Subscribe:

Sample text

Sample Text

Wednesday, 4 October 2017

TANZANIA KUKUMBWA NA TETEMEKO LA KIROHO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

Tanzania ambayo kihistoria imekuwa na sifa ya kuwa nchi ya amani, hata kuwa kimbilio la wakimbizi, sasa amani iko katika tetemeko la kutisha nchini Tanzania.
NANI WA KULAUMIWA?
Hili ni tetemeko ambalo liko katika ulimwengu wa roho. Tendo lolote la kulichukulia tetemeko hili kimwilimwili, tendo hilo litakuwa ni tendo la kumwabudu Yule mwovu aliye Baba wa Uovu (Kol.2:18). Na ni hatari kubwa.
Maelezo Na.3 ya Yn.8:12 ya Bibilia Takatifu toleo la Iringa hufafanua usemi wa Kristo Neno la Mungu kwamba Yeye amekuja kuwa Nuru ya Ulimwengu, na kwamba yeye amfuataye hatkwenda gizani kamwe, bali atakuwa na Nuru ya Uzima.
Maelezo Na.3 yanasomeka kama ifuatavyo: “Nuru na giza ni kielelezo cha falme mbili zinazohitilafiana na kupigana, yaani Ufalme wa Mema utawaliwao na Kristo, na Ufalme wa uovu unaomilikiwa na shetani. Kila ufalme unajaribu kuushinda mwingine. Watu wanagawanyika baina ya wana wa Nuru na wana wa giza kadiri waishivyo, kwa mvuto wa Nuru Kristo au kwa mvuto wa giza shetani. Wana hao wote watambulikana katika vitendo vyao”.
Kuhusu hao wawili wanaopambana, Biblia yenyewe hutuambia “Basi nasema, Nendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho na Roho kushindana na mwili kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka (Gal.5:16-17)”.
Gal.5:19-21 hutuorodheshea matendo ya mwili ambayo ni uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, UADUI, UGOMVI, Wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na kwamba wayatendao mambo ya jinsi hii hawataurithi ufalme wa Mungu.
Kinyume chake, Gal.5:22-23 hutuorodheshea tunda la Roho ambalo ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole kiasi.
NAFASI YA MAOMBI NA MAOMBEZI
Wewe na mimi tunakabiliwa na hawa wawili wapiganao ambao wanatugombania. Huyu hutaka tuwe maskani au Hekalu lake, na huyu hutaka tuwe kiti chake: 1Yoh.3:8a hutuambia kwamba atendaye dhambi (atendaye yale yaliyo orodheshwa katika Gal.15:19-21) ni wa Ibilisi.
Na anayemilikiwa na Ibililisi hukaliwa na Ibilisi kuwa kiti chake. Katika hali hiyo, mhanga hupofushwa; na moyo wake hufanywa kuwa mgumu kuiona na kufahamu iliyo kweli asije akamwongokea Mungu Kweli akamponya Yn.12:40; 2Kor.4:3-4).
Ndiyo maana Yn.8:47 hutuambia kwamba asiye wa Mungu Kweli hayasikii maneno ya Mangu kweli. Na kwa sababu ya kumilikiwa huko na Yule mwovu, Mungu Kweli hamsikii mhanga au mmilikiwa wa Yule mwovu (Yn.9:31). Kwa sababu hiyo, kulikurupukia swala la maombi na maombezi, ni kupoteza wakati na nyenzo katika ujumla wake. Watu wataomba na kuombea; lakini wataishia kuwa wambea.
MAPASWA YALIYOKO MBELE YETU
Kukubali kukusanywa kundi moja na Jemedari mmoja tu (Yn.10:16; 11:52). Vinginevyo, tunaambiwa katika YBS.34:23-24. “Iwapo mtu mmoja anajenga, mwenzake akabomoa, je! Faida yao ni nini ila kazi bure tu? Iwapo mtu mmoja anaomba, na mwingine analaani; Je! Bwana ataisikia sauti ya yupi?” Hivyo, katika vita hivi dhidi ya Ibilisi tunapaswa kuwa wamoja sawasawa na Neno la Mungu Efe.4:3-6.
Ili kuufikia Umoja huo tunapaswa kunyweshwa (1Kor.12:13) na kuvalishwa (Gal.3:27) utimilifu wote wa Mungu katika Kristo Neno la Mungu Kol.2:10; Efe.3:19). Ili hili lipate kutimilika, tunapaswa kulenenda kwa jinsi ya Kristo tukiwa tumeachana kabisa na kila kilicho cha kibinadamu, wala mafundisho ya awali ya ulimwengu (Kol.2:8-10). Kwenda kwa jinsi ya Kristo ndiko kule kwenda kwa imani 100% (Gal.5:4-5). Kwenda kwa jinsi ya Kristo ndiko kule kuenenda kwa Roho (Gal.5:16) sawasawa na mapenzi ya Mungu ambaye hutafuta watu wamwabudu katika Roho na kweli (Yn.4:23-24; 1Yoh.5:14-15).
KWA ANGUKO LA ADAMU NA EVA, WATU WOTE NI WA IBILISI (1Yoh.3:8a)
Kutokana na ukweli wa mambo ulivyo, watu wote wamekuwa wa Ibilisi kwa dhambi ya Adamu na Eva. Lakini kwa upande wa mpiganaji wa upande wa pili ni kwamba kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa (Ebr.10:14). Na utakaso umetimilika kwa kutolewa Mwili (Nafsi) wa Kristo Neno la Mungu mara moja tu (Ebr.10:10); ambamo ndani yake mna maji safi na hai yaliyomo katika Damu ya Yesu, Roho Mtakatifu (Yn.7:37-39) aliyemo katika Neno la Mungu (Ebr.10:19-22; Yn.17:17, 19; Efe.5:25-27).
Utakaso ni kule kuondolewa kwa ule mlima farakanishi ambao Yule mwovu ameupandikiza ndani yetu kuharibu mahusiano na mawasiliano na Mungu Kweli. Mlima huo unapoondolewa, ndipo Mungu huwa ndani ya nafsi ya mtu na nafsi ya mtu ndani ya Umoja wa Nafsi Tatu za Mungu Kweli. Hapo mtu huwa Umoja na Mungu. Mungu huwa ndiye Mtendaji Mkuu ndani ya nafsi ya mtu. Hapo ndipo nafsi ya mtu katika kuwa umoja na Nafsi Tatu za Mungu huwa mshindi na zaidi ya mshindi dhidi ya Ibilisi (Rum.8:37).
SIRI YA UMOJA UNAOTAKIWA, IMO KATIKA KUPOKEA HIYO ZAWADI YA UTAKASO
ambao hufuatiwa na kukamilishwa katika Umungu. Isisahaulike wala kupuuzwa kwamba pale Msalabani Kristo Neno la Mungu alionja mauti kwa ajili ya kila mtu; bila kujali dini, jinsia, umri, cheo, wala chochote kile kiwacho. Ni kwa ajili yako hapo kama ulivyo, na mimi hapa kama nilivyo.
Tumeona hapo juu kwamba Kristo Neno la Mungu alionja mauti kwa ajili ya kila mtu. Kristo Neno la Mungu alikufa kutuokoa kutoka utumwa wa dhambi ili atuweke huru kweli kweli (Mt.1:21; Yn.8:36) maana atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi (Yn.8:34).
Wasomi wa Bibilia tunaona kwamba kila akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila atendaye dhambi hakumwona wala hakumtambua (1Yoh.3:6). Na katika Kol.2:23 tunaambiwa kwamba ibada mnazojitungia wenyewe ambazo hazifai kitu kuzizuia tamaa za mwili zile zilizo- orodheshwa katika Gal.5:19-21.
Sasa sisi tunataka tuwe na ujasiri mmoja wa kumkaribia Mungu wetu kuhusu hili janga analotuletea Ibilisi. Tusipoteze ukweli kwamba Kristo Neno la Mungu Kaonja mauti kwa ajili ya kila mmoja wetu. Lengo la kufanya hivyo ni kututoa kwenye utumwa wa dhambi tuweze kuhusiana na kuwasiliana na Mungu katika Umoja wake wa Nafsi Tatu (Yn.17:21-23; 1Yoh.4:13).
Kwa kusimama katika aya hizi Kol.2:23 na Gal.5:19-21) kiukweli, bila uongo wala unafiki wowote mbele za Mungu Roho (Yn.4:24) katika Umoja wa Nafsi Tatu. “Kweli, na Neno, na Roho Mtakatifu, zipime ibada zinazoendeshwa kwenye dini au dhehebu lako lolote lile, je zinafaa chochote kuzizuia tamaa za mwili zilizoorodheshwa katika Gal.5:19-21? Kama jibu la kweli ni ndiyo mbele za Mungu Kweli basi ni vema na vizuri sana! Jibu likiwa hapana; basi ujue kwamba uko hatarini; kwani imekuwa kwamba uko mbali na Mungu.
Lakini hiyo isikutishe. Iko faraja kutoka kwa Mungu. Kwamba bado una uhai huu wa mwili wa nyama hata sasa ni kwa sababu Mungu kweli hapendi wewe upotee, bali kwamba umwongokee Yeye uwe mzima (2Pet.3:9). Na siku na wakati uliokubalika wewe kupata msaada wa Roho Mtakatifu, ni sasa.
Hivyo, nakuomba wewe rafiki yangu mpendwa wa Kristo Neno la Mungu, uliye mpenzi wa kujiunga katika jeshi la Kristo Neno la Mungu kuuangamiza ufalme wa Ibilisi kwako, kwa Tanzania na dunia katika ujumla wake, na kuomba kwanza ya yote kupokea zawadi au neema ya ondoleo la dhambi au utakaso kwa njia ya imani ya 100% (Mk.11:23) kwamba umeoshwa kwa maji safi na hai yaliyomo katika Damu ya Kristo Neno la Mungu, Roho Mtakatifu aliyemo katika Neno la Mungu ambaye ndiye Mwombezi wetu mbele za MUngu kweli.
Jambo hilo lifuatiwe na Ukweli kwamba Mungu kweli amesema, kwa Utakazo huo sasa amekushirikisha utimilifu wote wa Umungu wake. Kama Yeye alivyo ndivyo ulivyo na wewe duniani hapa (1Yoh.4:17); na kwamba dhambi zako na uasi wako uliopita hataukumbuka tena hata milele (Rum.3:25; Ebr.10:17).
Katika hali hiyo ya amani na Mungu kweli, sasa kwa nafsi yako mshukuru Mungu kwa ajili yako, kwa ajili ya Taifa letu Tanzania na kwa dunia katika ujumla wake.
UBARIKIWE SANA!!!
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0787 765 759
0714 118 428
0753 298 707
Chamayombe37@gmail.com

TUTENDEJE NDUGU ZETU (Mdo.2:37)?

Tumepata kujua kwa uhakika kwamba:
Mungu wetu ni Roho (Yn.4:24) aliye katika Umoja wa Nafsi Tatu ambazo ni Kweli, na Neno na Roho Mtakatifu.
Mbinguni anakokaa huyu Mungu ni huu Umoja wa Nafsi Tatu, na
Ufalme wake ambao ni wa haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu (Rum.14:17), umeundwa na huu huu Umoja wa Nafsi Tatu.
Baada ya kujua kweli hizi, sasa tutendeje?
Kabla ya yote, tunapaswa kufahamu kabisa kwamba shida au tatizo linalotukabili ambalo linahitaji kushughulikiwa ni lile kosa tulilolirithi kutoka kwa wazazi wetu wa kwanza, Adamu na Eva. Kosa lenyewe ni lile tendo la kumwamini Ibilisi na kumfanya Mungu wa pekee wa Kweli kuwa mwongo (Mw.2:16-17; 3:4-5).
Katika hili, Mdo.2:38 humnukuu Petro Mtume akisema, “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa Jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Petro Mtume amesema, “Tubuni mkabatizwe……….” Kubatizwa ni kufanywaje? Kwa kadiri ya 1Kor.12:13, kubatizwa ni kunyweshwa Roho Mtakatifu. Na kwa kadiri ya 1Yoh.4:13, hushirikishwa Roho wa Mungu ndio huko huko kubatizwa. Na kwamba kwa tendo hilo, mtu huwa ndani ya Mungu ambaye ni Roho mwenye Nafsi Tatu, na Mungu Roho mwenye Nafsi Tatu naye huwa ndani ya mtu husika. Kwa tendo hilo mtu husika huwa ameingizwa na kujumuishwa katika Umoja wa Nafsi Tatu za Mungu wa pekee wa Kweli.
Kwa tendo la Ubatizo huo katika Roho Mtakatifu, Mungu wa pekee wa Kweli amejibu 100% lile ombi alilowaombea watu wake siku moja kabla ya kusulubiwa kwake (Yn.17:21-23). Kwa ubatizo huo, wahusika wamezaliwa mara ya pili kwa Neno la Munu lenye uzima lidumulo hata milele (1Pet.1:23). Kwa Ubatizo huo wahusika wamehuishwa au kufufuliwa na kuketishwa pamoja na Kristo katika ulimwengu wa Mungu Roho aliye katika Umoja wa Nafsi Tatu (Efe.2:5-6; Kol.2:13-15).
Kwa ubatizo katika Roho Mtakatifu, wahusika wamezaliwa kwa Neno la Mungu lenye uzima lidumulo hata milele. Lakini “Neno la Mungu” ndilo Jina halisi la Kristo Yesu, Jina ambalo, kwa kadiri ya Ufu.19:12-13, lilikuwa siri ya Mungu. Jina ambalo lilidhihirishwa na Yesu mwenyewe (Yn.17:6, 26), na ambalo, kwa kadiri ya Mdo.4:12, ndilo Jina pekee tulilolipewa wanadamu litupasalo sisi tuokolewe kwalo, kama tulivyoona katika 1Pet.1:23.
SHARTI LA UBATIZO HUO NI KUTUBU
Petro Mtume alisema, “Tubuni mkabatizwe…..” Kwa maana kwamba sharti la kubatizwa ni “kutubu”. Kwamba ili mtu apate kubatizwa, sharti atubu. Na kutubu si swala la kutamka maneno tu. Mbona hilo hata kasuku hulifanya wakizoezwa. Kutubu ni tendo la kufanya kinyume kabisa cha kosa lililofanywa. Kutubu ni kufanya mapinduzi dhidi ya kosa.
KOSA MAMA NI LIPI?
Ni kwamba baada ya kujiumbia mtu wake awe nafsi kwa mfano na sura yake Yeye mwenyewe aliye Roho mwenye Nafsi Tatu zilizo Umoja, hata kumshirikisha Pumzi au Roho wake atiaye uzima (Mw.1:26; 2:7; Yn.6:63), Mungu alimwagiza mtu wake jinsi ya kuenenda.
Agizo lilikuwa kwamba asile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabays; kwa tahadhari kwamba siku atakayokula matunda ya mti huo atakufa hakika (Mw.2:17).
Ibilisi katika umbo la nyoka, akamkanushia Eva kwa kumwambia, “Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu mkijua mema na mabaya” (Mw.3:4-5).
Eva na Adamu wakawa wameshawishika kumwamini na kumtii shetani, na kumfanya Mungu mwongo hata kumwasi kabisa.
Hiyo ndiyo dhambi mama hapa duniani. Kwamba shetani ndiye wa kuaminiwa na kumtii. Na kwamba Mungu si wa kuaminiwa wala kumtii, kwa sababu ni mwongo.
Sasa, ili apate ubatizo uliosemekana hapo juu, mtu anatakiwa kufanya mapinduzi. Sharti amwamini Yeye (Neno la Mungu) aliyetumwa na Yeye (Kweli, Mungu Baba) (Yn.6:27); na kuachana kabisa na Yule muuaji ambaye hasimami katika kweli Yule mwongo aliye baba wa uongo. Mapinduzi hayo ndiyo kutubu; ndiyo toba ya kweli.
Lakini ili kubatizwa katika Roho Mtakatifu, ili kunyweshwa Roho Mtakatifu kunahitajika toba ya kina, siyo ya kijuujuu tu. Toba ya kina ni ile ya kumkaribia Mungu katika hali ya kuwa mkweli 100% kwa imani ya 100% kwamba umenyunyiziwa Damu ya Yesu, uachane na dhamiri mbaya. Uache kuhukumiwa na moyo wako; maana Nafsi yako imeoshwa kwa maji safi na hai yaliyomo katika Damu ya Yesu, Roho Mtakatifu ambaye yumo katika Neno la Mungu, Krito Yesu (Ebr.10:19-22).
Tumehamasishwa kulishika sana ungamo la tumaini letu lisigeuke; maana Yeye aliyeahidi kwa kusema, “Hii ndiyo Damu yangu ya agano imwagikayo kwa ajili ya wengi, Yeye aliyahidi kwa kusema, “Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa, ni mwaminifu wala hakuna uongo wowote ndani yake (Ebr.10:23; 1Yoh.2:21).
HITIMISHO
Kwa maelezo hayo yote jibu la swali lile “Tutendeje ndugu zetu?” Ni moja, nalo ni:
“HUU MWENENDO WA KUMFANYA MUNGU WA PEKEE WA KWELI KUWA MWONGO UKOME KWA KILA MMOJA WETU” Badala yake tutubu kwa maana iliyoelezwa hapo juu; na katika msingi wa kweli ya 100%, kila mmoja wetu, hata wewe hapo, awe na amani ya 100% na Mungu wetu wa pekee aliyefaulu 100% kuondoa tatizo la utumwa wa dhambi lililokuwa linatukabili na ambalo linakwamisha Uhalisia wa Ufalme wa Mungu duniani kwa hasara ya kila mhanga wa Ibilisi. Wote kwa sauti moja tuseme, “Kosa la kutomwamini Mungu Kweli, Roho aliye katika Nafsi Tatu, sasa BASI!!!” Na hivyo, kila mmoja wetu binafsi, kwa nafsi yake yote, kwa akili yake yote na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu itendayo kazi ndani yake aamini 100% kwamba pale Msalabani kazi imekwisha. Sasa yuko safi, na hakuna wa kumshitaki wala kumhukumu kwa lolote lile (Rum.8:31-39). Kila mmoja wetu awe na amani sawasawa na Neno la Mungu Rum.5:1.
Furahia Baraka unazobarikiwa na Mungu wa pekee wa kweli sasa hata na milele.
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0787 765 759
0714 118 428
0753 298 707
Chamayombe37@gmail.com

