9).
Ambao kwao Mwinjili luka yeye amekazia Jina " Jeshi "(Lk.8:30).
Katika hali hiyo ya uwingi wao .pepo watambulikana kuwa "Mtu wa kuasi,mwana wa uharibifu,yule mpingamizi ajiinuaye nafsi yake juu ya Kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa.hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu." 2Thes.2:3--4

Katika hali ya  kuwa nje ya ukweli huu,Dunia yote pia tumekuwa katika kosa la kumtambua Baba na Mkombozi wetu aliye utimilifu wote,kuwa Mungu.
Sasa ,baada ya kuona jinsi pepo katika uwingi wao na mbinu yao ya kujitengenezesha kuwa Mungu wa kuabudiwa, Nje kabisa ya Muumbaji mwenyewe na taratibu na utukuzwaji wake,baada ya kunua utimilifu wake usio na upungufu wowote,na baada ya kuhakikishiwa kwamba Muumba wetu ni Roho (Yn.4:23---24)aliye Umoja usiogawanyika wa nafsi  Tatu:Kweli ,Neno la Kweli na Uzima wa milele (1Yn.5:8).Itakuwa kioja na Ubatili mtupu kumfikiria Baba wa mababa naye ni miongoni mwa hao Miungu akilitumia Jina lililobuniwa na hao adui zake ajiinulie Nafsi zake Tatu.
Muumbaji wetu hawezi kuwa Mungu .Muumba  wetu Yeye ni Kweli (Yn3:33;. 8:26).  Ibilisi aliye Mwuaji au mwana wa uharibifu 2Thes.2:3  Ndiye aliye Mungu wa dunia .Yeye aliye Roho huenenda na watu wake kwa Roho na Kweli (Yn.4:24; Gal 5;16--17)Huzichukia Ibada za kimwili Yer.7 yote ,. 44 Yote,. Isa.66:1---4;.   1:10---18;.   Zab.50:7---23;.  Amo.5;21--27.
Hii ndiyo hatma ya safari zetu za " kuukulia ukweli wa Mungu ". Na ile ya " Kumjua Mungu " Mungu ni yule. "Pepo". Anayepigana na Muumba (Gal .5:16--23)  Ile Roho ya upotevu  aishilie mbali .Tuongozwe sasa na Roho wa Kweli tu ( 1Yoh .4:6
Marikiwe

Tuesday, 24 December 2019

AONDOA LA KWANZA ,ILI KUSUDI ALISIMISHE LA PILI(EBR.10;9

Kristo Neno la Kweli amekuja kuliondoa agano la Kwanza ambalo kwalo pepo watawala (2Thes 2;3-4) waliwatumikisha watu (Gal.4:3) kwa njia ile iliyosemekana katika (2Thes2:9--10) ili watu waukatae ukweli wasije wakaokoka (Yn.12:40) Ndiyo Maana tunaambiwa katika Kol. 2:18   "Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu ya wokovu mkaendelea kung'ang'ania na pepo watawala " legion " au Mungu .kamwe tusipotewe na ule ukweli kwamba kwa njia ile iliyosemekana katika 2Thes.2:3--4 Pepo watawala waliwatumikisha watu kwa njia ya torati au sheria ya Musa kujitengenezea kuwa miungu ya kuabudiwa kupingana na makusudi na taratibu za yeye aliye baba wa wote .
Kristo Neno la Kweli akaliteka jina Yoshua (Yesu).ambalo liliendeleza utawala wa torati ya Musa kuukomesha utawala wa torati ya Musa Rum.10:4.