MJUE MUNGU WA PEKEE WA KWELI

Kwa kadiri ya Bibilia Takatifu, Mungu wa pekee wa Kweli ni Roho (Yn.4:24) aliye katika Umoja wa Nafsi Tatu ambazo ni Baba, na Neno na Roho Mtakatifu (1Yoh.5:8, toleo la Kimataifa au 1 Yoh.5:7 toleo la Agano Jipya tu).
Kwa kadiri ya Yn.8:26, Baba aliyemtuma Mwana ni “KWELI”, na Nafsi “NENO” ndiye Mwana kwa Jina lake halisi katika kweli (Ufu.19:12-13). Kwa Nuru hiyo, Mungu wa pekee wa Kweli ni Roho aliye katika Umoja wa Nafsi Tatu ambazo ni Nafsi Kweli, na Nafsi Neno na Nafsi Roho Mtakatifu. Nafsi hizi Tatu ni Mungu mmoja, Roho asiyegawanyika.
JE? MUNGU HUYU WA PEKEE WA KWELI, ROHO ALIYE KATIKA UMOJA WA UTATU WAKE MTAKATIFU ANAKAA WAPI?
Katika hali yake ya kutoweza kugawanyika ni kwamba kila Nafsi miongoni mwao hukaa katika kila Nafsi miongoni mwao. Kwamba kila Nafsi Miongoni mwao, ni Maskani au Makao ya kila Nafsi miongoni mwao.
Hivyo, Maskani ya Umoja wa Nafsi Tatu Takatifu ni Umoja wa hizo Nafsi Tatu zenyewe. Hivyo, huo Umoja wa Nafsi Tatu wenyewe ndiyo mbinguni hasa anakokaa Mungu Roho aliye katika Nafsi Tatu Takatifu: Kweli, ambaye ni Baba, na Neno, ambaye ni Mwana, na Roho Mtakatifu.
JE? UFALME WA MUNGU ROHO ALIYE KATIKA UMOJA WA NAFSI TATU NI UPI?
Ufalme wa Mungu Roho aliye Umoja wa Nafsi Tatu Takatifu ni huo Umoja wa Nafsi hizo Tatu ambao muundo wake ni kama ifuatavyo:-
(1) Nafsi Kweli ambaye ni Baba ndiye Mfalme.
(2) Nafsi “NENO” ambaye ni Mwana ndiye Waziri Mkuu peke yake anayesimamia yote.
(3) Na Nafsi “ROHO” Mtakatifu ndiye Katibu Mtendaji anayetekeleza yote.
Hapo Ufalme wa Mungu huyu umetimilika 100%.
Baada ya kumfahamu Mungu wa pekee wa Kweli, Maskani yake na Ufalme wake, hebu tuone maombezi ya Yesu kwa ajili yetu, Mwana amwambia Baba, “Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa;….” (Yn.17:24).
Na kabla ya kusema hilo alimwambia Baba “Wote wawe na Umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani, yako; hao nao wawe ndani yetu; ile Ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo Umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi (Yn.17:21-23).
Katika maombi haya. Nii wazi kabisa kwamba Kristo Neno la Mungu anataka watu wake wakamilishwe kwa kuingizwa na kujumuishwa katika ule Umoja wa Nafsi Tatu Takatifu, Kweli na Neno na Roho Mtakatifu.
Katika Ebr.10:14 imeandikwa “Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Hao wanaotakaswa, wanatakaswaje? Wanaotakaswa wanatakaswa kwa ile dhabihu, yaani Damu ya Yesu iliyotolewa mara moja tu na idumuyo hata milele (Ebr.10:10, 12).
Hao wanakamilishwaje? Hao wanakamilishwa kwa kubatizwa katika Roho Mtakatifu kuwa Mwili wa Yesu kwa kunyweshwa Roho Mtakatifu (1 Kor.12:13). Na kwa Ubatizo huo wahusika huwa wamamvaa Kristo (Gal.3:27)). Katika ujumla wake, wahusika huwa wananyweshwa na kuvalishwa utimilifu wote wa Mungu (Efe.3:19; Kol.2:9-10). Hapo wahusika huwa wamekamilishwa katika Ukamilifu wa Mungu pekee wa kweli, Roho aliye katika Umoja wa Nafsi Tatu: Kweli na Neno, na Roho Mtakatifu.
Maana, kama anavyosema katika 1Yoh.4:13 “katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Rono wake”. Na katika aya ya 17 tunasoma “Katika hili, pendo limekamilika kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu, kwa kuwa, KAMA YEYE ALIVYO, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu”.
Hapo ombi la Kristo Neno la Mungu, Yn.17:21-24, limetekelezwa 100%. Watu wake tumezaliwa katika Mungu Roho aliye katika Umoja wa Nafsi zile Tatu. Hapo sisi sote tumekuwa wazaliwa wa Mungu Roho aliye katika Umoja wa Nafsi Tatu Takatifu. Hapo sisi sote tumo ndani ya Umungu Roho ulio katika Nafsi Tatu za Mungu wa pekee wa kweli. Hapo sisi sote, hapa hapa duniani tulipo, tumo ndani ya Ufalme wa Mungu wa pekee wa kweli. Hapo sisi sote tumo mbinguni, Umoja wa Nafsi Tatu Takatifu, hapa duniani tulipo (Yn.17:14-15).
Ndipo tunapoambiwa, “Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila atendaye dhambi hakumwona Yeye, wala hakumtambua. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu (1Yoh.3:6, 9).
Na katika 1Yoh.5:18 twasoma, “Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala Yule mwovu hamgusi”. Katika hili, ibilisi yuko kazini kukupofusha wewe rafiki na ndugu yangu, kukupofusha na kufanya nafsi yako iwe nzito kuufahamu ukweli huu eti wewe usimwongokee Mungu wa pekee wa kweli akuponye (Yn.12:40 na 2Kor.4:3-4).
Kazi hii shetani ameifanya na anaifanya. Na pengine wewe mwenzangu bado unaendelea kuwa mhanga (victim) wake ibilisi. Kwa uzima wa kweli na kwa usalama wako, rafiki, sasa hiyo iwe basi. Wakati uliokubalika na wa kusaidiwa na Roho Msaidizi ni sasa (2Kor.6:2).
Mungu ameendelea kukuhifadhi mpaka sasa, kwa sababu hapendi mtu yeyote, ikiwa pamoja na wewe hapo, apotee. Kamwe, usiendelee kumkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu Damu ya Kristo Neno la Mungu uliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema. Hakikisha unauingia Umoja wa Nafsi Tatu, sasa hivi. Hakikisha unauingia Umoja wa Nafsi Tatu, sasa hivi. Hakikisha unaingia mbinguni hivi sasa. Kamwe usingoje maji yamwagike ndipo eti wengine wajitahidi kukuzolea. Hayazoleki. Mbinguni unaingia wewe mwenyewe kwa kusaidiwa na Roho wa Kweli sasa hivi. Ndiyo maana ilibidi Kristo Neno la Mungu azaliwe katika Ubinadamu na kuja kwetu. Vinginevyo, angetungojea huko huko. Tuache kukubaliana na shetani anayewafanya watu wamwone Mungu wa Kweli ni mpumbavu katika mpango wake.
Rafiki na ndugu yangu katika Kristo Neno la Mungu, uendelee kubarikiwa kwa Baraka zote za Kiroho katika ulimwengu wa Roho ndani yake Kristo Neno la Mungu (Efe.1:3)
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0787 765 759
0714 118 428
0753 298 707
Chamayombe37@gmail.com

ENDELEZO LA MAENEO NYETI MATANO YAHITAJIYO KUJIFUNZWA KIKAMILIFU ZAIDI

Kati ya yale maeneo nyeti matano ambayo yamebainishwa katika kifungu cha 79 cha ile Barua “Ut Unum Sint”, tumekwisha kulipitia lile neneo linalomhusu Mama yetu Bikira Maria, na lile linahusu mahusiano kati ya Maandiko Matakatifu na Mapokeo Matakatifu. Na katika hali hiyo, sasa tumebakiwa na maeneo matatu ambayo ni:-
(1) Eneo linalohusu Sakramenti ya Ekaristi.
(2) Eneo linalohusu Sakramenti ya Upakwa Mafuta (Ordination), na
(3) Eneo linalohusu Utawala wa Kanisa (Magisterium) ambao unakabiliwa na jukumu na mamlaka ya kufundisha na kuhifadhi Imani.
SAKRAMENTI, ISHARA WAZI
Maeneo mawili ya kwanza kati ya maeneo matatu yaliyobaki yanahusu swala la Sakramenti. Kwa kadiri ya Katekisimu yetu Sakramenti imeelezwa kuwa ni “ISHARA WAZI”.
Kwa maana hiyo, swali linalotukabili sasa ni hili: Je, jambo hili la “Ishara wazi” linaendana na Mungu wetu wa pekee wa kweli ambaye Kristo Neno la Mungu ametufumulia katika Yn.8:26 kuwa ni kweli?
Ili tuweze kuwa katika hali ya kulikabili swali hili ipasavyo, sharti kwanza tujue uhalisia wa huyu Mungu wa pekee wa kweli, na uhalisia wetu sisi watu wake.
Injili ya Kristo Neno la Mungu ambayo imetimilika katika Nyaraka za Mitume, hutuambia kwamba Mungu ni Roho (Yn.4:24) aliye Umoja wa Nafsi Tatu zisizogawanyika 1Yon.5:7 (Biblia Ndogo ya Agano Jipya) na kwamba, kutokana na hali yake hiyo, awatafuta watu wamwabuduo katika Roho na Kweli (Yn.4:23).
Hivyo, kwa kusimamia Yn.8:26 na 1Yn.5:7 Biblia ndogo ya Agano Jipya, Mungu ni “Kweli” aliye Roho katika Umoja wa Nafsi Tatu, Kweli, na Neno, na Roho Mtakatifu.
JE, MTU NI NANI?
Kuhusu mtu, Bibilia hutuambia kwamba mtu ni nafsi kwa mfano na sura yake huyu Mungu aliye Nafsi Tatu (Mw.1:26), na kwamba yeye ni wa kuhuishwa kwa Pumzi (Roho) ya Mungu na kuumbiwa mwili wa nyama kutokana na mavumbi ya ardhi kuwa maskani yake hapa duniani (Mw.2:7).
Hivyo, mtu halisi ni nafsi (utu wa ndani) anayekaa katika mwili wa nyama hapa duniani.
Kwa kushirikishwa kwake Pumzi (Roho) ya Mungu, mtu amejumuishwa katika Umoja wa Nafsi Tatu, kwamba mtu ndani ya Mungu na Mungu ndani ya mtu (1Hoh.4:13); na hivyo kuwa mshirika wa utimilifu wote wa Mungu (Efe.3:19); na hivyo, kushiriki uhalisia ule ule wa Mungu, hapa duniani (1Yoh 4:17).
Hivyo, kiuhalisia, mtu halisi au mtu wa ndani (2Kor.4:16), ni nafsi kama alivyo Muumba wake, ni wa ulimwengu wa Roho, ni wa ulimwengu wa mbinguni (Fil.3:20); yuko nje ya milango ile mitano ya fahamu za kimwili wa nyama, yaani kuona, kusikia, kuonja, kunusa na kuhisi. Hii ni milango ya fahamu katika maisha yetu ya Ulimwengu huu wa mwili wa nyama hapa duniani tunapoishi kama wageni (1Pet.1:17); na siyo katika maisha yetu ya utu halisi, nafsi katika Umoja wa Nafsi Tatu za Mungu Kweli tulikojuishwa kwa kushirikishwa Roho wa Mungu (Yoh.4:13).
Kutokana na ukweli huu, mahusiano na mawasiliano kati yetu na Mungu wetu wa kweli yanapaswa kuwa kwa jinsi alivyo Yeye aliye Roho; wala hayapaswi kuendeshwa kwa akili za kimwili wa nyama (Kol.2:18).
Hivyo, Ndivyo Mungu alivyotuumba tuenende (Efe 2:10). Shetani akaja, katutaperi, akatuua na kuharibu mpango wa Mungu kwa ajili yetu. Kristo Neno la Mungu akaja kutufanya tuwe na uzima tena (Yon 10:10). Mungu akatuhuisha tena, akatufufua na kutuketisha pamoja na Kristo Neno la Mungu katika ulimwengu wa Roho (Kol.2:13-15; Efe 2:5-6).
Hivyo, lile agizo la kututakatwende kwa Roho ni agizo linalotutaka sisi tuliokombolewa na kuokolewa twende kwa kadiri ya uhalisia wa Mungu wetu aliye Roho na anayetafuta watu wamwabudu katika Roho na Kweli kwa kuwa Yeye ni Roho (Yn.4:24).
JE, UTARATIBU WA KWENDA KIROHO UKOJE?
Katika kutufundisha kuhusu swala hili, siku moja Yesu alimwuliza Yule Ofisa, “Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa (Yn.4:48)? Tena, ona alivyomwambia Mtume Toma, “Wewe kwa kuwa umeona, umesadiki. Wa heri wale wasioona wakasadiki (Yn.20:29). Na kinyume cha “heri” ni “Ole”. Kwa kauli hiyo tunaambiwa, “Ole wao wale wanaotaka waone ndipo wasadiki”.
Katika kutimiliza Injili ya Kristo Neno la Mungu, Nyaraka za Mitume kwanza hututafsiria neno imani; kwamba ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo; ni bayana ya mambo yasiyoonekana (Ebr.11:1).
Tunaambiwa katika Ebr.11:6 kwamba pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu; maana yeye amwendeaye Mungu sharti aamini kwamba Yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Katika Ebr.10:38 Mungu anasema, “Mwenye haki wangu ataishi kwa imani; naye akisitasita, Roho yangu haina furaha naye”.
Katika Yak.1:6-8 tunasoma, “Ila na aombe kwa imani pasipo shaka yoyote. Maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku. Na mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. Mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote”.
Tunaambiwa katika 2Kor.5:7; “Twaenenda kwa imani; si kwa kuona”. Na katika Gal.5:4-5 tunaambiwa, “Mmetengwa na Kristo ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria. Mmeanguka na kutoka katika hali ya neema (aliyotustahilia Mungu katika Kristo Neno la Mungu pale Msalabani). Maana sisi kwa Roho tunalizamia tumaini la haki kwa njia ya imani”.
Hivyo, sisi watu, kwa kuwa utu wetu halisi, nafsi, ni wa uhalisia wa Mungu pekee wa Kweli ulio nje ya milango ya fahamu za kimwili wa nyama, mahusiano na mawasiliano na Mungu wetu wa pekee wa kweli ni siri kati ya Mungu na mtu kwa njia ya imani; ni siri kati ya Umoja wa Nafsi Tatu na utu wa ndani, nafsi, iliyo utu halisi ihuishwayo kwa Roho wa Mungu iliyotiwa ndani ya mtu husika.
Kwa mantiki hii, ibada za kisakramenti na kivisakramenti ni ibada zilizo kinyume kabisa cha uhalisia na mapenzi ya Mungu. Tena, kwa kweli, ni ibada adui dhidi ya Mungu wa kweli anayetafuta kuabudiwa katika Roho na kweli. Hizi ni ibada za kumwabudu mungu mwingine na zinazoenendwa na yesu mwingine (2Kor.11:4). Kumwamini au kutomwamini Mungu itakiwavyo, ni swala la kibinafsi. Hakuna kufanyiana. Ndiyo maana ni siri kati ya mtu na Mungu katika kumkaribia Mungu kwa moyo wa kweli na utimilifu wa imani (Ebr.10:22). Izingatiwe kwamba neno “Imani” ni kwa kadiri ya tafsiri ya Ebr.11:1 na si vinginevyo. Si swala la kuamini yaliyotengenezwa na wakubwa fulani (Kol.2:8-10), au yale mtu anayojitengenezea mwenyewe kwa akili zake za kimwili wa nyama au nafsi yake.
ENEO LA UTAWALA WA KANISA
Eneo nyeti la tano lililobainishwa katika kifungu cha 79 cha “”Ut Unum Sint” ni lile eneo linalohusu Utawala wa Kanisa (Magisterium) ambao unakabiliwa na jukumu na mamlaka ya kufundisha na kuhifadhi imani.
Kuhusu eneo hili, hebu tuanze na Yn.6:45, Andiko ambalo hutuambia kwamba watu wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Na Yn.14:26 Yesu hutuambia kwamba Roho Mtakatifu Msaidizi atatufundisha yote na kutukumbusha yote. Tena huyo Roho wa kweli atatuongoza na kututia kwenye kweli yote, (Yn.16:13). Na 1Kor.2:10-12 hutueleza wazi kwamba Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
Ndiyo maana nimesema hili swala la mahusiano na mawasiliano kati ya Mungu na mtu ni siri kati ya Mungu na mtu.
Katika Mt.23:8-10 Kristo Neno la Mungu anaweka yote pamoja, “Bali ninyi msiitwe Rabi, maana Mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu. Wala msimwite mtu baba duniani, maana Baba yenu ni mmoja aliye wa mbinguni (wa uhalisia wa Roho). Wala msiitwe viongozi, maana kiongozi wenu ni mmoja naye ndiye Kristo”.
Kwamba, swala hili la mahusiano kati ya Mungu na mtu ni la kila mtu binafsi limetabiriwa na manabii. Katika Yer.31:33-34 Mungu aliahidi, “Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaandika; nami nitakuwa Mungu wao nao watu wangu. Wala hawatamfundisha mtu na jirani yake, na kila mtu na ndugu yake wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao; hadi aliye mkubwa miongoni mwao maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”.
Na kwa unabii wa Ezekiel Mungu alisema, “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni kutoka kwa uchafu wenu wote, na kutoka kwa vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo npya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu na kuzitenda (Eze.36:25-27).
Utabiri huu ndio ule ulioelezwa ya Yesu mwenyewe kama tulivyoona hapo juu katika Mt.23:8-10, na kutimilizwa kama ulivyoelezwa katika 1Kor.12:13; Gal.3:27 na ule upakwaji mafuta ulioelezwa katika 1Yoh.2:20, 27. Aya hizo za mwisho zatuambia, “Ninyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote. Nanyi mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake”.
Upakwa mafuta na Roho Mtakatifu ulitabiriwa kama ahadi katika nyakati za manabii, sasa katika nyakati timilifu unaelezwa kwamba umetimilika kama tunavyohakikishiwa katika Nyaraka za Mitume zilizo utimilifu wa Injili ya Kristo Neno la Mungu.
MASWALI YA KUJIULIZA NA MAJIBU YAKE
Ndipo tunapokuwa na haki ya kujiuliza:
Je? Maeneo haya ya ishara Wazi na Utawala wa Kanisa kama yalivyo kiuhalisia, hayaendi kwa injili nyingine iliyo tofauti na ile waliyoihubiri Mitume (Gal.1:8-9) na hivyo kuenenda na injili iliyo laaniwa inayotupeleka kwa yesu mwingine na roho nyinginezo mbali na Roho wa Kweli (Kor.11-4)?
MATENDO AU MATUNDA NDIYO DIRA
Tumeamriwa na kuonywa “Wapenzi msiiamini kila roho, bali zipimeni hizo roho, kama zimetokana na Mungu, kwani kuna Roho wa kweli na roho ya upotevu (1Yon.4:1, 6).
Tena tumeagizwa, “Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri. Au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake kuwa mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana. Enyi wazawa wa nyoka, mwawezaje kunena mema mkiwa wabaya? Maana kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya (Mt.12:33-35) Mtawatambua kwa matendo yao (Mt.7:16, 20).
Tumeagizwa, “Basi nasema Nendeni kwa Roho, wala hatazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa maana mwili hutamani kushindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka (Gal.5:16-17).
Matendo ya kwenda kwa mwili yameorodheshwa na Paul Mtume katika Gal.5:19-21 kuwa ni: Uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, husuda, ulevi, ulafi na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawambia mapema kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu wayatendao mambo ya jinsi hiyo, hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tena twaambiwa, “Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili (Kol.2:23).
Twaangalishwa, “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundishao ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo. Maana katika Yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmetimilika katika Yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka (Kol.2:8-10).
Pia, tunatakiwa tupate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, tupate kujua kabisa siri ya Mungu yaani Kristo; ambaye ndani yake Yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika (Kol.2:2-3).
Kiuhalisia katika maeneo haya matatu, kunakosekana kabisa jitihada za kuwasaidia wadau wa kanisa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani Kristo.
Ndipo tunapoambiwa kwamba tunda la kwenda kwa Roho ni lile lilioodheshwa katika Gal.5:22-23; na katika Gal.5:4-5 twasoma, “Mmetengwa na Kristo ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria. Mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Lakini sisi kwa Roho twalitazamia tumaini la haki kwa njia ya Imani”.
MUHTASARI WA MAENEO MATATU YA MWISHO KATI YA YALE MATANO
Baada ya maagizo, maamuru maelekezo maangalisho tuliyoyapewa na Neno la Mungu tunahitimisha ukweli kwamba yale maeneo mawili ya kiishara wazi yako nje ya Kristo na Mungu wa pekee wa kweli anayetaka kuabudiwa katika Roho na kweli.
Na lile eneo la Utawala wa Kanisa nalo liko nje ya Kristo Neno la Mungu kwa sababu kanisa linalohusika na Utawala huu ni kanisa la kimwili na imani inayofundishwa ni ile inayosemekana katika ile sala ya Imani “Mungu wangu nasadiki ninayofunashwa kusadiki na Kanisa Katoliki la Roma; kwani ndiwe uliyefumbulia hayo. Imani hii iko nje kabisa na ile imani iliyotafsiriwa katika Ebr.11:1 na kusisitizwa katika aya nyinginezo nyingi za Biblia.
Hiki kipengele “Ndiwe uliyefundulia hayo….” Hakizingatii ukweli kwamba:-
(1) Yupo yule mwasi na mpingamizi ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho mungu ama cha kuabudiwa, hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu (2Thes.2:4).
(2) Ipo roho ya upotevu (1Yon.4:6) ambayo iko kazini kuwapoteza watu wasiijue kweli wasije wakamwongokea Mungu wa kweli akawaponya (2Kor.4:3-4; Yn.12:40).
Na kutokana na dira tuliyoipewa kupimia roho, hali yakushamiri madhambi hata ndani ya wana makanisa, ni kithibiti tosha kwamba roho ya upotevu ndiyo inayoshikilia makanisa na kupofusha wana makanisa wasichomoke kutoka gereza na minyororo ya utumwa wa dhambi. Mfalme wa Uwezo wa anga, roho Yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi ndiye anayetawala, makanisa.
Hivyo, maeneo matatu yaliyotubakia yako katika uadui dhidi ya Mungu wa pekee wa kweli. Ipo haja ya kujitoa katika hali hii.
MAENEO HAYA MATATU YAKO KINYUME CHA “UT UNUM SINT”
Katika kifungu Na.1 cha Barua yake ya Kichungaji “Ut Unum Sint”, Mt. Papa Yohani Paulo II anatoa hamasa ya kupambana na mwelekeo wa dunia ya kufuta kabisa nguvu za Fumbo la Ukombozi. Katika kifungu hicho, Papa amewataka waamini Kristo kuuishi UKWELI mmoja kuhusu Msalaba, kinyume cha dunia inayokana ukweli kwamba katika Msalaba mtu ana chimbuko la uzima mpya. Dunia hudai kwamba Msalaba hauwezi kumpa mtu maono wala matumaini. Dunia husema kwamba mtu si chochote bali ni kitu cha kiudongo tu kinachopaswa kuishi kana kwamba Mungu hayupo.
Kwa kwenda kimwili wa nyama kama inavyothibitika katika maeneo haya matatu, makanisa yetu siyo tu kwamba yanaelekea, bali kiuhalisia, yanakanusha nguvu ya Fumbo la Ukombozi pale Msalabani. Kiuhalisia, makanisa yetu hayatambui Fumbo la Ukombozi ulio katika Kristo Yesu ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili aoneshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa (Rumi 3:24-25). Makanisa hayatambui kwamba Mungu ametupatanisha sisi na Nafsi yake kwa Kristo pale Msalabani; yaani Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na Nafsi yake asiwahesabie makosa yao. Kwamba Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye (2Kor.5:18-19, 21).
Kwa kutotambua ukweli huu wa wema, huruma, upendo, uwezo na namna za Mungu (Isa.55:8-13) makanisa hujitungia ibada na taratibu zao za kuhusiana na kuwasiliana na Mungu ambazo hazifai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili (Kol.2:23; Gal.5:19-21). Matokeo yake watu hubaki kuwa watumwa wa dhambi. Na Mungu hawasikii wenye dhambi (Yn.9:31). Ndiyo maana kuna kutengwa na Kristo, kuanguka na kutoka katika hali ya neema. Iliyobaki ni kutourithi ufalme wa Mungu (Gal.5:4-5, 21; Ebr.10:26-27, 29). Kwa kutoenenda kwa Roho, makanisa hushiriki 100% ile dhambi ya kupuuza kilichofanyika pale Msalabani.
SASA MCHAWI WETU NI NANI?
Basi niseme nini juu ya hayo? Kifupi, tumtambue mchawi wetu. Naye si mwingine, bali ni shetani. Kumtafuta mchawi mwingine nje ya Shetani ni kupoteza muda na mwelekeo. Tumeambiwa, “Hata hamwezi kufanya mnayotaka (Gal.5:17). Nafsi wewe ni nafsi tegemezi: Au kuungana na Kweli au Ibilisi. Wewe kama wewe, au mimi kama mimi, sote hatuwezi kufanya tunayotaka (Gal.5:17).
Ukihama dini au ukianzisha dini, ibilisi atakukuta huko huko. La kufanya tumekwisha kuambiwa katika 1Kor.7:20 na 24, “Basi ndugu zangu, kila mtu na “akae mbele za Mungu”, pale pale alipo. Hakikisha unakaa mbele za Mungu wa pekee wa kweli hapo hapo ulipo.
Tunaukumbuka usemi wa Papa Yohani Paulo II, Kifungu cha 80 cha “Ut Unum Sint” kwamba wote, kuanzia Maaskofu hadi waamini walei, wamepokea Upako wa Roho Mtakatifu. Tumeona matokeo ya kupokea Upako Mtakatifu ni kuingiwa na Roho Mtakatifu anayekaa ndani ya mtu kumfundisha kweli yote na kumwongoza mtu na kumtia kwenye kweli yote. La kufanya ni moja tu; nalo ni kuhakikisha unakaa mbele za Mungu wa pekee wa kweli, kwa Neno lake yaani Roho wake anayekutamani kiasi cha kuona wivu (Yak.4:5). Yeye atakunong’oneza siri yake yote (1Yon.2:20, 27). Kaa katika Neno lake (Yn.8:31-32). Hicho ndicho chakula kitiacho uzima (Yn.6: 63), tena uzima tele (Yn.10:10).
Amani yake Kristo Neno la Mungu, amani ile aliyoisema katika Yn.14:27, itamalaki ndani yako na kati yetu katika kuukulia ukweli wa Mungu kwa sifa na Utukufu wa huyu Mungu wetu wa pekee wa kweli, na kwa uzima na usalama wetu.
Na ubarikiwe kwa Baraka zote za kiroho katika ulimwengu wa roho ndani yake Kristo Neno la Mungu (Efe.1:3) sasa na hata milele.
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0787 765 759
0714 118 428
0753 298 707
Chamayombe37@gmail.com