Hii ni hekima ya Muumba ambayo wenye kuitawala dunia hii (hao pepo )hawaijui hata moja .Maana kama wangaliijua ,wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu (1Kor.2:8).kwa sababu ya kutojua Siri hii ,Jina Yesu (Yoshua )likawa mwisho wa Jina Yesu (Yoshua )pale msalabani kwa utukufu wa Kristo Neno la Kweli(Kol.2:13--15)Na torati ikafikia mwisho wake.
Kwa tendo hilo, Kristo Neno la Kweli ,akawa amehitimisha Imani mpya (Ebr,12:2)Na kwamba Mtu akiwa katika huyu Kristo amekuwa kiumbe kipya : Ya kale yamepita tazama ! Yamekuwa mapya (2kor.5:17).
Tunapohimizwa kwenda kwa Roho katika Gal.5:16, ni pamoja na kutomwangalia Yesu wa kimwili (2kor.4:18).Yesu wa kimwili ,Yesu wa Torati.ni kivuli tu Cha Kristo Neno la Kweli adumuye milele .Kazi y kivuli au nakala iliishia pale msalabani ambapo torati imefutwa na kuondolewa Isiwepo tena (Kol 2:13--15)
Ndiyo maana tunaambiwa ule ukweli wa Gal.5:4,. "Mmetengwa na Kristo ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria ambayo ni torati ya Musa.
Mbarikiwe san

Monday, 23 December 2019

MWIVI HAJI  ILA AIBE ,. ACHINJE NA. KUHARIBU(YN.10:10a)
Katika 2Thes.2:3--4. Paulo Mtume hutueleza habari za yule Mtu was kuasi.Mwana  wa uharibifu ;. Yule mpingamizi.ajiinuaye nafsi  yake juu ya Kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa : hata yeye mwenyewe kuketi hekalu la Mungu :akijionesha  nafsi yake kana kwamba yeye ndiye  Mungu.
Hivyo ndivyo pepo watawala walivyowatumikisha watu kwa njia ya torati ya Musawajitengeneze kuwa miungu ya dunia  kuabudiwa na watu badala na kinyume Cha Mwumba mwenyewe.kwa sababu wamejitengeneza  hivyo .hawa miungu  ni sanamu  za kiroho .Na ndivyo  hawa tuliotakiwa  katika 1Yoh.5;21 kwamba tujilinde  nafsi zetu na hao sanamu.Na ndiyo kahaba na wazinzi waliosemekana katika 1Kor.6;15---20.   Ufu.14;4,.     8.  Na Ufu.18;3.
KRISTO NENO LA KWELI AMEKUJA ILI TUWE. NA UZIMA ,KISHA   TUWE NAO TELE(YN 10;10b)
1Yon.5;6.  Hutuambia kwamba KRISTO NENO la. Kweli amekuja katika Maji na katika Damu.Amekuja   katika Maji  ili kututakasa na kutusafisha ili atunyweshe Tena maji yake ya kutububujikia uzima wa  milele.(Yn4;10.  14;7;37--39 Maana  Ndani yake Kristo. Ndimo ulimo uzima (Yn 1;4;.  6;63).  Amekuja katika damu ili kuwa dhabihu ya Ukombozi .kutupatanisha na Baba. (Mt.26;28.   Ebr .2;17; Kol. 1;14;  1Yoh 2;1--2)
Kristo. amekuja kututoa katika hali ya kuwa wana. Wa giza la Mungu wa Dunia .na kutuingiza Tena katika hali ya kuwa wana wa Nuru(Yn.8;12;.  12;36.  46)  yake yeye mwenyewe.
UTAKATIFU UKO KATIKA KRISTO  NENO LA  KWELI TU.

Mambo ya Kristo neno la Kweli hakuna ayafahamuye ila Roho wake yeye mwenyewe tu.1Kor.2;11)
Sisi hatukuipokea roho ya Mungu wa dunia.bali Roho atokaye kwa Muumba .aliye Kweli.Tena twayanena tuliyokirimiwa  na Mwumba wetu si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu .ambayo chanzo chake. Ni. Pepo.Tawala (Kol. 2;8)Bali  yanayofundishwa na Roho wa Kristo.tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya Rohoni (2pet.1;20-21).1kor.2;3