MAENEO NYETI YANAYOHITAJI KUJIFUNZWA KWA UKAMILIFU ZAIDI

Katika kifungu cha 79 cha Barua yake ya Kichungaji “Ut Unum Sint” Mt. Papa Yohani Paul II anatubainishia maeneo matano ambayo yanahitaji kujifunzwa kwa ukamilifu zaidi.
Maeneo hayo ni:-
(1) Mahusiano kati ya Maandiko Matakatifu kama Mamlaka ya juu kuliko yote katika maswala ya imani, na Mapokeo Matakatifu kama si ya kupuuzwa na kuwekwa kapuni katika kufafanua Neno la Mungu.
(2) Ekaristi kama Sakramenti ya Mwili na Damu ya Kristo. Toleo la sifa kwa Baba, kumbukumbu la Sadaka na uwepo halisi wa Kristo na Miminiko litakasalo la Roho Mtakatifu.
(3) Upakwa Mafuta (Ordination) kama Sakramenti ya kumtoa mtu kwenye ulei kumwingiza kwenye Ukleri kwa huduma za ibada za kikanisa.
(4) Utawala wa Kikanisa Uliodhaminishwa kwa Papa na Maaskofu walio Umoja naye. Utawala huo waeleweka kama wajibu na mamlaka, itekelezwayo katika Jina la Yesu kwa madhumuni ya kufundisha na kulinda imani.
(5) Na mwisho kuna swala la Mama yetu Bikira Maria, ambalo tumekwisha kulipitia.
SWALA NA.1
Katika kushughulikia Swala Na.1 ni muhimu tujue kwamba Injili ya Kristo Neno la Mungu inamhusu Yeye mwenyewe katika kuja kwake awe Nuru ya Ulimwengu ili kila amwaminie na kumfuata asikae gizani, bali awe na uzima wa milele (Yn.8:12; 12:46). Kwamba amekuja aupe ulimwengu akili kwamba umjue Yeye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele (1Yoh.5:20).
Na Mapokeo Matakatifu, kama inavyosemekana katika vifungu 17 na 78 vya “Ut Unum Sint”, ni mafundisho na/au Mahubiri ya Mitume yanayotufikia kwa njia ya Nyaraka zao.
YESU ALIWAAMBIA NA KUWAFANYIA NINI MITUME?
Katika Lk.10:16, Bwana Yesu aliwaambia Mitume, “Awasikilizaye ninyi, anisikiliza mimi; naye awakataaye ninyi,anikataa mimi; naye anikataaye mimi, amkataa Yeye aliyenituma”.
Tena akasema “Yeye ampokeaye mtu yeyote nimtumaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea Yeye aliyenituma” (Yn.13:20).
Katika Yn.14:15-18, Kristo Neno la Mungu akawaambia Mitume, “Mkinipenda mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, Naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; Ndiye Roho wa Kweli. Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu”.
Akaendelea kusema katika Yn.14:26 “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu ambaye Baba atamtuma kwa Jina langu, atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia”.
Na katika Yn.16:12-14 akawaambia, “Hata bado ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini Yeye atakapokuja, huyo Roho wa Kweli atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa Shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
Kauli hizi zote kwa pamoja zatuhakikishia kwamba mwanadamu kama mwanadamu katika uasili wake hawezi kufahamu kweli ya Mungu.
Ndiyo maana Kristo Neno la Mungu ametukataza tusikubali kuitwa walimu, “Bali ninyi msiitwe Rabi, maana Mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu (Mt.23:8). Na katika Yn.6:45 “Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu”.
KRISTO ATIMIZA AHADI YA KUWAOMBEA MITUME
Katika Yn.17:21-23 tunalisoma ombi: “Wote wawe na umoja, kama vile Baba ulivyo ndani yangu nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, Nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma; ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi”.
AHADI YA KUWAPA ROHO MTAKATIFU YATIMIZWA
Baada ya kukamilishwa kwa tendo la Ukombozi, na kuondolewa dhambi pale Msalabani, siku kadhaa kupita baada ya kufufuka kwake, Yesu akawatokea Mitume wake, akawaambia tena “Amani iwe kwenu; kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu”.
Kwa tendo hilo la kuwapa au kuwashirikisha Roho Mtakatifu, ikawa kwamba Mitume wako ndani ya Mungu na Mungu ndani ya Mitume (1Yoh.4:13). Mitume wakawa wamejumuishwa katika Umoja wa Nafsi Tatu za Mungu, Mitume wakawa Umoja na Mungu. Mitume wakawa wamenyweshwa (1Kor.12:13) na kuvalishwa (Gal.3:27) utimilifu wote wa Mungu (Efe.3:19). Kama vile Mungu wa pekee wa Kweli alivyo, ndivyo walivyokuwa sasa Mitume ulimwenguni humu (1Yoh.4:17). Wakawa tayari wamezaliwa mara ya pili (Yn.3:3) kwa Maji hai ya Roho Mtakatifu (Yn.3:5; Yn.4:10, 14; 7:37-39). Wakawa wameuingia rasmi ulimwengu wa Mungu wa pekee wa kweli, ulimwengu wa mbinguni, ulimwengu wa Roho.
Hapo Mitume wakawa wamebakiwa na kazi moja tu. Nayo ni kuukulia Umungu wa pekee wa Kweli (Pet.2:2) kwa kadiri ya maongozi ya Roho Mtakatifu aliyekuwa ndani ya kila mmoja wao. Hapo kila mmoja wao alikuwa ndani ya Mungu wa Pekee wa Kweli, na Mungu wa Pekee wa Kweli alikuwa ndani ya kila mmoja wao, kwa huyo Roho Mtakatifu aliyekuwa ndani ya kila mmoja wao. Hatima yake ni kwamba kila mmoja wao alikuwa ndani ya kila mmoja wao, kwa huyo Roho Mtakatifu kuwa ndani ya kila mmoja wao.
Na kwa kuwa Umoja wa Nafsi Tatu za Mungu wa Pekee wa Kweli haugawanyiki kwa njia ya huyo Roho, kila mmoja wao alikuwa ndani ya Umoja wa Utatu Mtakatifu na Umoja wa Utatu Mtakatifu ukawa ndani ya kila mmoja wao. Hapo ndipo kila mmoja wao alipopata kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu (Efe.3:19) hapa duniani (1Yoh.4:17).
Na kwa jinsi hii, yale Kristo Neno la Mungu aliyojisomea Mwenyewe kuhusu kutumwa kwake (Lk.4:18); yakawa yametimilika 100% kwa Mitume.
Hivyo, mahusiano kati ya Injili na Mapokeo (Nyaraka za Mitume) ni kwamba ile kazi ya Yesu kuwa Nuru ya Ulimwengu (Yn.8:12; 12:46) na kutupatia akili ya kumjua Mungu wa pekee wa kweli (1Yoh.5:20), imetimilikia katika Mapokeo Matakatifu au Nyaraka za Mitume. Bila Nyaraka za Mitume, Injili ya Kristo Neno la Mungu haijatimilika, ina mapungufu.
MADHARA YA KUPUUZA MAPOKEO MATAKATIFU
Hivyo, kupuuza Nyaraka za Mitume au Mapokeo Matakatifu ni kujiamlia kubaki gizani milele. Tena ni kumpuuza Kristo na Yeye aliyemtuma Kristo (Lk.10:16), ni kumkufuru Roho Mtakatifu aliye Mtendaji Mkuu.
Kupuuza Mapokeo Matakatifu au Nyaraka za Mitume ni janga kuu la kukomeshwa mara moja kwa sifa na Utukufuu wa Mungu wa pekee wa Kweli, na kwa usalama wetu sisi watu wake aliojiumbia mwenyewe ambao Ibilisi ametuteka kwa utaperi.
Wakati umefika wa kuondokana na laana iliyosemekana katika Gal.1:8-9. “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiria ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiria, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, naseka tena, mtu awaye yote akiwahubiria ninyi injili yoyote, isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe”.
Kwa nini ni laana kuhubiri injili nyingine? Injili yoyote isiyo ile waliyoihubiri Mitume, injili yoyote inayogongana na Injili walioihubiri Mitume, ina mapungufu. Hivyo, injili yoyote inayogongana na Mahubiri ya Mitume inapelekea kumhubiri Yesu mwingine na kuoenenda na maroho mengine mbali kabisa na Roho Mtakatifu (2Kor.11:4).
KAULI YA MABABA WA KANISA
Katika kifungu cha 100 cha Barua yake ya kichungaji “UT UNUN SINT” Mt. Papa Yohani Paulo II amerejea Barua yake aliyokuwa amewaandikia Maaskofu, Makleri na Waamini wa Kanisa Katoliki kuonesha njia ya kufuatwa katika kuelekea kwenye Adhimisho la Yubilee Kuu ya Mwaka Mtakatifu 2000.
Katika Barua hiyo walengwa waliambiwa “Maandalizi bora kuliko yote kwa elfu mpya yanaweza kuelezeka kwa ujitoaji uliopyaishwa katika kutumia kiuaminifu kadiri iwezekanavyo Mafundisho ya Vatikani II katika maisha ya kila mtu binafsi na katika Kanisa lote kwa ujumla.
Miongoni mwa Mafundisho ya Vatikani II ni yale ambayo Baba huyu ametuambia katika Barua yake hii hii “UT UNUM SINT” nayo ni: Kuwa waaminifu kwa Injili, Kuiongokea Injili kwa kina, kuwa na fikra mpya, kuwa na mtazamo mpya wa mambo (Kifungu cha 15). Kuiheshimu Kweli kuliko chochote kile kwa kuwa Kweli ni Mungu (Kifungu cha 18).
Na katika kifungu cha 36, Baba anatuambia kwamba katika mchakato wa kutafuta kweli, namna zote za kuelezea imani zetu kamwe zisiwe kizingiti. Ukweli wote ambao Roho Mtakatifu huwaongoza wanafunzi wa Kristo sharti Upokewe wote. Aina zote za ujanjaujanja na makubaliano ya kirahisirahisi (ikiwa ni pamoja na unafiki) lazima yaepukwe kabisa. Maswala nyeti sharti yatafutiwe ufumbuzi, kwani vinginevyo, yatarudi tena wakati mwingine, au kwa namna zile zile, au katika sura tofauti.
Hivyo ndivyo Mababa wa Kanisa Katoliki wanavyotufundisha na kutuelekeza au kutuongoza. Hivyo ndivyo Wachungaji wetu wakuu wanavyotuchunga. Basi, hivyo ndivyo Mahaba na wachungaji wetu walio chini yao wanavyopaswa kutulea na kutuchunga. Vinginevyo ndipo linaposimama lile neno, “Awasikilizaye ninyi, anisikiliza mimi; naye awakataaye ninyi, anikataa mimi, naye anikataaye mimi, amkataa Yeye aliyenituma”.
Kristo Yesu Neno la Mungu ndiye Njia, kweli na Uzima (Yn.14:6). Tena ametuhakikishia kwamba Yeye ndiye Mlango (Yn.10:7, 9) tena ndiye Mchungaji mwema (Yn.10:11, 14). Sasa, yeyote Yule amkataaye Kristo kwa kuwakataa Mitume ameuingiaje huo ubaba au uchungaji, na anamwakilisha Yesu yupi? Je, Siyo Yule Yesu mwingine aliyesemekana katika 2Kor.11:4? Na kama ni hivyo, atabakia aendelee kuwaangamiza watu wa Mungu mpaka lini? Tuwe waaminifu kwa Injili, na kuiongokea Injili kwa kina!
HITIMISHO
Pengine kazi njema anayoifanya Raisi John Magufuli katika kuisafisha Serikali na nchi ya Tanzania ingekuwa mfano mzuri katika kusafisha Makanisa yetu. Na pia katika kutekeleza jambo hili, mfano mwingine ni ule tunaoukuta katika jeshi la Gideoni. Kati ya maaskari 32,000, askari walichujwa hata wakabaki watu 300 (mia tatu tu). Na kwa idadi hiyo ndogo, Mungu akajithibitishia ushindi wa kishindo (Amu.7:1 na kuendelea)..
Walatini walikuwa na msemo wao, “Non numerantur, sed ponerantur” kwamba jambo la maana si idadi (jinsi wanavyohesabiwa, bali thamani (jinsi wanavyothaminiwa). Au kwa Kiswahili, “wingi si hoja”. Ni bora kubaki na wahudumu wachache chini ya Uongozi wa Mungu wa Kweli kuliko kuwa na lukuki la wahudumu walio chini ya Yesu mwingine na maroho mengine. Watambulikana kwa matendo yao (Mt.12:33).
Nuru ya Kristo ambayo ilipangwa iufikie ulimwengu kwa njia ya Mapokeo Matakatifu au Nyaraka za Mitume kamwe isiruhusiwe iendelee kukwamishwa kwa hoja au kisingizio chochote kile. Nyaraka za Mitume ziheshimiwe 100%, kwani Injili ya Kristo Neno la Mungu ndimo ilimotimilikia. Nje ya hapo ni kuenenda kimapungufu na kutumbukia kuzimu kaburi la milele la nafsi zilizo nje ya Umoja wa Nafsi Tatu za Mungu wa Pekee wa Kweli. Kilele cha kuufikia Ukweli wa Mungu ni Nyaraka za Mitume.
Yote yakiwa kwa sifa na utukufu wa Mungu wa pekee wa kweli, na kwa wokovu wa watu wa Mungu wanaodidimizwa gizani au maangamizoni kwa upofushaji unaoendelea wa Yule mwovu ibilisi (2 Kor.4:3-4; Yn.12:40).
Barikiwa Sana!!!
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0787 765 759
0714 118 428
0753 298 707
Chamayombe37@gmail.com

WAKARISMATIKI WAKATOLIKI KUWA WAKARISMATIKI KWELI KWELI NA WAKATOLIKI KWELI KWELI

Kati ya vipengere hivi viwili, “Karismatiki”na “Katoliki”, kipengere “Katoliki” kimekwisha kushughulikiwa katika mada iliyoitwa “KANISA LA KRISTO NENO LA MUNGU”. Hivyo, hapa tutajikita katika kujifunza kipengere “KARISMATIKI”.
Katika mada iliyohusu IMANI tumepitia fundisho la Mitume wa Kristo Neno la Mungu kuhusu ukombozi, upatanisho, ondoleo la dhambi au utakaso kwa njia ya IMANI katika Damu ya Kristo Yesu.
Lakini utakaso si jambo linaloishia hewani. Utakaso ni kuondoa kizingiti au kifarakanishi. Kifarakanishi kinaondolewa ili iweje?
Ebr.10:14 hutuambia, “Lakini kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa, Kumbe matokeo ya kutakaswa ni kukamilishwa. Na aliye kamili ni Mungu. Hivyo , kukamilishwa kunahusika na mtu kushirikishwa Umungu wa pekee wa kweli.
Kunafanyikaje? 1Kor.12:13 hutuambia, “Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu wayahudi au kwamba tu Wagiriki; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja”. Kumbe kubatizwa kwa roho ni kunyweshwa roho mtakatifu. Nikushirikishwa Mungu wa pekee wa kweli.
Na kwa Ubatizo huo wa kunyweshwa Roho Mtakatifu, wote watakuwa wamemvaa Kristo Yesu kuwa watoto wa Mungu wa pekee wa kweli (Gal.3:27, 26). Kwa ubatizo huo wa kunyweshwa Roho Mtakatifu, wahusika huwa ndani ya Mungu, na Mungu ndani ya nafsi husika. Nafsi husika huwa warithi wa Mungu warithio pamoja na Kristo Neno la Mungu (Rum.8:17). Watu au nafsi husika zitakuwa zimetimilika katika utimilifu wote wa Mungu (Efe.3:19; Kol.2:9-10). Kama vile mtoto wa simba alivyo simba, vivyo hivyo, mtoto wa Mungu ni Mungu (1Yoh.4:17).
KUTIMILIKA KWA SHARTI LA KUUONA NA KUUINGIA UFALME WA MUNGU
Kwa ubatizo huo wa kunyweshwa na kuvalishwa Umungu alilolitoa Bwana wetu Kristo Neno la Mungu kwamba mtu asipozaliwa mara ya pili hatauona Ufalme wa Mungu, litakuwa limetimilika (Yn.3:3; 1Pet. 1:23).
MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO (Yn.3:5)
Mtu asipozaliwa kwa maji yapi? Katika mazungumzo kati ya Kristo Yesu na Yule mwanamke Msamaria pale kisimani, Kristo Neno la Mungu alimwambia Yule mwanamke, “Kama ungalijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye nipe maji ninywe, wewe ungalimwomba Yeye Naye angalikupa maji yaliyo hai. Yeye anywae maji haya ataona kiu tena. Bali yeye anywaye maji nitakayompa mimi ataona kiu hata milele. Bali maji hayo yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji yakimbubujikia uzima wa milele” (Yn.4:10, 14).
Na katika Yn.7:37-39 Bwana Yesu Neno la Mungu anatualika, “Mtu akiona kiu na aje kwangu anywe. Aniaminiye Mimi kama vile Maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na Neno hilo alilisema kuhusu Roho ambaye wale waaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa”.
Hivyo maji yanayohusika na ubatizo aliouleta Kristo Neno la Mungu si maji ya kumwagiwa wala kuzamishwa; bali ni maji ya kunyweshwa yakae ndani ya mtu kumbubujikia uzima wa milele, uzima ule ule wa Mungu wa pekee wa kweli.
La kukazia hapa ni kwamba Mkarismatiki kweli kweli ni Yule aliyenyweshwa Roho Mtakatifu. Na kwa tendo hilo mtu huyo yuko ndani ya Kristo Neno la Mungu na Kristo Neno la Mungu yumo ndani ya mtu ahusikaye. Hivyo mtu huwa Roho moja na Kristo Neno la Mungu. Na kwa jinsi hiyo mtu huwa mshiriki wa utimilifu wote wa Mungu. Na hapo aweza kufanya yote aliyofanya Kristo Neno la Mungu; (Yn.14:12) maana Mtendaji ni Roho Yule Yule atendaye ndani ya Kristo aliye ndani ya huyo mtu ahusikaye. Maana atendaye si huyo mtu ahusikaye, bali ni Roho Mtakatifu ambaye yuko ndani ya Kristo aliye ndani ya mtu husika. Na hivyo, kumsifu huyo mtu ni dhambi ya kumwibia Mungu Utukufu wake.
Kamusi ya Kiingereza inatuelezea msukumo wa Kikarismatiki (Charismatic Movement) kwamba ni msukumo wa kimsingi katika Makanisa ya Kikristo ambao hukazia karama au vipawa ambavyo husadikiwa kwamba vinatolewa na Roho Mtakatifu.
Mtazamo huu wa kukazia karama au vipawa hauzingatii ukweli kwamba Yule asi huwa anajiinua juu ya kila kiitwacho Mungu au cha kuabudiwa; huyu ambaye haachi kuingia katika hekalu la Mungu akijionesha nafsi yake kama kwamba yeye ndiye Mungu (2Thes.2:3-4).
Kuhusu ukweli huu, Bwana aliye Kristo Neno la Mungu anatuonya, “Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki; kwa maana watajitokeza makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu wapate kuwadanganya, ikiwezekana, hata hao wateule. Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele” (Mk.13:21-23).
Katika hili mafundisho ya Mitume yanazidi kuweka wazi; hao waliambiwa Roho Mtakatifu atawaongoza awatie katika kweli yote:
1. “Kuja kwa Yule mwasi ni kazi ya shetani, atumiaye uwezo wote, ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli wapate kuokolewa (2Thes.2:9-10).
2. Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama (Ufu.13:13-14).
3. “Hizo ndizo roho za mashetani zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote (Ufu.16:14).
Kuhusu swala hili la ishara na ajabu, Kristo, Neno la Mungu alituonya mbele (Mk.13:23). Je, wakarismatiki tunaonyeka kiasi gani katika hili. Ikiwa watu, baada ya kupokea utakaso kwa njia ya imani katika Damu ya Yesu, hunyweshwa Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu huwa mkazi ndani ya watu kuwabubujikia uzima, (Yn.4:14). Huyo roho ambaye huwa anaitwa “Shuka roho, shuka na moto wako!! N.k. ni roho gani huyo kama siyo Yule aliyeshangawa na Paulo Mtume katika 2Kor.11:4? Je, huko si kumtumikia shetani badala ya Kristo Neno la Mungu?
Tukubali, tusikubali, ukweli unabaki kwamba Karismatiki Katoliki ni tunda la Vatikani II; na Mababa waliofuata waliipokea Karismatiki Katoliki kuwa ni Baraka kwa Kanisa.
Kutokana na ukweli huu, Karismatiki Katoliki inapaswa kuwa ni chombo cha utekelezaji wa fundisho la Vatikani II kama tunavyofikishiwa na Mababa Mtakatifu.
Mababa wanatutaka tuwe waaminifu kwa Injili; tuiongokee Injili kwa kina, kuwa na fikira mpya, kuwa na mtazamo mpya wa mambo, kuiheshimu kweli kuliko chochote kila; na, katika mchakato wa kutafuta kweli, namna zetu za kuelezea imani zetu kamwe zisiwe kizingiti.
Ili kuwa waaminifu kwa Injili au kuongokea Injili kwa kina kunadai utekelezaji wa sharti la kuwa mwanafunzi wa Yesu kweli kweli, nalo ni kukaa katika Neno lake (Yn.8:31-32).
Kujikita katika Uinjilishaji badala ya kujikita katika kujua kweli huishia kujawa na wafanya mazingaumbwe (Conjurers) badala ya wainjilishaji katika Karismatiki Katoliki ambao bila aibu wanajiita, “Wakarismatiki kweli kweli na wakatoliki kweli kweli. Na kwa sababu hiyo, hawatakuwa nje ya wale walioambiwa “Ninyi ni wa baba yenu ibilisi; na tamaa za baba yenu ndizo mpe ndazo kuzitenda; maana yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli. Asemapo uongo asema yaliyo yake mwenyewe; maana yeye ni mwongo na baba wa huo” (Yn.8:44).
NENO LA MUNGU NI UZIMA
1. Kumeshuhudiwa watu watatu kuondokewa na kansa ya ziwa walipojua na kuamini ukweli wa Neno la Mungu kwamba mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu na kuyachukua magonjwa yetu (Mt.8:17). Tangu tarehe 24/12/2005, mhusika mmoja wapo ni hai hadi sasa. Hata wawili waliofuata miaka ya badaye, nao ni hai.
2. Wawili kuondokewa na ukimwi wa shetani kwa kujua na kuamini kushirikishwa kwao utimilifu wote wa Mungu (1Yn.4:13; Efe.3:19; Kol.2:9-11). Badala ya ukimwi wa ibilisi wakapokea Ukimwi wa Yesu, ukamilifu au utimilifu wa kinga mwilini. Wanadunda katika uzima wa Yesu, Neno la Mungu hata sasa.
3. Kuna Mama aliyepokea kutodhurika kwa mwanawe aliyekunywa sumu ya kutibia minyanya kwa hoja kwamba Yesu Neno la Mungu amesema, “Hata mkinywa cha kufisha hakitawadhuru” (Mk.16:17-18).
Yote kwa yote, kweli, ni dawa; tena ni dawa ya uhakika; kwani kweli ni Mungu mwenyewe mwenye kuponya yote (Hek.16:12). Tena Kristo Neno la Mungu, kasha tuombea kwa Baba, “Uwatakase kwa ile Kweli; Neno lako ndiyo kweli. Nami najiweka wakfu mwenyewe ili na hao watakaswe katika Kweli” (Yn.17:17, 19). Je, inawezekana Baba kumkatalia Mwana ombi hili? Mungu hudumu wa kuaminiwa; maana hawezi kujikana mwenyewe (2Tim.2:13). Ukiwa na moyo mgumu kuupokea na kuuamini Ukweli huu ni kwa hasara yako.
Badala ya kujikita kwenye makongamano yanayogharimu muda na mali nyingi; hebu sasa Karismatiki iwe Chuo Kikuu cha Elimu ya mbinguni kwa kujikita katika Neno la Mungu (Yn.8:31-32) ili kukidhi mapenzi ya Mungu anayetaka watu wote waokolewe na kujua ile kweli (1Tim.2:4). Watu wa Mungu wanaangamia kwa kukosa maarifa (Hos.4:6). Tena watu wa Mungu wanapotea kwa kutojua Maandiko wala uwezo wa Mungu, (Mt.22:29). Karismatiki iwe chombo cha kudhihirishia njia ya wokovu.
Mungu akubariki kwa Roho wake wa Kweli wa kukuongoza akutie kwenye kweli yote (Yn.16:13) na kukuwezesha kuukulia Umungu wa pekee wa Kweli hata kumfikia Yeye katika yote (Efe.4.13-15). Yote yakiwa kwa sifa na utukufu wa Mungu wa pekee wa Kweli, kwa usalama wako na wa dunia yote Mungu aliyoiumba kwa ajili yake.
Kujigamba kwamba Umkarismatiki kweli kweli na Mkatoliki kweli bila kunyweshwa na kuvalishwa utimilifu wote wa Mungu ni kuwa mwongo na mtumishi wa Ibilisi; ni KUJILAANI.
Amini kwamba Mungu wa pekee wa kweli, Baba wa Bwana wetu Kristo Neno la Mungu, na Baba yetu, amekubariki kwa sababu ya kuikubali na kuipenda ile Kweli kwani Kweli ni Yeye mwenyewe. Kuikubali na kuipenda Kweli ndipokumkubali na kumpenda Mungu wa pekee, wa Kweli. Achana kabisa na uongo.
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0787 765 759
0714 118 428
0753 298 707
Chamayombe37@gmail.com

IMANI NI NINI, KWA NANI, KATIKA NINI NA MATOKEO NI NINI?