Sasa ni budi tuzingatie tuambiwayo. Na mwenye utakatifu wake .soma Yn.15;3
17;17,Efe 5;25--27.
Aidha tuzingatie lile sharti la kuwa mwanafunzi wa Kristo ;nalo ni kukaa katika Neno lake litakasalo (Yn8;31--32,. 36.)na kuachwa  huru kutoka utumwa wa dhambi na umilikiwaji na Mungu wa dunia hii (1Yoh.3;8;5;19).Kinyume chake ni kuwa mwanafunzi wa Mungu wa dunia na kuwa mmilikiwa wake .Huyu mwivi na kahaba kwa majina religioni na Mungu.
Ili kuokoa nafsi zetu na kizazi chetu tunapaswa kubadilika mara moja kwa kukaa katika Neno la Bwana wetu (Yn 8;31--32;.  15;7)bila  Ajizi yoyote .Hapa ndipo penye usalama wetu wa uhakika na salama
Mbarikiwe sana.

Tuesday, 17 December 2019

KWA NINI NIMEKATAA KUSALIWA NA RE--LEGIONI YEYOTE ILE !

KWA NINI NIMEKATAA KUSALIWA NA RE-LEGIONI YEYOTE ILE !
Ni miaka kadhaa imepita tangu niache kuhudhuria Ibada.
Hii inatokana na kuhamasika nilikohamasika na Barua "UT  Unum Sint" iliyo andikwa na Muhashamu sana Papa Yohani Paulo 11 mwaka 1995.
Ile hamasa ya kuwa waaminifu kwa Injili kuwa na fikra mpya. Kuwa na mtazamo mpya wa mambo.kuitafuta kweli na kushikamana nayo.Imenifikisha kwenye ukweli usiopingika kwamba "Re--ligion"  ni kushikamana na mapepo yali yaliyojitambulisha katika Mk5:9. Na kumwomba Mungu ni kuliomba lile sanamu la kiroho (1Yoh5:21)  lililojitengeneza lenyewe kwa utaratibu ulioelezwa katika 2Thes  2:3--4 kwamba yule mtu wa kuasi.mwana wa uharibifu.yule mpingamizi ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho "Mungu " ama kuabudiwa :hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la "Mungu"akijionesha nafsi yake kwamba yeye ndiye Mungu.Mungu ni huyo pepo mchafu .Huyo Mungu  pepo mchafu hawezi kuwa yule aliyefunuliwa na kristo Neno la kweli .kwamba ni "KWELI"
Na mwana wa Kweli hawezi kuwa yule yesu wa Torati ya Musa ambayo imemghadhibisha kweli hata akaifuta na kuiondoa isiwepo tena.Tendo ambalo limelelekea pepo .Mungu katika ujumla wao.kunyang'anywa nguvu zao :na kuanza imani mpya katika kristo Neno la Kweli Ebr.12:2.na kwa imani hii mpya ya kale yamepita .Tazama yamekuwa mapya(2Kor.17)
Kuendelea na mambo ya akina legion na sanamu "Mungu "ni ubatili mtupu .ndiyo maana kuna kutengwa na kristo Neno la kweli katika kuenenda kitorati.jambo ambalo nimelikataa tangu miaka kadhaa iliyopita.kamwe lisifanyike katika Umzoga wa kibanda changu  hiki.
Cha kufanyika badala ya maibada batili kwa mapepo ambayo utawala wao umefutwa rasmi pamoja na torati yao.ni kile ambacho Mhashamu Papa Fransis  amekisema katika kifungu cha 121 cha barua yake ya kichungaji kwamba "kile ulichokuja kutambua .kile kilichokusaidia kuishi na kikakupa matumaini.ndicho unachohitaji pia kukiwakilisha kwa wengine"
Kwa kuwa kibanda hiki muda wake wa kutumiwa na kristo utakuwa umepita .wewe utakuwa umebarikiwa sana ikiwa utashirikiana na wenzio kuniwakilisha kufanya tendo la kuwasilisha kwa kusanyiko litakalokuwapo.katika vipindi mbali mbali vya kusanyiko . Vile vile vilivyosemekana hapo juu kwa kutumia blogger yangu KUUKULIA UKWELI WA MUNGU

Monday, 16 December 2019

"UT UNUM SINT"

"UT UNUM  SINT"
BARAGUMU LA KIKOROKORONI.