Katika kutafakari swala la imani, hebu tuanze na aya zifuatazo: Gal.5:16-17; Mk.10:27; 9:23 na Mt.17:20.
Gal.5:16-17 hutuambia, “Basi nendeni kwa Roho wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili, maana hizi zimepingana HATA HAMWEZI KUFANYA MNAYOTAKA.
Nafsi ya mwanadamu ambaye ni mfano na sura ya Mungu, aliye Nafsi Tatu, ilipata kuwa nafsi hai baada ya kushirikishwa uzima halisi wa Mungu mwenyewe (Mw.2:7).
Hivyo, mwanadamu kama mwanadamu ni nafsi isiyo na uhai wake mwenyewe. Na hivyo, katika hali hiyo mwanadamu kama mwanadamu hawezi kufanya kitu.
Ndiyo maana, katika Mk.10:27 Bwana Yesu Neno la Mungu, anasema “Kwa binadamu haiwezekani”, kwani hana uhai wake mwenyewe. Ndiyo maana tunaambiwa wazi, “Roho ndiyo itiayo uzima (Yn.6:63).
YOTE YAWEZEKANA KWAKE AAMINIYE [MK.9:23], WALA HALITAKUWAKO NENO LISILO WEZEKANA KWENU [MT.17:20]
Tumekwisha kupata tafsiri ya neno “IMANI” kwamba ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo; ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Au, kwa Kiswahili kinachosemekana kwamba ni cha kisasa, “Imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; ni kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona. Imani ni kuyachukulia tusiyoyaona, kwamba yamekwisha kutimilika 100%.
IMANI KATIKA NINI? AU KUAMINI NINI?
Baada ya kujua maana ya neno imani, swali linalofuata ni “KUAMINI NINI?” Vinginevyo tutabaki hewani, na hapo ibilisi atakuwa amepewa nafasi.
Katika hili, Bwana Yesu anajibu, “Mwaminini Mungu” (Mk.11:22), ambaye kwake yote yawezekana (Mk.10:27) mpate kuuvaa utimilifu wote wa uwezo wa Mungu wa kuhamisha hata milima (Mk.11:23).
KUMWAMINI KRISTO NENO LA MUNGU
Katika Yn.14:1 KRISTO NENO LA MUNGU atuambia, “Mnamwamini Mungu, niaminini na Mimi”. Kristo Neno la Mungu alikwisha kutudhihirishia kwamba Baba yake aliyemtuma ni kweli (Yn.8:26). Jambo hili lilikwisha kushuhudiwa na Yeye ashuhudiaye, Roho Mtakatifu (1 Yoh.5:7) kwamba Mungu ni kweli (Yn.3:33).
Sasa hapa atuambia, “Mnamwamini Mungu aliye kweli; niaminini na Mimi niliye Neno lake. Yn.17:17 anatusisitizia kwamba Mungu aliye kweli na Neno lake ni Umoja, pale alipomwambia Baba, “Uwatakase kwa ile kweli; Neno lako ni kweli.
MANENO YA YESU MWISHONI MWA MAISHA YAKE DUNIANI
Bwana Yesu akawaambia wanafunzi wake “Hata bado ningali ninayo mengi ya kuwaambia lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote…….” (Yn. 16:12-13)
Baada ya kufufuka kwake, pamoja na mengineyo, aliwaambia, “Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawatuma ninyi. Naye akiisha kusema hayo, AKAWAVUVIA, AKAWAAMBIA, POKEENI ROHO MTAKATIFU”. ( Yn.20:21-22)
Hapo ndipo utume wa mitume ulipotimilika. Maana, pamoja na kuwatuma, amewatia Roho Mtakatifu wa kuwaongoza awatie kwenye kweli yote. Na ndiyo maana Paulo ana ujasiri wa kusema “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbiguni atawahubiria ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiria na alaaniwe (Gal.1:8-9). Hata anatushangaa pale tunapowavumilia wale wanaohubiri mayesu wengine na hata kupokea maroho mengine (2Kor.11:4).
Kwa nini Paulo Mtume asema haya yote? Ni kwa sababu wao walimpokea Roho Mtakatifu halisi (Original) kutoka kwa Kristo Neno la Mungu mwenyewe. Roho waliyempokea kutoka kwa Yesu asingeweza kuwa roho ya upotevu.
Wakiwa wanaongozwa na Roho wa Kweli, kwenye kweli yote wanatufundisha yafuatavyo:
(1) Basi nasema nendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili, kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana HATA HAMWEZI KUFANYA MNAYOTAKA (Gal.5:16-17).
(2) Mmetengwa na Kristo ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani (Gal.5:4-5).
(3) “….wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani Kristo; ambaye ndani yake Yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika (Kol.2:2-3).
(4) “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu; kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu wala si kwa jinsi ya Kristo. Maana katika Yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmetimilika katika Yeye aliye kichwa cha kila enzi na mamlaka Kol.2:8-10.
(5) Kwa kuwa katika Yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; na kwa Yeye kuvipatanisha vitu vyote na Nafsi yake akiisha kufanya amani kwa Damu ya Msalaba wake (Kol.1:19-20a).
(6) Watu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika Damu yake. apate kuonesha haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimilifu wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa (Rum.3:23-25).
(7) Kristo akajitoa ili makusudi alitakase na kulisafisha Kanisa lake kwa maji katika Neno…..” Efe.5:26-27
(8) Hivyo, ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye kafara ya suluhu kwa dhambi ya watu wake (Ebr.2:17).
(9) Ndipo aliposema, “Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza kusudi alisimamishe la pili; katika mapenzi hayo, mmepata utakaso kwa kutolewa Mwili wa Yesu (Neno la Mungu) mara moja tu. (Ebr.10:7-10)
Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kulia wa Mungu. Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Ndipo asemapo, “Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi (Ebr.10:11-18).
(10) Katika Ebr.10:19-23 tunaambiwa, “Basi, Ndugu kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa Damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia yaani Mwili wake; na kuwa na Kuhani Mkuu juu ya Nyumba ya Mungu; NA TUKARIBIE WENYE MOYO WA KWELI KWA UTIMILIFU WA IMANI HALI TUMENYUNYIZIWA MIOYO TUACHE DHAMIRI MBAYA, TUMEOSHWA MIILI KWA MAJI SAFI. NA MLISHIKE SANA UNGAMO LA TUMAINI LETU LISIGEUKE; MAANA YEYE ALIYEAHIDI NI MWAMINIFU”.
(11) Wala hawezi kujikana mwenyewe ‘ kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe”. (2Tim.2:13).
Hayo ndiyo wanayotufundisha Mitume wa Yesu Neno la Mungu kuhusu swala la ondoleo la dhambi.
YESU MWENYEWE ANASEMAJE KUHUSU ONDOLEO LA DHAMBI
Katika Mt.20:28 atuambia, “Kama vile mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa Nafsi yake iwe fidia ya wengi”. Na katika Mt.26:28 anaweka wazi zaidi: “Kwa maana hii ndiyo Damu yangu ya agano jipya imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi”.
MATOKEO YA UTAKASO AU ONDOLEO LA DHAMBI
Kwa kadiri ya Ebr.10:14, tokeo la utakaso ni kukamilishwa hata milele. Ukamilishwaji huu upo katika kushirikishwa Roho Mtakatifu (1Yoh.4:13); tendo ambalo hufanyika kwa kunyweshwa Roho mmoja (1Kor.12:13) na kumvaa Kristo Neno la Mungu (Gal.3:27); na hivyo kuwa mwana wa Mungu (Gal.3:26) kuwa kama Mungu mwenyewe alivyo (1Yoh.4:17). Na hivyo, kushiriki tabia ya Uungu (2Pet.1:4) ikiwa ni pamoja na uwezo.
Ili kufikia hilo, siri ya Mungu iko katika Yesu Neno la Mungu, nayo ni kuamini utakaso kwa Damu ya Yesu ambaye ni Roho Mtakatifu ambaye ndani yake mna maji hai (Yn.4:10, 14; 7:37-39); naye huyu Roho yumo ndani ya Neno kama vile Neno alivyo ndani ya Roho na Kweli, katika Utatu wao Mtakatifu.
HITIMISHO
Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Tena imani ni nguvu kuu; kwani yote yawezekana kwake aaminiye, wala hakuna Neno lisilowezekana kwake aaminiye. (Mk.9:23; Mt.17:20)
Lakini nguvu hiyo iko katika kushirikishwa utimilifu wote wa Mungu (Efe.3:19) kwa kunyweshwa Roho Mtakatifu (1Kor.12:13; 1Yoh.4:13), na hivyo kumvaa Kristo Neno la Mungu (Gal.3:27).
Ili kunyweshwa Roho Mtakatifu, kuzaliwa mara ya pili (Yn.3:3, 5), sharti mtu awe amepokea upatanisho na utakaso kwa njia ya imani katika Damu ya Yesu (Rumi.3:25; Kol.1:20; Ebr.10:19-22) iliyomo katika Neno la Mungu (Efe.5:26-27).
Nje ya hayo tunaambiwa “MAANA TUKIFANYA DHAMBI KUSUDI BAADA YA KUUPOKEA UJUZI WA ILE KWELI, HAIBAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI; BALI KUNA KUITAZAMIA HUKUMU YENYE (KWENYE) KUTISHA NA UKALI WA MOTO ULIO TAYARI KUWALA WAO WAPINGAO. MTU ALIYEIDHARAU SHERIA YA MUSA HUFA PASIPO HURUMA KWA NENO LA MASHAHIDI WAWILI AU WATATU. MWAONAJE? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA NI KITU OVYO, NA KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA? (EBR.10:26-29).
Kwa maana asema, “Kwa wakati uliokubalika nilikusikia. Na katika siku ya wokovu nilikusaidia, tazama, wakati uliokubalika ndio sasa, tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa (2Kor.6:2).
Chakuzingatiwa kwa makini ni ukweli huu kwamba kumwamini Mungu kama Mungu hakuna thawabu yoyote. Tendo hilo hata mashetani hulifanya; tena kwa kutetemeka.( Yak.2:19).
Bali tunalotakiwa sisi ni kulitambua na kuliamini lile tendo timilifu la kutohesabiwa makosa ( Rumi.8:33-34, 2Kor.5:19) na kutakaswa kwa maji safi yaliyomo katika damu ya Kristo Neno la Mungu ambaye ni Roho Mtakatifu ( Efe 5:25-27, Ebr.10:19-22, Yoh.7:37-39)
Katika yote, siachi kumshukuru Mungu wa pekee wa kweli kwa udhihirisho wake kwenye Mtaguso wa Vatikani II na katika Mababa (Mapapa) Mtakatifu waliofuata katika utayari wao kutekeleza kusudio lake la kuumba upya dunia yake inayoharibiwa na Yule mwovu.
Kwa namna ya pekee nazingatia zile kauli za ule Waraka wa Kichungaji “UT UNUM SINT” ulioandikwa na Mt. Papa Yohani Paulo II ambao kwao ametutaka tuwe waaminifu kwa Injili, kuiongokea Injili kwa kina, kuwa na fikra mpya na matazamo mpya wa mambo (Kifungu Na.15). Katika Waraka huo pia Baba ametuhimiza kuiheshimu Kweli zaidi ya chochote kile, kwa hoja kwamba Kweli ni Mungu (Kifungu 18) na kwamba kwa hoja hiyo hiyo, namna zetu za kuielezea imani yetu zisiwe kuzuizi katika mchakato wetu wa kutafuta Kweli (Kifungu Na:36).
Na tubarikiwe sote sawasawa na Efe.1:3.
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0787 765 759
0714 118 428
0753 298 707
Chamayombe37@gmail.com

KANISA LA YESU [NENO LA MUNGU

1. Kanisa la Yesu ni moja Takatifu, Katoliki na la kimitume. Kwamba Kanisa la Yesu ni moja ni kwa sababu, kwa njia ya Kristo, pamoja naye na ndani yake, kila mdau wa Kanisa la Yesu yuko ndani ya kila Nafsi ya umoja wa Nafsi Tatu za Mungu; na kila Nafsi ya Utatu Mtakatifu yuko ndani ya kila mdau wa Kanisa la Yesu. Na kwa utaratibu huo ni kwamba kila mdau wa Kanisa la Yesu yuko ndani ya kila mdau wa Kanisa la Yesu (Yn.17:21-23). Kwa jinsi hii wadau wa Kanisa la Yesu, kwa pamoja huwa maskani moja ya Mungu pekee wa kweli katika Roho (Efe.2:18-22)
2. Kanisa la Yesu ni Takatifu kwa sababu hutakaswa sawasawa na maombezi ya Yesu (Yn.17:17, 19), na kwa Neno la Mungu kweli (Efe.5:25-27); Ebr.10:1923). Na kwa utakaso huo hukamilishwa katika Umungu huo kwa kunyweshwa Roho wa kweli (1Kor.12:13). Na hivyo kumvaa Kristo kushiriki utimilifu wa Mungu. Katika hali hiyo, hatendi tena dhambi (Yoh.3:6, 9; 5:18).
3. Kanisa la Yesu ni Katoliki. Neno Katoliki” maana yake halina mipaka (Universal).
Sasa Kanisa la Yesu ni Katoliki kwa sababu kwanza Yesu alionja mauti kwa ajili ya kila mtu (Ebr.2:9); ili kujikusanyia watu wake waliotawanyika wawe wamoja tena (Yn.11:52), chini ya Mchungaji Mmoja (Yn.10:16); kuwanywesha Roho mmoja ili wawe mwili mmoja (1Kor.12:13); na hivyo kumvaa Yesu bila ubaguzi wowote (Gal.3:27). Ili kuwa Roho moja na Yesu (1Kor.6:17) na hivyo kuwa mdau wa Kanisa na Yesu (Gal.3:29; Rum.8:9) popote pale walipo.
4. KANISA LA YESU ni LA KIMITUME
Kwa kadiri ya Yn..11:52, Kanisa la Yesu ni kusanyiko la watoto wa Mungu waliotawanyika ili wawe wamoja tena. Mitume walikuwa wa kwanza kuchaguliwa wawe Kanisa moja la Yesu. Kwa muda wa miaka mitatu wakaandaliwa jinsi ya kuwa wadau wa Kanisa la Yesu.
Ili kuwa mdau wa Kanisa la Yesu sharti mtu awe Roho moja na Yesu (1Kor.6:17) kwa kunyweshwa Roho wa kweli (1Kor.1Kor.12:23) ili hivi kwamba mtu kuwa ndani ya Mungu na Mungu ndani ya mtu, kuwa umoja na Mungu (1Yn.4:13). Hivyo ndivyo mtu huwa wa Yesu kweli (Gal.3:29; Rumi 8:9).
Katika hali hiyo mtu amekuwa amezaliwa mara ya pili katika Umungu pekee wa kweli (Yn.3:3, 5; Gal.3:26). Ili hili lipate kutendeka, sharti mtu apokee, ile neema au zawadi ya upatanisho kwa njia ya imani katika Damu ya Yesu; (Rumi 3:24—26; Ebr.10:19-23). Kwani haitawezekana Mungu kurudi ndani ya mtu kabla ya Upatanisho.
Kwa kupokea upatanisho kwa njia ya imani katika Damu ya Yesu, Mungu Baba huziachilia katika ustahimili wake dhambi zote zilizotangulia kufanywa (Rum.3:25); na kumhesabia mtu husika haki katika Kristo Yesu (2Kor.5:21).
Pamoja na Yesu kuwafundisha mitume wake mengi kuhusu Ufalme wa mbinguni, lakini katika Yn.16:12-15. Bwana Yesu awaambia mitume wake “Hata bado ningali ninayo mengi ya kuwaambia lakini, hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote ….”. Kujua mambo ya Mungu, sharti mtu awe na Roho wa Mungu. Na Roho wa Mungu hupatikana baada ya Yesu kutukuzwa (Yn.7:39)
Hii inatukumbusha kile Yesu alichokisema kuhusu mito ya maji yaliyo hai ambayo hutoka ndani yake yeye aaminiye. Wakati huo Roho huyo alikuwa hajaja kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa (Yn.7:37-39).
Hii inamaanisha kwamba lile swala kuu la jinsi ya ujio wa Roho wa kweli na jinsi ya uendeshaji wa Kanisa lake na mengineyo mengi, Yesu hakuwaambia Mitume wake kwa sababu ni maswala yanayotendwa na Roho wa kweli mwenyewe akiwa ndani yake mtu husika; kama anavyo-tuambia katika 1Kor.2:12, “Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu: (Soma 1Kor.2:10-16).
Mitume walimpokea Roho wa kweli pale walipovuviwa na Yesu na kuambiwa pokeeni Roho Mtakatifu (Yn.20:22). Tangu hapo Bwana Yesu kwa huyo Roho wake wa kweli akakamilisha ngwe nzito iliyobaki ambayo sisi sasa twaipata katika nyaraka zao hawa mitume, huyo Roho wa kweli na jinsi ya kumpata.
Kwa sababu hiyo, kupuuza Nyaraka za Mitume ni janga kubwa mno ambalo mtu huweza kujiingiza kwa hasara yake mwenyewe na hata wale anaowaongoza, ikiwa mtu huyo ni Kiongozi. Kweli yote kuhusu elimu ya ufalme wa mbinguni hupatikana katika Nyaraka za Mitume. Kuhubiri habari za Yesu nje ya mahubiri ya Mitume ni laana (Gal.1:8-9) kwa sababu hayo yatakuwa ni mahubiri yalio nje ya kweli yote. Yn.16:12-13) aliyotuletea Bwana Yesu.
Kwa kufanya dhambi ya kuwapuuza Mitume wa Yesu, badala ya kuhubiri taratibu za kuondokana na utumwa wa dhambi, Makanisa huishia kuhubiri mungu pesa kwa masilahi ya wahusika. Badala ya kumhubiri Mungu wa Mbinguni, makanisa humhubiri mungu wa kuzimu kwa maangamizi ya wahubiri na wahubiriwa, wenyewe bila kujua. Ni HATARI!
5. KANISA LA YESU NI LA ULIMWENGU WA MBINGUNI
Pamoja na sifa nne hapo juu, kutokana na ile simulizi ya Tajiri na Lazaro (Lk.16:19-31), na kujifunua kwa Bwana Yesu, Neno la Mungu, kwamba Yesu ni wa juu, si wa Ulimwengu huu (Yn.8:23) tunajifunza kwamba mtu hukabiliwa na aina mbili za ulimwengu; yaani ulimwengu wa Mungu wa mbinguni na ulimwengu wa kuzimu, kule yule mwasi alikoshushwa kutokana na dhambi yake ya kujikweza (Isa 14:13-15).
Katika kutuombea kwa Baba, Bwana Yesu alimwambia Baba “Neno lako nimewapa na ulimwengu umewachukia kwa sababu wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe ulimwenguni; bali uwalinde na Yule mwovu; maana wao si wa ulimwengu kama mimi nivyo wa ulimwengu (Yn.17:14-16). Tena asema, Baba hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo (Yn.17:24).
Tena tunasoma, Akatufufua pamoja naye, akatukatisha pamoja naye katika ulimwengu wa Roho katika Kristo Yesu (Efe.2:6). Ni akina nani hao? Hao ndio Kanisa la Yesu aliojitakasia kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na dosari wala kunyanzi, wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa (Efe.5:25-27).
Kwa njia ya Yesu Kristo, wadau wa Kanisa la Yesu hupata njia ya kumkaribia Baba katika kunyweshwa Roho mmoja(Efe.2:18; 1Kor.12:13). Na katika Kristo Yesu wadau wa Kanisa lake wamejengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho (Efe.2:22).
Kwa mantiki hii wadau wa Kanisa la Yesu wanapaswa kwenda kwa Roho (Gal.5:16-17). Kwa kadiri ya Kol.3:1-3) wanapaswa kutafuta yaliyo juu Kristo aliko; Kwani Uhai wao umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu (Kol.3:1-3). Uenyeji wao uko mbinguni (Fil.3:20). Katika umoja wa nafsi Tatu, kweli na Neno na Roho wa Kweli (1 Yon.5:7 au 8). Wao ni washirika wa tabia ya Mungu wa mbinguni (2 Pet.1:3-4). Hapa duniani wadau wa Kanisala Yesu wao ni wageni (1Pet.1:17). Hawapaswi kuipenda dunia (1Yoh.2:15-17). Nao hutambulikana kwa tunda la Roho (Gal.5:22-23).
Kwa kuwa Kanisa la Yesu liko katika ulimwengu wa Mungu aliye Roho, Kanisa hili liko nje ya ile milango 5 ya fahamu za mwili wa nyama; macho, masikio, pua, ulimi na ngozi. Kanisa la Yesu huenda katika Roho na Kweli kwa njia ya imani; kwa maana halisi ya neno hili IMANI, yaani kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana (Eb.11:1).
Kama tulivyoagizwa katika Gal.5:16-17 kwenda kwa Roho sifa hii ya Kanisa la Yesu inahusu pia zile sifa nne za kwanza za Kanisa la Yesu, kwamba Kanisa la Yesu ni moja Takatifu, Katoliki na la kimitume. Sifa zote zinapata hadhi katika Mungu pekee wa Kweli ambaye ni Umoja wa Nafsi Tatu, Kweli na Neno na Roho wa Kweli (1Yoh.507) 8).
Mungu aliye Roho (Yn.4:24), mwenye Nafsi Tatu, Kweli na Neno na Roho wa Kweli, amejiumbia mtu wake kwa mfano na sura yake mwenyewe (Mw.1:26) na kumshirikisha uzima = Roho wake (Mw.2:7) ili kukidhi mapenzi yake ya kuabudiwa katika Roho na Kweli (Yn.4:23).
Na hilo ndilo Kanisa lake la Ulimwengu wa Mbingun, ambalo ingawa lipo katika ulimwengu huu, lakini halienendi kwa kuangalia vinavyoonekana (2Kor.4:18). Ni Kanisa linaokwenda kwa imani, si kwa kuona (2Kor.5:7). Na Mungu mwenyewe anasema, “Mwenye haki wangu ataishi kwa imani, naye akisitasita, Roho yangu haina furaha naye (Ebr.10:28). Kanisa la Yesu ni la ulimwengu wa mbinguni, ulimwengu wa ROHO.
6. HITIMISHO
Basi kutokana na hayo, mimi binafsi naamini kwamba ule Waraka wa Kichungaji wa Papa Yohani Paulo II, “The Call for Christian Unity (ut unum sint) chini ya uongozi wa Vatikani II, ni uamsho wa kutuamsha sisi sote tuamke na kuondokana kabisa na huu usingizi wa mauti ya milele unaotukabili.
Waraka hututaka kuwa waaminifu kwa Injili. Pamoja na mengineyo mengi tunayoagizwa na Injili, Injili hututaka kwenda kwa Roho wala hatutazitimiza tamaa za mwili ambazo zimeorodheshwa katika Gal.5:19-21, na ambazo wazitendao hawataurithi ufalme wa Mungu.
Kwamba dhambi au maasi hushamiri duniani, kama ilivyoshuhudiwa kwenye Kongamano la Miaka 35 ya Karismatiki Katoliki kule Dodoma, ni kidhibiti tosha kwamba dunia na dini zake huendeshwa kimwili badala ya kwenda kwa Roho kama tulivyoagizwa na Injili. Dunia na dini zake zinaiasi Injili.
Tena, kwa mujibu wa mada ya kuzipima roho; ni dhahiri kwamba Roho wa Kweli amepotezwa. Dunia na dini zake huenenda na roho ya upotevu inayowafanya watu wa Mungu wampoteze Mungu wao wa kweli. Huenenda na Roho ya upotevu inayowafanya watu wa Mungu wampoteze Yesu, Neno la Mungu kweli, na kuenenda na mayesu wengine wa kuzimu.
Sasa wakati umefika wa kudhamiria kwa dhati ya 100% kwenda kwa Roho kama tulivyoagizwa na Injili ya Mitume (Gal.5:16-17; 1:8-9).
Wakati wa kutimilika kwa mapenzi ya Mungu (1Tim.2:4) kwamba watu wote waokolewe (Kol.1:13) na kupata kujua yaliyo kweli (Yn.17:3) sasa umefika.
Wakati umefika sasa wa kuachana kabisa na fikira za kidini ambazo huwapelekesha watu wa Mungu kwa makristo wa uongo (Mk.13:21-22); fikira za kidini ambazo huwapelekesha watu wa Mungu waenende na mayesu wengine au roho nyingine ambazo huwapelekesha watu wa Mungu mbali kabisa na Yesu, Neno la Mungu Kweli (2Kor.11:4; Yn.8:26; 3:33).
Wakati umefika sasa wa kumwambia Yule mungu wa ulimwengu wa kimwili ambaye ni mwuaji, mwongo na baba wa uongo, wakati umefika sisi dunia tumwambie kwa ujasiri 100% maadamu tuna Roho wa Kweli, tumwambie, Umetuonea kwa kutugharagaza katika maasi na maovu yako kiasi cha kutosha. Sasa tunasema BASI!!!” Tumwambie kwa ujasiri yeye na wafuasi wake, wakome na wabaki peke yao huko kuzimu, pande za mwisho za shimo walikoshushwa (Isa.141:15).
Wakati uliokubalika ndio sasa; na siku ya wokovu ambayo Mungu Kweli huwatakia watu wake ndio sasa; na ndio sasa ambapo ataka watu wake kujua Kweli.
Ndugu yangu nikupendaye kwa upendo wa Kristo, fahamu kwamba Nuru ya Yesu imeng’aa gizani wala giza haikuweza (Yn.1:5). Jipe moyo, Yesu ametushindia (Yn.16:33). Na ubarikiwe kwa Baraka zote za kiroho katika Ulimwengu wa Roho ndani yake Kristo, Neno la Mungu Kweli (Efe.1:3), sasa hata na milele!!.....
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0714 118 428
0787 765 759
0753 298 707
Email: chamayombe37@gmail.com