Kwa kadiri ya Eze.3:16--21 "UT UNUM SINT" Ile barua ya kichungaji iliyoandikwa na papa Yohana paulo 11 mwaka 1995.ni baragumu la kikoro koroni au kiulinzi.kuitangazia dunia kwamba iko kwenye njia potevu.
Katika kifungu cha kwanza (1) Barua hiyo tunakuta habari za Mpinga kristo asemaye ."Mtu si chochote .bali ni kitu cha kiudongo tu ambaye anapaswa aishi kana kwamba hakuna Baba wa wote aliye juu ya yote.atendaye kazi katika yote na ndani ya yote.(Efe.4:6)
Dhidi ya mtazamo huo wa kimpinga kristo uliopelekesha dunia upotevuni.kifungu cha 15 huwataka waamini kuwa waaminifu kwa Injili.kuwa na fikra mpya na mtazamo mpya wa mambo.kinyume kabisa na fikra na mtazamo wa mambo ambao umeipeleka dunia upotevuni.
Kifungu cha 18  chaeleza ubatili wa umoja wowote ule au makubaliano yoyote yale yaliyofikiwa kwa gharama ya ukweli.Hii ni sababu makubaliano kama hayo hupingana na Baba wa wote aliye "Kweli"(Yn8:26 .  3:33) asiye na uongo wowote ule ndani yake(1Yoh.2:21.
Katika ujumla wake.kifungu cha 18 ni rejea mada DIGNITATIS HUMANAE ya VATIKANI 11 ya 1965.mada ambayo ilisisitiza kwamba hadhi au uthamani wa Utu .Uko katika kutafuta"Kweli" na kuambatana nayo.
Kifungu cha 32 chaelekeza kwamba katika safari ya kutafuta kweli .wadau husika wawe wanashirikishana "Kweli" wanayoifikia .kwa njia ya mafundisho.mawasiliano  au kwa njia ya mazungumzo.
Katika jambo hili.Baba na Mwokozi wetu ashukuriwe na kutukuzwa sana kwa kuwezesha njia za mitandao .kama vile Whatsapp ,Facebook,Instagram n.k. yeye aliye Baba wa wote.aliye juu ya yote .atendaye kazi katika yote na ndani ya yote .awahifadhi na kuwabariki kwa Baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa Roho ndani yake kristo Neno la Kweli wahudumu wa vyombo hivyo (efe1:3)
Kifungu cha 36 chasema kwamba wadau husika wanapaswa kuing'ang'ania Imani walio fikishiwa na roho wa kweli ,bala mapunguzo yoyote .wala makubaliano ya kiwepesiwepesi .Vifungu 77--78 Vinagisia tamanio la kufikia kanisa lililo moja .takatifu .katoliki na la Kimitume.
Kifungu cha 80 chagusia swala la Upakwa mafuta uliyo kwa wote bila ubaguzi wa aina yoyote ile.
Korokoroni au Mlinzi amekwisha kutimiza jukumu lake mbele za Bosi wake aliyemtuma .hadaiwi chochote .
Je? Wewe na mimi tunalichukuliaje jambo hili la kuwa waaminifu kwa Injili ,kuwa na fikra mpya , kuwa na mtazamo mpya,kuitafuta kweli na kuing'ang'ania kwa sifa na utukufu wa Baba yetu atupendaye upeo kwa upendo wa milele ? Tunamrudishia nini ?
Je ? Ni busara kuendelea kumng'ang'ania aliyetupeleka upotevuni kwa hasara yetu ya milele ?
Mimi mwenzio nimemkataa sasa na hata milele .Hata maiti yangu nimekwisha kutangaza Jumuiani mbele ya Paroko ."SITAKI IFANYIKE IBADA YA KIDINI YOYOTE ILE"

LUKA ROKI CHAMAYOMBE
0714118428
Www.chamayombe.blogspot.com