BIKIRA MARIA MAMA WA MKOMBOZI NA MAMA YETU MZAZI

Miongoni mwa maswala nyeti ambayo Papa Yohani Paulo II aliagiza yajifunzwe kwa upya ni swala la Mama yetu Bikira Maria (The Call for Christian Unity (Kifungu cha 79).
Katika uhalisia wa mambo ni kwamba ubinadamu unakabiliwa na tatizo la utumwa wa dhambi unaotokana na dhambi ambayo imepelekea ulimwengu huu kuwa chini ya miliki ya Yule mwovu.
MPANGO WA UKOMBOZI
Mshahara wa dhambi ni mauti (Rumi 6:23). Watu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Rumi 3:23). Hivyo, kiuhalisia watu wote wamekufa, ni maiti.
Ili kurejesha uzima, ilibidi Yeye mwenyewe arudi ndani ya mtu wake aliyejifarakanisha kwa kumwamini Yule mwovu. Na haiwezekani arudi ndani ya mtu wake hali dhambi ingalimo ndani yake.
Katika hali yake ya umauti, na kutokana na hali ya dhambi kuwa ukuta au kiambaza kati yake Mungu na mtu wake, mtu hawezi kufanya lolote lile kujikwamua kutoka utumwa wa dhambi.
Ndipo Yeye mwenyewe akamua kushiriki ubinadamu, ili Yeye mwenyewe katika hali ya kibinadamu amharibu shetani (Ebr.2:11-17), kuifuta na kuiondoa dhambi isiwepo tena; na hivyo kufuta enzi na mamlaka ya shetani (Kol.2:13-15).
Kukamilisha kusudio hili la kushiriki hali ya kibinadamu, akamteua Bikira Maria, ambaye amekubali na kubarikiwa kwa utakaso na kuingiwa na Roho Mtakatifu. Na kadiri ya 1Yoh.4:13, kwa huko kushirikishwa Roho Mtakatifu, Bikira Maria akawa ndani ya Mungu na Mungu ndani ya Bikira Maria, akawa umoja na Mungu katika Utatu wake Mtakatifu, tayari kutimiza kazi ya ukombozi kama ilivyokusudiwa.
Hivyo katika kutimiza kazi ya ukombozi Bikira Maria hayuko nje ya Mungu katika Utatu wake Mtakatifu.
BIKIRA MARIA MAMA MZAZI WA WAZALIWA MARA YA PILI
Bikira Maria ni Mama wa Yesu ambaye ni Neno la Mungu aliyefanyika Mwili (Yn.1:14).Tumboni mwa Bikira Maria.
Wale ambao kiuhalisia wanaambiwa “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili kwa mbegu isiyoharibika, kwa Neno la Mungu lenye uzima lidumulo hata milele (1Pet.1:23); hao ndio wale wanaosemekana katika Ebr.2:11, “Maana Yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja; kwa ajili hii Yesu haoni haya kuwaita ndugu zake.
Atakasaye ni Neno aliyefanyika Mwili. Wanaotakaswa ni hao waliozaliwa mara ya pili kwa Neno la Mungu lidumulo hata milele. Wote wamezaliwa na Neno la Mungu. Neno la Mungu ndiyo mbegu ya kiume iliyowazaa. Ni ndugu, ni makaka “Brothers)” siyo “Half-Brothers”).
Maadamu sisi nasi tumezaliwa kwa Neno la Mungu, Yesu Neno la Mungu aliyefanyika Mwili tumboni mwa Bikira Maria, sisi tuliyezaliwa kwa Neno la Mungu nasi tulikuwa naye tumboni mwa Bikira Maria. Alipomzaa Yesu katuzaa pamoja na Yesu.
Hivyo, kiuhalisia, Bikira Maria ni Mama yetu mzazi wala si mama wa Kambo.
BIKIRA MARIA WA MLIMA KARMERI NA BIKIRA MARIA WA FATIMA
Je, Bikira Maria anayehusika na matumizi ya Skapulari iliyoandikwa, “Whoever dies wearing this Scapular will never suffer eternal hell” na Bikira Maria wa Fatima aliyetuhimiza kusali rosari, ni Bikira Maria wa kweli?
Tumeagizwa kuzipima roho, maana kuna Roho wa kweli na roho ya upotevu (1Yoh.4:1, 6). Bikira Maria wa kweli kamzaa Yesu wa kuwaokoa watu wake kutoka utumwa wa dhambi (Mt.1:21). Sasa Bikira Maria anayehimiza taratibu ambazo hazisaidii kitu kuokoa watu kutoka utumwa wa dhambi, huyo anaweza kuwa Bikira Maria wa kweli? Je, huyo atakuwa nje ya Yule mwasi ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho mungu au cha kuabudiwa? Yule ambaye huketi hata katika hekalu la Mungu, akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu? (2thes.2:4)
Kwenye Mabanda ya Huduma ya Kufunguliwa, wanapelekwa watu wenye mapepo ambao wamevaa rosari na Skapulari. Kama vitu hivi vina nguvu ya Mungu pekee wa kweli, mapepo yanaishije na watu waliovaa vitu hivi? Na kama yanaweza kuishi nao wanovaa vitu hivi, yatashindwaje kuwasindikiza kuzimu mwishoni mwa maisha yao hapa duniani?
Ikiwa ibada wanazoenenda nazo (kuungama, kuhudhuria Misa, kukomunika, kutoa zaka na sadaka) hazifai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili (Kol.2:23; Gal.5:19-21), yaani, hazifai kitu kulikabili tatizo la utumwa wa dhambi. Ibada hizo anapofanyiwa akiisha kufa zitapata wapi nguvu ya kuweza kutatua tatizo la dhambi?
Hivi, ibada hizi haziishii kuwa mchezo wa kuigiza tu? Nakubaliana na agizo la Papa Yohani Paulo II kwamba tuwe waaminifu kwa Injili tuwe na fikira mpya, mtazamo mpya wa mambo na wongofu wa kina.
Kwa usalama wetu tuzingatie agizo hili ambalo linatokana na Mtaguso wa Vatikani II. Mungu anataka watu wote waokolewe na kupata kujua iliyo kweli (1Tim 2:4). Maana watu wake wanapotea kwa kuwa hawajui Maandiko wala uwezo wa Mungu (Mt.22:29). Na njia ya kujua kweli ni kukaa katika Neno lake; ndipo tutakapo kuwa wanafunzi wake Yesu kiukweli, na kujua kweli itakayotuweka huru (Yn.8:31-32).
Ibada hizo kwa Bikira Mria ni ibada zilizo laaniwa kwa sababu
• Ziki nje kabisa ya injili iliyohubiriwa na mitume wa Kristo Neno la MUNGU.
• Zinawapambanisha Kristo Neno la Mungu mbaye, kwa kadiri ya mapango wa MUNGU, ndiye Mwombezi( Rum.8:26-27,34; ebr.2:17; 7:25; 1Yoh.2:1-2).
• Kadiri ya 1Yoh.4:13, Bikira Maria ni mshiriki wa umoja wa nafsi tatu za MUNGU. Hivyo ,fikra za kumchomoa Bikira Maria awe nje ya utatu mtakatifu wa Mungu ni fikra farakanishi amabazo ni za yule mwovu. Hatupaswi kuafikiana naye.
Ni ujumbe kutoka kwa nduguyo katika Neno la Mungu, la Mungu aliyefanyika Mwili kututoa kwenye utumwa wa dhambi. Tumshukuru kwa Roho Mtakatifu.
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0714 118 428
0787 765 759
0753 298 707
Email: chamayombe37@gmail.com

YESU, NENO LA MUNGU, MPATANISHI NA KAFARA YA UPATANISHO KWA DHAMBI ZA WATU

Tunasoma katika Rum.3:23-26 kwamba wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; kwamba wanahesabiwa haki bure kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika DAMU yake, ili aoneshe haki yake kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; apate kuonesha haki yake wakati huu; ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminiye Yesu.
Mshahara wa dhambi ni mauti (Rum.6:23); Mungu wa pekee wa kweli, kwa wema na upendo wake mkuu anaowapenda watu wake upeo (Yn.13:1) kwa upendo wa milele (Yer.31:3), na kwa uvumilivu wake usiopimika, akaazimia kufanya mpango wa kumrudisha mtu wake na kumfufua au kumhuisha kwa upya.
Ili hili lipate kutimilika, sharti kile kifarakanishi kilichomfanya aachane na mtu wake, dhambi, kiondolewe kwanza, kisiwepo “tena” ndani ya mpendwa wake.
Lakini dhambi ni mlima mkubwa mno kuweza kushughulikiwa na mtu au kiumbe chochote duniani, hata mbinguni. Zaidi ya hilo, ni kwamba katika hali ya dhambi, kiuhalisia, utu wa ndani, utu halisi, yaani nafsi imekufa, ni marehemu, kutokana na ukweli kwamba mshahara wa dhambi ni mauti. (Rum.6:23). Na maiti haiwezi kufanya lolote kujikwamua katika umauti wake, wala kumsaidia mwingine.
Ndipo Mungu mwenyewe, katika kujikombolea mtu wake, akaamua kuwa ndani ya Mungu Mwana, Neno, kuwapatanisha wanadamu na Nafsi yake mwenyewe asiwahesabie makosa yao (2 Kor.5:19); bali kwamba wawe wenye haki (watakatifu) wake katika Kristo Mwanawe wa pekee (2Kor.5:21).
Kwamba kwa upatanisho ambao huhitimishwa kwa njia ya imani katika nguvu za Damu ya Yesu aliyefanywa kuwa dhambi, Mungu katika ustahimili wake, huziachilia, yaani huzifuta dhambi zilizotangulia kufanywa (Rum.3:25), na wala hazikumbuki tena kabisa (Ebr.10:17). Na ndipo Mungu kwa amani tele humnywesha (Kor.12:13) na kumvalisha utimilifu wote wa Mungu (Gal.3:27) ili mtu awe mwana wa Mungu (Gal.3:26).
Hapo ndipo mtu anapokuwa ametimilika kwa utimilifu wote wa Mungu (Effe.3:19).katika Kristo Yesu aliye kichwa cha kila enzi na mamlaka (Kol.2:9-10). Hapo mambo huwa kama Mungu alivyo, ndivyo mtu naye anavyokuwa hapa duniani (1Yon.4:17).
KUPATANISHWA NA MUNGU YUPI? KUHUSU NINI?
Tatizo linalotukabili binadamu ambalo ibilisi amewafunga na kuwagharagaza binadamu ni utumwa wa dhambi (Yn.8:34). Na ndilo hilo Yesu ametumwa kuja kulishughulikia atutoe tuwe huru (Mt.1:20-21).
Mungu mwenyewe, katika Umoja wake wa Utatu Mtakatifu, amelishughulikia swala la upatanisho kiutimilifu. Ona alivyolianza katika ile Sala yake Kuu kama tunavyosoma katika Yn.17. Kisha tuone Mungu anavyoitenda katika Nyaraka za Mitume. Hebu soma Rum.8:26-27, 34; 2Kor.5:19; Ebr.7:25; 1Yn.2:1-2.
Nje ya hapo ni uzushi mtupu kama tunavyoambiwa katika Kol.2:23, na matunda yake kama tunavyodhihirishiwa katika Gal.5:19-21.
Mt.12:33-35 hutuagiza: “Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake kuwa mabaya. Maana kwa matunda yake mti hutambulikana. Enyi watoto wa nyoka mwawezaje kunena mema mkiwa wabaya? Maana kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. Mtu mwema katika akiba njema, hutoa yaliyo mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya”.
Na katika Gal.5:16-18 twasoma, “Basi nasema, Nendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani kushindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria”.
Sasa sisi, kwenye dini zetu, hata amri za Mungu hazitutoshi. Tunajiongezea na lukuki lwa sheria nyinginezo nyingi tu.
Swala lililopo ni, Je, tutaanza lini kuwa waaminifu kwa Injili kama tulivyoagizwa na Papa Yohani Paulo II? Je, tutaacha lini kujikabidhisha kwa mungu wa dunia hii ambaye hupofusha fikira zao wasioamini isiwazukie nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu (2 Kor.4:3-4); na ambaye huwapelekesha watu wa Mungu kwa makristo wengine na maroho, mengine mengine tu? Na hata pengine kujiinua katika Jina la Mzazi wetu Bikira Maria?
Tutaachana lini na ile roho ya upotevu ambayo hupofusha macho na kufanya mioyo mizito watu wasije wakaona kwa macho yao na kufahamu kwa mioyo yao wakamongokea Kristo wa kweli akawaponya (Yn.12:40)?.
Je watu wa Mungu waendelee kuangamizwa hivi mpaka lini? Mpaka lini kazi ya Mwana wa Mungu aliyoifanya pale Msalabani itaendelea kupuuziwa? Je, mpaka lini tutaendelea kumdhihaki Mungu kwa kusali sala ya “Baba yetu…..” tukimwambia “Ufalme wako ufike, utakalo lifanyike….” pindi tunakuwa vizingiti au vikwazo kwa Ufalme wa Mungu na mapenzi ya Mungu ambaye hutaka watu wote waokolewe na kupata kujua yaliyo kweli? Je, kusali sala ile kuko mbali na unafiki:? Unafiki huu utaisha lini hata tumkaribie Mungu wetu wenye moyo wa kweli kwa utimilifu wa imani (Ebr.10:22).
Tumemdhihaki Mungu wetu wa pekee wa kweli Umoja wa Nafsi Tatu Kweli na Neno na Roho wa Kweli kiasi cha kutosha, kwa kulipuuza lile agizo la kwenda kwa Roho (Gal.5:16) na la kuufanya mti kuwa mzuri. Sasa tuseme BASI!!! Twendeni kwa Roho na kuufanya mti kuwa mzuri, badala ya kung’ang’ana na yaliyopitwa na wakati.
TWENDE KWA ROHO
Tumeona kwamba Gal.5:16 yatutaka twende kwa Roho ndipo hatutazitimiza kamwe tamaa za mwili. Na Kol.2:8 yatuangalisha tusije tukafanywa mateka kwa elimu ya bure na madanganyo matupu; kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
Injili yatutaka kwenda kwa jinsi ya Kristo. Jinsi ya Kristo ni ipi?, Bwana Yesu ametupatia sharti lake la mtu kuwa mwanafunzi wake ni kukaa katika Neno lake (Yn.8:31-36).
Injili inatuhakikishia kwamba uhakika wa usalama dhidi ya dhambi uko katika Neno lake. Anawaambia wafuasi wake, “Ninyi mmekuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia (Yn.15:3).
Katika ile Sala yake kuu amwambia Baba, Neno lako nimewapa, ulimwengu umewachukia kwa sababu wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu (Yn.17:14).
Tena amwambia Baba, “Uwatakase kwa ile Kweli; Neno lako ndiyo kweli. Mimi najiweka wakfu mwenyewe ili na hao watakaswe katika kweli (Yn.17:, 19).
Efe.5:25-27 yatuambia kwamba Kristo Yesu ametoa Nafsi yake makusudi alitakase na kulisafisha Kanisa lake kwa maji safi katika Neno.
N.B. Tatizo kubwa linalojitokeza ni matumizi ya karatasi. Katika ujumla wake, nafasi zilizo wazi ni sawa, kama siyo zaidi na nafasi zilizotuika.
Ebr.10:19-23 yatuhakikishia kwamba Kuhani Mkuu ametuosha miili kwa maji safi yaliyomo katika Damu yake ambaye ni Roho Mtakatifu (Yn.4:10, 14; 7:37-39) ambaye ni Neno la Mungu (Yn.6:63).
Utimilifu wote uko katika Kristo Yesu aliyekuja katika Maji na katika Damu (1Yn.5:6). Huko ni kwenda kwa jinsi ya Kristo (Kol.2:8); na ndiko kwenda kwa Roho (Gal.5:16); na ndiko kwenda kwa Hekima iliyoshuka kutoka mbinguni (Yak.3:15; 1Kor.1:24).
Nje ya hapo ni kwenda kwa hekima ya dunia na ya shetani. Na kama tulivyoambiwa katika Gal.5:17, nafsi ya mtu haiwezi kufanya inavyotaka, hekima ya dunia, hekima ya kwenda kimwilimwili ni hekima ya Mungu wa dunia hii, mpofushaji wa fikira, roho ya upotevu ifanyayo watu wapotee njia ya kumfikia Baba katika ulimwengu wake wa Roho (Efe.2:6).
UMUHIMU WA KUZINGATIA 100% ANGALISHO LA KOL.2:8-10
Angalisho la Kol.2:8-10 lapelekea kutufikisha kwenye ukweli kwamba tatizo la utumwa wa dhambi haliwezi kutatuliwa kwa taratibu za kidini za wakati wowote ule.
Taratibu za kidini kama vile Sabato, Sikukuu, Kuungama (1Mfal.8:46-50; Nehemia 1:4-11), kuombea wafu (2Mak.12:38-46) n.k. zilikwisha kuwako duniani. Lakini zote hazikufaa kitu katika kulikabili tatizo la utumwa wa dhambi.
Utatuzi wa tatizo la dhambi uko katika kuufanya mti uwe mzuri ili matunda yake yapate kuwa mazuri (Mt.12:33-35).
Yesu amekuja kumfanya mtu azaliwe katika umungu kwa upya (Yn3:3, 5). Amekuja kumshirikisha umungu kwa upya, ili mtu aweze kujilinda hata asiguswe na yule mwovu (Yn.5:18). Ili hili litimilike sharti kwenda kwa jinsi ya Kristo (Kol.2:8). Na jinsi ya Kristo ni ile iliyoelekezwa katika Yn.8:31-32, 36 na Gal.5:16.
Kwa njia hiyo mtu hupata kufikia utimilifu wote wa Mungu (Efe.3:19 na kuwa kama Mungu mwenyewe alivyo (1Yn.4:17). Hapo mtu huwa ana mti mzuri, na matunda yake huwa mazuri. Hapo mtu hawezi kutenda dhambi, kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu kwa huyo Roho wa kweli aliyemnyweshw (1Kor.12:13) kumfundisha yote kumkumbusha yote (Yn.14:26), kumwongoza katika kweli yote (Yn.16:13), kumfundisha yote (1Kor.2:10) na kumwombea kama Baba apendavyo (Rum.8:26-27).
Kwa utendaji huo wa Roho wa kweli, dhambi haitafurukuta tena katika mtu aiaminiye kazi ya Mungu pekee wa kweli katika Mwanawe Neno ambaye ni kweli (Yn.17:17).
Basi ndugu yangu! Mungu wa pekee wa kweli, Baba wa Bwana wetu Kristo Yesu na Baba yetu naakubariki wewe pamoja na ndugu wote kwa Baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa Roho ndani yake Kristo Yesu, sasa na hata milele. Amina!!!
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0714 118 428
0787 765 759
0753 298 707
chamayombe37@gmail.com

MAELEZO KUHUSU NURU NA GIZA


Maelezo yanayopatikana katika Bibilia Takatifu toleo la Iringa kuhusu aya Yn.8:12 yatuelezea kwamba Nuru na Giza ni kielelezo cha falme mbili zinazohitilafiana na kupigana; yaani ufalme wa mema unaotawaliwa na Kristo na Ufalme wa uovu unaomilikiwa na shetani.
Maelezo yanatueleza kwamba kila ufalme unajaribu kuushinda mwingine. Na kwamba watu wanagawanyika baina ya wana wa Nuru na wana wa giza kwa kadiri waishivyo. Kwa mvuto wa Nuru, Kristo au kwa mvuto wa giza shetani.
Maelezo yanahitimisha kwa kusema kwamba wana hao wote watambulikana katika vitendo vyao.
Kwa upande wa Mungu wa pekee wa kweli, Bibilia yenyewe hutuambia kwamba Mungu hutaka watu wote waokolewe na kupata kujua yaliyo kweli (1Tim.2:4).
Kwa upande wa shetani, 2Kor.4:3-4 hutueleza kwamba iwapo Injili yetu imesitirika, imestirika kwa hao wanaopotea ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini isiwazukie (wasiione) Nuru ya Injili ya Utukufu wake Kristo aliye Sura yake Mungu.
Na Yn.12:40 yatueleza “Amewapofusha macho na kuifanya mizito mioyo yao; wasije wakaona kwa macho yao, wakafahamu kwa mioyo yao, wakaongoka nikawaponya (kwa kuwaokoa).
Kumbe tuko katika mkabala wa vita vikali. Mungu wa pekee wa kweli anataka watu waijue kweli ili waokoke. Shetani yeye hataki watu waijue kweli wasije wakaokolewa na kuponywa.
Hebu, ndugu yangu, jipime mwenyewe mbele za Mungu wa pekee wa kweli ukiwa mwenye moyo wa kweli kwa utimilifu wa imani. Kama huna muda na Neno la Mungu, kama Neno la Mungu kwako ni jambo la ziada tu, au ikiwa kwako kutafuta kweli ya Mungu ni kupoteza wakati ambao umepewa na Mungu, basi tambua kwamba Yule mwovu yuko kazini kwa maangamizi yako ya milele yote.
Mbaya zaidi ni pale mtu, kwa kutumia cheo, huwa kizingiti kwa wengine kuitafuta kweli. Mtu kama huyo hujithibitisha kwamba ni mtumishi wa shetani. Kwake mtu huyo kile kiapo “Namkataa shetani, na mambo yake yote, na fahari zake zote”, ni kiapo cha uongo, unafiki na ubatili mtupu. Na ibada yenyewe huwa ni ibada ya kujisajiri kwenye ufalme na utumishi wa Shetani.
Hapo moja kwa moja zile laana zilizosemekana katika Yn.8:44 na 20:29 huwa halisi kwa mhusika. Mhusika huwa mmilikiwa wa shetani.
Hivyo mtu kuwa mtumwa wa dhambi, hasa dhambi ile kuu ya kutomwamini Mungu (Mk.11:22), dhambi ya kumfanya Mungu mwongo (1Yn.5:10) huwa ni kitu cha kawaida, si cha ajabu kwake.
Wakati uliokubalika wa kufuta usajili batili kwa shetani ndiyo sasa. Kufanya kosa siyo kosa. Kosa ni kuendelea na kosa.
Kuijua kweli ndicho Mungu anachokutaka (1Tim.2:4) na kukuagiza (Yn.8:31-32). Kamwe usimruhusu shetani aendelee kukukamata katika ujinga kwa maangamizi yako na ya wengine.
Ubarikiwe!!
LUKA ROKI MAGHALI CHAMAYOMBE
0714 118 428
0787 765 759
0753 298 707
chamayombe37@gmail.com
Mimi "Kuukulia Ukweli wa Mungu" niko katika mchakato wa kuukuli ukweli wa MUngu wa pekee wa kweli.
Mungu wa peke wa kweli akubariki kwa abaraka zote za kiroho katika ulimwengu wa Roho ndani ya Kristo Yesu {Efe. 1:3} kwa kunipokea kama nilivyo wala kuwakataza kwa namana yoyote ile wale ambao Mungu wa pekee wa kweli amewajalia Nuru ya kujiingiza katika mchakato huu ulio himizwa katika Barua ya kichungaji ya Mtakatifu Papa Yohani Paulo II aliyoipa jina "UT UNUM SINT" ikiwa na maana " ILI WAWE UMOJA"
Dira zetu za kuukulia ukweli wa Mungu kweli ni Neno la Mungu {Yn.8:31-32} na nyaraka za kichungaji za mababa { mapapa} wa kanisa kama tunavyo endelea kufundishwa na dira hizo mbili.
Mungu atuepushe na kila aina ya uzushi kutoka kwa yeyote awaye yule. MUNGU ATUBARIKI SOTE. Amina.